adriz
JF-Expert Member
- Sep 2, 2017
- 12,207
- 26,521
Moja kwa moja..
1. Kusovu past papers imekuwa dili kwa Wanafunzi
Kumekuwa na misemo maswali au mitihani inajirudia na hili ni ukweli ambao hauna shaka. Unakuta Wanafunzi pamoja na walimu wanawekeza muda wao sio kusoma kuelewa bali kusovu mitihani ya Taifa iliyopita kwa lengo kuu ni kuwa yakijirudia mwanafunzi asikose, na ni kweli mtu ambaye anayesovu pastpaper nyingi anauwezekano mkubwa wa kufaulu na vyema mitihani. Kungekuwa na utungaji makini wa mitihani kwa kupima uelewa maswali yasingeisha kiasi cha kujirudia sana na wala Wanafunzi wasingehangaika kukarira mapast papers ili wafaulu.
2. Vitu vya kusoma practicality (kwa njia ya vitendo vinasomeshwa theoretically (kwa njia ya nadharia)
Pamoja na kuwa na maabara karibia shule nyingi lakini bado unakuta vitu vingi vya kujifunza kwa njia ya vitendo bado mnapewa kwa njia ya nadharia na unakuta maabara nyingi shuleni na vyuoni zina upungufu mkubwa wa vitendea kazi au kukuta vitendea kazi duni na havitosholezi kuendana na idadi ya Wanafunzi.
Mfano unakuta mwalimu anasema tu Sodium ikiungana na element Fulani inatengeneza kitu Fulani ambacho kina rangi na harufu Fulani , na Mwanafunzi anakariri tu bila kuona reaction husika.
3. Kuvuja na kuiba mitihani
Kwa miaka mingi kumekuwa na skendo za kuvuja mitihani karibia ngazi zote za Elimu haswa vyuoni , kama elimu yetu ingekuwa inapimwa kwa uelewa na sio kukariri pamoja na kuwa na udhibiti mkali basi swala hilo lingepungua kwa kiasi kikubwa sana.
4. Kukithiri kwa matukio ya udanganyifu kwa Wanafunzi
Vyuoni watu wanafanyiana mitihani , wananunua tafiti na kughushi data.
MABADILIKO
Pamoja na kuwepo changamoto hizo juhudi mbalimbali za serikali zinaonekana katika kubadilisha mifumo mbalimbali katika utoaji wa Elimu mfano shule za misingi ,sekonadari na Advanced level Kuna mabadiliko katika vitabu vya sasa na baadhi ya mifumo ikilenga katika kupunguza na kuthibiti kadhia n hizi.
Changamoto ipo kwa upande wa vyuoni naona bado kumesahaukika sana na mambo yanaenda kienyeji..
Je , juhudi zipi zifanyike ili Elimu yetu iwe katika ubora mzuri?