Tetesi: Miongoni mwa Wabunge 19 waasi wa CHADEMA wawili kati yao ni wake za Benson Kigaila na Salumu Mwalim hoja kuwa waliapa bila baraka za chama zinaukweli?

Tetesi: Miongoni mwa Wabunge 19 waasi wa CHADEMA wawili kati yao ni wake za Benson Kigaila na Salumu Mwalim hoja kuwa waliapa bila baraka za chama zinaukweli?

Patriot missile

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2024
Posts
280
Reaction score
423
Kwa ufupi sana,

1. Huyu Kigaila anayesema Lissu ni CCM mke wake yuko Bungeni tena bila ya baraka za Chama hii kwa akili ya kawaida kabisa inawezekana kweli Kunti hakutumwa na mumewe?

2. Hata Salumu Mwalimu Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Mke wake yuko Bungeni tena bila ya baraka za chama lakini jambo hili kwa akili za kawaida kabisa inawezekanaje huyu Katibu mkuu anatafuna Posho za Bunge eti hajui mkewe aliendaje kuapa?

3. Taifa hili linafahamu fika Halima na Bulaya ni maswaiba wakubwa wa Freeman Mbowe je hoja kwamba wadada hawa waliapa bila baraka za rafiki yao mkubwa Freeman Mbowe zinaukweli?

4. Mimi nasema hawa wanawake wanaonewa bure tena nashauri Mbowe, Mwalimu na Kigaila waadhibiwe kwa makosa haya na Chama kitamke msamaha juu ya hao wanawake wote 19

5. Napendekeza wabunge hawa warudi kundini ili Maisha yaendelee ila hawa Wala rushwa waondoke na Uenyekiti apewe mtu asiye Mbowe.
 
Mimi nasema hawa wanawake wanaonewa Bure nashauri Mbowe, Mwalimu na Kigaila waadhibiwe kwa makosa haya na Chama kitamke msamaha juu yao.
Mwenyewe umeona umetoa bonge la hoja😆😃😀

CHADEMA mwaka wa nne sasa wanataka itolewe barua iliyoandikwa kwenda Kwa tume ya uchaguzi kupendekeza hao wanawake 19 kuwa wabunge wa viti maalum. Si bunge wala Tume ya uchaguzi walioweza kuonesha hiyo Barua.

Au unadhani viti maalum wanakwenda bungeni bila ya utaratibu?
 
Ule ulikuwa ni mchongo tu kati ya hawa vijana wenye wake zao na Ndugai hata barua naamini haipo.

Mke wa Naibu anaapaje bila Naibu kujua?
Huyu Kigaila ni tatizo sana pale CHADEMA
 
Ule ulikuwa ni mchongo tu kati ya hawa vijana wenye wake zao na Ndugai hata barua naamini haipo.

Mke wa Naibu anaapaje bila Naibu kujua?
Huyu Kigaila ni tatizo sana pale CHADEMA
Kwa ivo Eva alipokula tunda la mti wa kati ya Bustani Adam alijua?

Mambo ya kubashiri kwenye uhalisia ni ushirikina. Kama Kuna ushahidi si uwekwe hadharani?
 
Kwa ivo Eva alipokula tunda la mti wa kati ya Bustani Adam alijua?

Mambo ya kubashiri kwenye uhalisia ni ushirikina. Kama Kuna ushahidi si uwekwe hadharani?
Adam hakujua ila aliporudi alikaribishwa na Akala ndicho anachokifanya Kigaila na Mwalimu,

Kama mnawaondoa hawa wanawake na kuwaacha hawa Viongozi wakubwa ni makosa makubwa.
 
Kwa ufupi sana,

1. Kigaila mke wake Yuko Bungeni bila baraka za Chama hii kwa akili ya kawaida inawezekana?

2. Salumu Mwalimu Mke wake Yuko Bungeni bila baraka za chama hii kwa akili za kawaida inawezekana?

3. Halima na Bulaya ni maswaiba wakubwa wa Freeman Mbowe je hoja kwamba wadada hawa waliapa bila baraka za rafiki yao huyo zinaukweli?

Mimi nasema hawa wanawake wanaonewa Bure nashauri Mbowe, Mwalimu na Kigaila waadhibiwe kwa makosa haya na Chama kitamke msamaha juu ya hao wanawake wote 19.
mimi najua waziwazi kuwa waliruhusiwa na mbowe
 
Kwa mujibu wa sheria, mtu akiishafikisha the age of majority, ambayo kwa Tanzania ni umri wa miaka 18, then, kila mtu ataubeba mzigo wake mwenyewe, mume hawajibiki kwa makosa ya mkewe au mke hawajibiki kwa makosa ya mumewe, na kupitia sheria ya ushahidi ihusiyo mahusiano ya uwajibikaji, fiduciary relationship, watu wenye mahusiano hayo, wana kinga ya kutoohojiwa kijinai, kutoa ushahidi dhidi ya jinai ya wenza wao, iitwayo vicarious liability.

Hivyo hawahusiki na vitendo vyao vya kisiasa, ila kwa vile they are sharing the ssma bed, kupitia kanuni ya karma, viongozi wote wa CC ya Chadema, waliojilia mzigo kwa hao wanawake 19, kisha kukaa ndani ya CC na kuwatimua, wataadhibiwa na karma!.

Kwenye bandiko langu Makamanda walioigharimia CHADEMA kwa machozi, jasho na damu, leo ni wakuitwa wasaliti? Karma Haitawaacha salama, itawatandika tu nilisema
Wanabodi,

Mimi ni muumini wa kitu kinachoitwa "Karma", na nimekuwa nikikihubiri mara nyingi tuu humu jukwaani kuwa karma ndio the power pekee ambayo hutoa hukumu ya haki hapa duniani, kwenye karma, mtu unaadhibiwa au kuhukumiwa kwa mawazo, maneno na matendo yako, karma haina mswalie Mtume, wala haujui nani ni nani!, kwenye hukumu ya karma, inatembeza bakra za kutosha na adhabu kubwa ya mwisho ya karma huwa ni kula kichwa!. "The Power of 'Karma'- Ndio Hukumu Pekee ya Haki Kamili Hapa Duniani!, Unahukumiwa kwa Matendo Yako!

Leo kikao cha CC ya Chadema, kinakaa as usual, kama kawaida yao, kikao hiki huwa kinakaa as a Kangaroo court!, kama kilivyokuwa kinakaa huko nyuma na kutoa hukumu za kikangaroo za ajabu ajubu ikiwemo timua timua, ambazo karma za hukumu hizo, zinakuja kuigharimu Chadema mbele ya safari, tatizo, wakati wa karma payback time unapofika, when karma strikes back,
no one remembers, hakuna anayekumbuka kuwa kinachotokea ni hukumu ya Karma ya matendo yake ya nyuma!. Tatizo la karma, unaweza kufanya kitu kidogo, tuu, kwako ukakiona ni kidogo, it's nothing and insignificant, lakini when karma takes its toll, mapigo ya karma yanayokushukia ni mapigo makubwa in three folds, kulinganisha na ulichotenda, hadi huwezi kukumbuka ulifanya nini kustahili kinachokupata!. Ila pia, anayehukumiwa pasipo haki, karma pia huwa ina mtake care, na kumu elevate kwa kumuweka mahali pa juu palipoinuka, machoni pa watesi wake!.

, CHADEMA, Msishangilie, Mkajisahau, Jiandaeni kwa "Karma!"
haiwezekani watu na makamanda wameipigania Chadema kwa kuigharimikia kwa Machozi, Jasho na Damu, halafu leo uje uwaite wasaliti na kuwatimua kama mbwa!, kamwe Karma haiwezi kuacha salama Chadema!. Ndani ya majina yale 19 ya wabunge wa viti maalum wa Chadema, walioapishwa, wabunge 5 ni wake au 'vidumu' vya wajumbe wa CC ya Chadema ambao sio vile 'vidumu' vya 'mpango kando', no!, ni vidumu vya cohabitation, mnaishi nyumba moja, mnalala chumba kimoja, kitanda kimoja!, huku mkiishi katika dhana ya ndoa, na kila mtu anawatambua kama mke na mume!, haiwezekani mwenza wako, akaibukia kwenye majina ya viti maalum bila wewe kujua, kisha akaamkia Bungeni Dodoma kuapishwa bila wewe, kujua!, namhurumia sana KM. JJ. Nnyika ni mtu muadilifu sana, lakini hajui, the games people plays
P
 
Kwa mujibu wa sheria, mtu akiishafikisha the age of majority, ambayo kwa Tanzania ni umri wa miaka 18, then, kila mtu ataubeba mzigo wake mwenyewe, mume hawajibiki kwa makosa ya mkewe au mke hawajibiki kwa makosa ya mumewe, na kupitia sheria ya ushahidi ihusiyo mahusiano ya uwajibikaji, fiduciary relationship, watu wenye mahusiano hayo, wana kinga ya kutoohojiwa kijinai, kutoa ushahidi dhidi ya jinai ya wenza wao, iitwayo vicarious liability.

Hivyo hawahusiki na vitendo vyao vya kisiasa, ila kwa vile they are sharing the ssma bed, kupitia kanuni ya karma, viongozi wote wa CC ya Chadema, waliojilia mzigo kwa hao wanawake 19, kisha kukaa ndani ya CC na kuwatimua, wataadhibiwa na karma!.

Kwenye bandiko langu Makamanda walioigharimia CHADEMA kwa machozi, jasho na damu, leo ni wakuitwa wasaliti? Karma Haitawaacha salama, itawatandika tu nilisema

P
Asante sana P,
 
Ili nikuelewe,weka nakala ya vyeti vya ndoa hapa.
Nakala ya cheti cha kuzaliwa, cheti cha ubatizo, cheti cha ndoa, na mikataba binafsi ya watu, viko chini ya personal info, vinalindwa na sheria ya the right to privacy, ila kwa sheria yetu hata dhana tuu ya ndoa, cohabitation, ni ndoa! huyo mwenza ni anahesabika ni mke.
P
 
Kwa ufupi sana,

1. Huyu Kigaila anayesema Lissu ni CCM mke wake yuko Bungeni bila baraka za Chama hii kwa akili ya kawaida kabisa inawezekana?

2. Hata Salumu Mwalimu Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Mke wake yuko Bungeni bila baraka za chama lakini jambo hili kwa akili za kawaida kabisa inawezekana?

3. Taifa hili linajua fika Halima na Bulaya ni maswaiba wakubwa wa Freeman Mbowe je hoja kwamba wadada hawa waliapa bila baraka za rafiki yao huyo zinaukweli?

4. Mimi nasema hawa wanawake wanaonewa bure nashauri Mbowe, Mwalimu na Kigaila waadhibiwe kwa makosa haya na Chama kitamke msamaha juu ya hao wanawake wote 19

5. Napendekeza wabunge hawa warudi kundini ili Maisha yaendelee ila hawa Wala rushwa waondoke na Uenyekiti apewe mtu asiye Mbowe.
UWT tumie akili, kwanini kesi huwa inatajwa mara moja kwa mwaka?
 
Back
Top Bottom