Tetesi: Miongoni mwa Wabunge 19 waasi wa CHADEMA wawili kati yao ni wake za Benson Kigaila na Salumu Mwalim hoja kuwa waliapa bila baraka za chama zinaukweli?

Mimi G4N naapa kwamba kuanzia leo sitashabikia chama chochote cha siasa. Hii inakuja baada ya kujiridhisha kuwa watu wote wapo ktk vyama vya siasa kwa maslahi na malengo yao binafsi.
Hapana Mkuu ,tuendelee kupiga kelele ili tuwakomboe vijana waliotekwa na CDM.
 
Kinachoshangaza sana ni jinsi Bunge na Serikali walivyowang’ang’ania hao wabunge feki muda wote huu kinyume cha katiba na sheria pamoja na CHADEMA kuchukua hatua kamili za kitaasisi kuwaondolea uanachama! Ni kituko.

Hii bla bla ya kuwa wenza wa viongozi ingekuwa na mashiko kama kilichokuwa chama chao kingekuwa kingekuwa kimefanya taratibu rasmi za kitaasisi kuwapeleka huko bungeni na kutambua rasmi uwepo wao huko.

Naielewa vizuri hoja ya Paschal Mayala kuhusu KARMA kwa wote wanaoshukiwa kufanya uhuni katika suala hili. LAKINI si huu ujinga unaopigiwa kelele zisizo na mantiki na machawa wa CCM na viongozi yake.
 
Uaneni bwana hamna maana nyie
Yaani unaona kuuana ni jambo la kawaida?

Watu wa aina yako ndiyo walimchagua Hitler kuwa kiongozi wao. Watu wanaoona uhai wa wengine hauna maana kwa kuwa tu hawakubaliani nao wanaweza kuwa na mojawapo ya sifa hizi;

1. Waoga
2. Wabinafsi
3. Katili
4. Hawajui thamani Yao
5. Wanafikra za kitumwa
6. Wana wivu kwa mafanikio ya wengine.
7. Wanafiki
8. Wazembe
9. Hawana akili
10. Mazwazwa
 
Sasa Machadema mna faida gani?
 
Paskali
Hiyo karma ni imani yako na mimi nina yangu. Tuachane nayo na tuangalie sheria inasemaje. Karma ni imani ya Wahindu ambayo haina mantiki wala mashiko. Hata muuaji anaweza kuiambia mahakama kuwa ni karma imemtuma kuua kwa hiyo yeye hana makosa!! Wewe Paskali kama wakili msomi unaweza kutoa hoja ya Karma mahakamani?
 
Mchongo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…