Mikopo Consultant
JF-Expert Member
- Oct 28, 2024
- 2,375
- 4,784
Sensema Wananzengo
Jukwaa lisichukuliwe kama jukwaa la mbao tu - lile la kampeni, jukwaa ni neno lenye uwanda mpana, kuanzia jukwaa la mbao, jamii forum, twitter, redioni, youtube n.k hayo yote ni majukwaa ya kukutana na umma.
Hii sio miongozo rasmi - kwamba sijui nimenukuu kutoka kwenye kitabu gani huko, hii ni miongozo tu ambayo binafsi nimeichunguza kwa kufuatilia mawasilisho ya viongozi mbalimbali kwa umma.
Kiongozi anayeweza kuwa gwiji wa hizi dondoo na nyinginezo ambazo mtaziweka humu, atakuwa ametatua matatizo mengi sana, kwani matatizo mengi hutokea kwa viongozi wengi kukosa kuwa 'King Makers' kwenye majukwaa - kushindwa kuzi'master' dondoo za namna ya kuongea na umma ukiwa kwenye jukwaa.
Kuna baadhi ya viongozi mnaowafahamu, walikuwa/ni magwiji kwenye huu uwanda wa kusema na watu, hawa ni: J.K Nyerere, Bill Clinton, Bashar Al Assad, Vladmir Putin, Askofu Yuda Thadei Ruwaichi, Tundu Antipas Lissu, kwa uchache wao.
Siku Askofu Gwajima anahutubia wananchi, nilikwisha ziandaa hizi dondoo. Nimeisikiliza hiyo hotuba jana Jumapili na nikagundua kwamba Askofu Gwajima alicheza vizuri kwenye baadhi ya dondoo. Na sote tunajua matokeo ya hotuba ile, Taifa lilishangilia 'wa wa waaaa', na wameipa hadhi ya daraja 'A', japo kuna mahali naona kama alipoteana pale aliposema, 'majeshi yawe na makampuni', haikuifanyia tafiti vema hii hoja.
Dondoo zenyewe ni hizi hapa, na kwasababu sijafanya marejeo kutoka kwenye kitabu chochote, itapendeza kama tutaweza kupata nyongeza. Nadhani kuwafundisha viongozi kujua kusema na jukwaa ni kitendo kilichojaa umungu ndani yake, hivo, karibuni nyote.
1. Usichanganye lugha unapoongea (pendelea kutumia lugha ya wazawa). Huwa inatia kichefuchefu kuongea kiswahili na kutupiamo maneno ya kiingereza. Mwalimu wangu mkuu kwenye hili ni Askofu Yuda Thadei Ruwaichi. Amenifanya ninunue kamusi ya Kiswahili ya Bakita na kila wiki nitahakikisha natafuta kumsikiliza kupitia 'Youtube'. Tundu Lissu bila shaka anafuata, anaongea vema kwa Kiswahili, sema uwakili labda unamfanya kutupiamo Kiingereza kidogo, ila haimuondolei daraja A kwenye hili.
2. Heshimu Utu wa Mtu - hata kama mtu ni jambazi, usitumie neno 'lijambazi' wakati unavyoongea na umma. Usiutweze utu wa binadamu. Hapa utaona ni kivipi watu walikereka kwa Rais Samia Suluhu kutumia neno 'lijitu' kwenye hotuba yake.
Hoja hii ina muendelezo wake; Inatia kinyaa kuharibu na kutolipa jina la mtu heshima. Mzilankende, Jiwe, badala ya Hayati Magufulu; Mama Samia, Mama Abdul, badala ya Rais Samia Suluhu. Haijalishi unamchukia mtu kiasi gani, unavyosema na umma, toa heshima ya jina la mtu bila kuongeza wala kupunguza chumvi.
3. Mwiko kutamka sehemu za siri za mwanamke au mwanaume - utawafanya watu kucheka ila watakuona wewe ni punguani (makosa alikuwa akifanya Hayati Pombe Magufuli).
4. Elewa haki jumla za binadamu, ziwe kwenye lipsi zako, usizivunje kwa maneno. Hapa nadhani tunaweza kufanya marejeo kwenye hotuba za Hayati Magufuli, ambazo alikuwa anazikiuka waziwazi haki za binadamu kwa kuziongea, na ilikuwa inatia kinyaa.
5. Elewa uwepo wa 'Jumuiya ya Kimataifa' kwa ujumla wake, usitake kujionesha wewe ni shujaa kwa kutweza nguvu ya Jumuiya ya Kimataifa mbele ya jukwaa lenye umma. Jumuiya ya Kimataifa hawakujiita hilo jina pasipo kujua mamlaka na nguvu yao ni nzito kiasi gani. Ukiwatweza kwa maneno watatafuta namna ya kukuadhibu kwa wakati muafaka.
6. Kuwa objective, ukiwa na data inapendeza zaidi, kwasababu utakuwa unaongea kwa facts - hapa Vladimir Putin na Bashar Al Assad wapo vizuri sana. Viongozi wakubwa huandaa hotuba zenye facts. Hapa namsifu Askofu Gwajima kwa kutendea haki hii dondoo, kwa muda nikadhani namsikiliza Vladmir Putin akihojiwa na mwanahabari nguli, Tucker Carlson, ambapo Putin anatiririka facts.
7. Achana kabisa na hoja za mafungu - hizi ni zile hoja za kuokoteza maneno hapa na pale, halafu unayachukua na kukusanya pamoja ukijua kwamba unaongea vitu vya maana kumbe unaongea 'ushubwada'. Hili ni tatizo hata hapa jukwaa la jamii forum, hoja za mafungu zinatutesa sana.
8. Usiongee general, ongea specifically - usiseme 'tumepiga hatua kubwa kama nchi kwenye kutekeleza ujenzi wa madarasa', wewe tuambie specifically ulitaka kujenga mangapi halafu ukafanikiwa kujenga mangapi. Usituletee hizo hadithi zako za kupiga hatua, maana hata mtoto mdogo pia anaweza kupiga hatua.
9. Heshimu mahojiano ya papo kwa papo na waandishi wa habari. Jitenge na majibu ya hovyo na yenye utata hata pale unapochokonolewa. Hapa mimi huwa nakumbuka swali konki la mwandishi Pascal Mayalla kwa Hayati Pombe Magufuli, lakini akajikuta anaishia kutwezwa jina lake kwa kuambiwa 'Mayalla' kwa Kisukuma ni njaa. Ilikuwa ni irrelevant response na ikapelekea kwamba ionekana Mwandishi Mayalla amemkosea Rais, na hii ikapelekea 'Washenzi' kama alivyowatamka Mayalla, kumshughulikia vilivyo baada ya kuuliz lile swali, ambalo anapenda kusema ni konki.
10. Usitake kuwa msemaji wa kila jambo - Ukiona swali ni gumu sana na unatakiwa kulitolea ufafanuzi, pendelea zaidi kuamini mamlaka nyingine za kiuongozi. Saa nyingine na mara nyingi pendelea kusema, 'Hii tuwaachie wengine'.
Kama wewe ni mwanasiasa, jikite sana kwenye siasa na uelewe vema mambo ya siasa. Inapotokea umemwagwa kwenye uwanda ambao sio wako, kama habari za mambo ya dini, utabibu, usalama, diplomasia n.k, japo unaweza kuwa na ujuzi wa mambo hayo ila unatakiwa kujiepusha na kutoa maoni yenye utata.
Hili boko alilitoa Hayati Pombe Magufuli kipindi kile cha janga la Uviko-19, alivaa viatu vya kitabibu isivyotakiwa, alitaka kuwa msemaji wa kila kitu, na nyinyi ni mashahidi ni jinsi gani ilikuwa inatia kinyaa na kukera.
Kwisha kusema hayo, mimi nafunga ukurasa wa fikra zangu kwenye hizo dondoo kumi, lakini nafungua ukurasa wa majadiliano kutoka kwenu, ili tupate dondoo nyingi zaidi.
Pia mniombee nipo safarini na barabara ni mbovu kweli kweli. Mpaka najiuliza, hivi ni kwanini tu tusiiuze tu bandari ya Daslam na haya mapori ili tujenge hii barabara?? Naongelea kwa mfano yani, tukifanya hivo itakuwaje??
Wasalaam
MC