Miongozo ya utunzaji wa Kadet isipauke haraka

Miongozo ya utunzaji wa Kadet isipauke haraka

Captain mopao

Senior Member
Joined
Feb 25, 2021
Posts
133
Reaction score
384
Hii ni miongozo kwa wanaopenda kuvaa kadeti, fanya haya ili isipauke mapema.

☆Tumia sabuni ya kipande unapoifua usitumie sabuni ya unga

☆Igeuze nje ndani unapoifua

☆Usiianike kwenye jua anika kwenye kimvuli

☆Usiipige pasi ikibidi ipige ikiwa imegeuzwa

☆Usiiloweke muda mrefu kwenye maji

☆Usiikamue maji unapoianika iache ikiwa na maji

☆Usitumie maji chumvi katika kufua

Hizo ni baadhi ya sheria chache kati ya nyingi, kuifanya nguo yako isichakae mapema
Nawasilisha ndugu zangu.

1621417621692.png

Hizi ni sheria kwa wanaopenda kuvaa kadeti, fanya haya ili sipauke mapema

☆tumia sabuni ya kipande
unapoifua usitumie sabuni ya unga

☆igeuze nje ndani unapoifua

☆usiianike kwenye jua anika kwenye kimvuli

☆usiipige pasi ikibidi ipige ikiwa imegeuzwa

☆Usiiloweke muda mrefu kwenye maji

☆usiikamue maji unapoianika iache ikiwa na maji

☆usitumie maji chumvi katika kufua

Hizo ni baadhi ya sheria chache kati ya nyingi, kuifanya nguo yako isichakae mapema
Nawasilisha ndugu zangu
Hizi sheria zinahusu kadeti zinazouzwa kwa mafungu😆😆😆
 
Vipo vya kunwaga. Wewe nenda kwenye maduka yanayouza vitambaa vya ukweli, maeneo ya Posta au hata Karikoo.

Khimji ni muuzaji maarufu wa vitambaa, duka lake lipo makutao ya barabara ya Morogoro na Samora
Kadeti Ni ya spesho Tena ile OG.lkn ya kushona barazani Wala siwezi kujaribu. Itakuwa Utopolo
 
Mimi nina kadeti tatu zina zaidi ya miaka 3. Masharti hayo siyafuati, lakini bado ziko bomba, isipokuwa moja ndio imeanza kupauka.

NB: Kadeti hizi nilinunua kitambaa dukani na kushonesha kwa fundi.
Mkuu kitambaa gani hicho
Naomba hata picha aise
 
Kadeti Ni ya spesho Tena ile OG.lkn ya kushona barazani Wala siwezi kujaribu. Itakuwa Utopolo
Sawa ndugu. Maisha ni kupanga na kupanga ni kuchagua......... Panga na chagua kile unachoona kinakufaa. Lakini kumbuka hata hizo zinazoitwa kadeti original nazo zimeshonwa na wanadamu kwa kutumia machine (cherehani) za kisasa, ambazo tunazo pia hapa Bongo.
 
Mkuu kitambaa gani hicho
Naomba hata picha aise
Nenda kwenye duka la Mhindi anaitwa Khimji, lipo kwenye makutano ya barabara ya Morogoro na Samora. Ni muuzaji maarufu wa vitambaa vya suruali vya kila aina na ubora tofauti Dar. Vyangu vya kadeti nilivyoshonesha suruali nilinunua hapo.

Uzuri wa suruali za kushonesha mwenyewe fundi anashona kutokana na maelekezo yako na vipimo vinachukuliwa ninavyokuhusu. Mfano kama kiuno chako ni nchi 33, atakushonea kwa kipimo hicho. Suruali nyingi za special hazina vipimo vya namba tasa, wanashufwa.
 
Vipomo sio ishu

Mimi nanunua nguo kwa kuangalia kitambaa na fasheni tu

Nguo hata ikiwa bwanga sio ishu ukipeleka kwa fundi inakuwa safi tu

Nguo ikiwa ndogo ndo tatizo......
 
Back
Top Bottom