Miongozo ya utunzaji wa Kadet isipauke haraka

Miongozo ya utunzaji wa Kadet isipauke haraka

K
Hii ni miongozo kwa wanaopenda kuvaa kadeti, fanya haya ili isipauke mapema.

☆Tumia sabuni ya kipande unapoifua usitumie sabuni ya unga

☆Igeuze nje ndani unapoifua

☆Usiianike kwenye jua anika kwenye kimvuli

☆Usiipige pasi ikibidi ipige ikiwa imegeuzwa

☆Usiiloweke muda mrefu kwenye maji

☆Usiikamue maji unapoianika iache ikiwa na maji

☆Usitumie maji chumvi katika kufua

Hizo ni baadhi ya sheria chache kati ya nyingi, kuifanya nguo yako isichakae mapema
Nawasilisha ndugu zangu.

Kama hivi ukiwa unakaa maji chumvi unafanyeje?!
 
Mimi nina kadeti tatu zina zaidi ya miaka 3. Masharti hayo siyafuati, lakini bado ziko bomba, isipokuwa moja ndio imeanza kupauka.

NB: Kadeti hizi nilinunua kitambaa dukani na kushonesha kwa fundi.
Zitakuwa zinatofautiana na za mleta Uzi (kwenye picha pale) bila shaka
 
Back
Top Bottom