Getrude Mollel
JF-Expert Member
- Apr 26, 2022
- 270
- 362
Kuna matukio yametoka hivi karibuni kwenye medani yetu ya siasa hapa nchini, matukio ambayo yamevunja sana mioyo ya wafuasi wa Chama Kikuu cha Upinzani, CHADEMA.
Matendo ya chama yanaweza kuimarisha imani ya wanachama/wafuasi ya wanachama kwa chama chao, au kuzorotesha kabisa. CHADEMA kwa matendo yenu ya hapa na pale ambayo bila shaka mnafanya bila mkakati wala kufanya tafakuri, baada ya uchaguzi wa 2025 mtajikuta mmepoteza sifa ya kuwa Chama Kikuu cha upinzani.
Matukio yenyewe ni kama yafuatayo
1. Kitendo cha Lissu kurudi na kuondoka Tanzania
Fikiria ile hamu waliyokuwa nayo na kiongozi wao alipokuwa Ubelgiji. Siku amerudi watu walikwenda kumpokea na kumlaki kwa mahaba na mawada. Ila baada ya muda mfupi tu pasi na kuwa na sababu za msingi ameondoka zake na kurudi Ubelgiji. Kitendo hiki kimevunja sana mioyo ya wanachama wa UFIPA.
2. Kupokea ruzuku waliyoikataa
"Tukipokea ruzuku ni sawa na kukiri kwamba uchaguzi wa 2020 ulikuwa wa haki na halali" - Mbowe. Mbowe alinukuliwa akitamka haya maneno, na maneno haya yaliwapa nguvu sana wanachama wa Chadema. Ila katika hali ya sintofahamu na kushangaza zaidi, UFIPA bila haya wala soni, wamepokea ruzuku hiyo ya zaidi ya Shilingi milioni 800 za Kitanzania. Kitendo hiki kimesigina zaidi mioyo ya watu wa UFIPA.
3. Rais Samia Suluhu kukubali kuwa mgeni Rasmi katika shughuli ya BAVICHA
Ndani ya CHADEMA wapo separatists ambao hawataki hata kidogo kuona kuna muingiliano katika ya chama chao na serikali. Hii imewachoma sana kundi hilo. Mfano Mdude ni watu wa aina hii. Rais Samia Suluhu anatumia 'Soft Power' kupata anachotaka kutoka Chadema, hatumii nguvu na mabavu kama mtangulizi wake.
4. Lema kutusi VICOBA na Bodaboda
Wengi wako mtandaoni kuitetea kauli ya Lema kwamba alikuwa sawa kwenye matamshi yake dhidi ya bodaboda na wanawake wanaoshiriki VICOBA. Kauli hii kutoka kwa Lema haikutegemewa kabisa na wafuasi wa chadema lakini hata kwa watanzania ambapo wanafuatilii siasa. Kauli za Lema za kejeli na dharau kwa bodaboda na watu wa vicoba zimeacha madoa kwa watu wa makundi mbalimbali kwenye jamii..
5. Kujitoa kuwahoji akina Halima Mdee na wenzake.