Hawa hawa serikali za mitaa ndiyo huwa wanasubiri mkuu wa mkoa husika atangaze usafi kwa kila kaya ndio wao waanze kuhimiza wananchi mkuu wa mkoa akilega lega na wao wanapotezea, wao kazi yao kuomba elfu 2 ya muhuri tu kwa wananchi, yn Afrika wacha tu wazungu watutukane cz watu hatupo committed kabisa tumeweka mbele rushwa kila kona wkt tuna wajibu wa kubadilika ili kuendana na kasi ya maendeleo ya dunia ya sasa.
Serikali kupitia dmdp imejenga barabara lukuki kila mtaa kilichobaki ni wananchi kupitia serikali za mitaa kuhimizwa kufanya usafi wa barabara zetu lkn kinyume chake barabara zinajaa mamichanga Lundo na wakati mwingine magari makubwa yenye shehena yanapita kwenye barabara hizo hizo na kuharibu kabisa barabara. Wacha niishie hapa cz huu uzi wa usafi nitaufungua baada ya uchaguzi mana saizi kila mtu anajifanya yuko bize na uchaguzi unafki wa mwafrika umetapakaa kila kona ngj nisubiri uchaguzi uishe.