Mipango ya kuwazuia Dr Slaa na Lowassa kugombea Urais yaiva.

Mipango ya kuwazuia Dr Slaa na Lowassa kugombea Urais yaiva.

Hakuna uhusiano wowote kati ya Ubunge na Urais!Kama kweli kuna kipengeie cha kipuuzi kama hicho kwenye rasimu basi Watz watumie mabaraza ya Katiba kukataa upuuzi huu.!
 
JUMAPILI, JULAI 21, 2013 08:08 NA GABRIEL MUSHI, DAR ES SALAAM

*Rasimu kutumika kuwaondolea sifa ya kugombea urais
*Yumo pia Membe, Magufuli, Sitta, Zitto na Wassira




MKAKATI wa kuwaengua vigogo wanaotajwa kung'ang'ania kugombea nafasi ya Urais katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 sasa umebainika, MTANZANIA Jumapili linaripoti.

Kwa mujibu wa uchunguzi wa kina uliofanywa na gazeti hili, mkakati huo ambao umelenga kuwang'oa viongozi hao, unadaiwa kutekelezwa na baadhi ya wanasiasa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Rasimu ya Katiba Mpya, iliyotolewa hivi karibuni na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.



Imeelezwa kuwa kupitia Rasimu hiyo ya Katiba Mpya, kuna vipengele vilivyopenyezwa kwa nia ya kuwabana watu fulani fulani ndani na nje ya CCM ambao wanatajwa kuusaka ukuu wa dola mwaka 2015 na chama hicho hakitaki kuona wanakuwa kikwazo dhidi yake.Mtoa habari wetu ndani ya CCM alilidokeza gazeti hili kuwa vipengele hivyo ambavyo vimewekwa kama mtego, ni vile vinavyotaja sifa za mgombea Urais na mgombea Ubunge.




Bernard Membe

Kwa mujibu wa taarifa zilizotufikia, kutokana na hilo, baadhi ya wanasiasa ndani ya CCM kwa makusudi wameamua kuufanya mjadala kuhusu serikali tatu kuwa mkali, ili kuzuia mjadala mpana katika masuala mengine.

Kipengele ambacho kama kikiachwa bila kufanyiwa marekebisho kinaweza kuwabana wanasiasa wengi ndani na nje ya CCM wanaotajwa kuwania Urais 2015 ni pamoja na kile cha Sura ya Saba, ambacho kinazungumzia Serikali ya Jamhuri ya Muungano kuhusu Serikali, Rais na Makamu wa Rais, katika sehemu ya kwanza C kwenye kipengele cha 75 (E) kinachozungumzia sifa za Rais kimeeleza kuwa mtu atakuwa na sifa ya kuchaguliwa kushika nafasi ya madaraka ya Rais wa Jamhuri ya Muungano ikiwa: anazo sifa za kumwezesha kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa Katiba hiyo.

Wakati ikiwa hivyo katika sifa za kuwania nafasi ya Rais, kwenye Rasimu hiyohiyo kipengele cha sifa za kuwania nafasi ya Ubunge kilichopo katika sura ya tisa, sehemu ya pili (A) inayozungumzia kuhusu uchaguzi wa wabunge, katika kipengele cha (2a) kimeeleza kuwa mtu hatakuwa na sifa za kugombea/ kuchaguliwa kuwa Mbunge ikiwa mtu huyo aliwahi kuwa Mbunge kwa vipindi vitatu vya miaka mitano.

Kutokana na hilo, ni wazi kuwa viongozi au vigogo waliowahi kuwa wabunge kwa vipindi zaidi ya vitatu vya miaka mitano hawatakuwa na sifa za kugombea Urais kwa sababu tayari kipengele cha sifa za kuwania Urais kimetaja kuzingatia sifa za mgombea ubunge.

Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na gazeti hili, umebaini kuwa vigogo karibu wote ndani na nje ya CCM wanaotajwa kutaka kuwania nafasi ya Urais watakuwa wamepoteza sifa za kuwania nafasi hiyo endapo kipengele hicho kitaachwa bila kufanyiwa mabadiliko.

Vigogo hao wanaotajwa kutoka CCM ni Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.

Wengine ni Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi na Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba, wakati kutoka Chadema ni Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willbroad Slaa na Zitto Kabwe.

Watakaokuwa wametupwa nje
Kulingana na sifa zinazotajwa kwenye kipengele hicho, viongozi wanaotajwa kutaka kuwania nafasi hiyo lakini watakuwa wamegonga mwamba ni pamoja na wafuatao;

Edward Lowasa ambaye aliwahi kuwa Waziri Mkuu kwa muda wa miaka miwili na hadi sasa ni Mbunge wa Monduli kupitia CCM, ameshika nafasi hiyo kwa vipindi vitano vya miaka 25 kuanzia mwaka 1990 hadi sasa, moja kwa moja atakuwa amepoteza sifa ya kuwania Urais, kwani tayari amezidi vipindi vitatu vya kuwa mbunge.

Samuel Sitta, ambaye ni Mbunge wa Urambo Mashariki (CCM), ameshika nafasi hiyo kwa vipindi sita kwa muda wa miaka 30, kuanzia mwaka 1975 hadi 1995 na 2005 hadi sasa, naye pia atakuwa amepoteza sifa.

Dk. John Magufuli, ambaye ni Mbunge wa Chato (CCM) kwa vipindi vinne vya miaka 20 kuanzia mwaka 1995 hadi 2015, naye atakuwa ameshapoteza sifa, kwani amezidi vipindi vitatu.

Bernard Membe, ambaye pia ni Mbunge wa Mtama (CCM) naye atakuwa ametupwa nje, kwani hadi sasa ameshika nafasi hiyo ya Ubunge kwa vipindi vitatu vya miaka 15 kuanzia mwaka 2000 hadi 2015.

Dk. Willborad Slaa, atakuwa ametupwa nje ya ulingo kwani amewahi kutumikia vipindi vitatu vya Ubunge kunzia 1995 hadi 2010 katika Jimbo la Karatu kwa kupitia Chadema.

Zitto Kabwe ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, atakuwa ametimiza sharti la kuwa mbunge kwa vipindi viwili, lakini atagonga mwamba katika sharti la umri, kwani atakuwa hajatimiza umri wa miaka 40 kama rasimu ilivyoendelea kupendekeza, badala yake atakuwa na umri wa miaka 39.


Waliosafishiwa njia
Dk. Harrison Mwakyembe, ambaye ni Mbunge wa Kyela (CCM) ameshika nafasi hiyo vipindi viwili vya miaka 10 kuanzia mwaka 2005 hadi 2010.

Dk. Emmanuel Nchimbi ambaye ni Mbunge wa Songea Mjini (CCM) ametumikia nafasi hiyo kwa kipindi kimoja cha ubunge wa jimbo kuanzia mwaka 2010 hadi sasa.

Januari Makamba, ambaye ni Mbunge wa Bumbuli (CCM) amedumu kwa kipindi kimoja kuanzia mwaka 2010 hadi sasa hivyo atakuwa na sifa za kuwania urais.

Freeman Mbowe, ambaye ni Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema na Mbunge wa Hai, naye atakuwa na sifa ya kuwania nafasi hiyo, kwani atakuwa ametumikia nafasi hiyo kwa vipindi viwili kwa miaka 10 kuanzia 2000 hadi 2005 na 2010 hadi sasa.

Suala la Urais limezua mjadala mkubwa ndani na nje ya CCM, baadhi wakikomoana kuhakikisha mwingine hapiti kwenye nafasi hiyo. CCM ndicho kinachoonekana kuathirika zaidi, kwani jambo hilo tayari limesababisha makundi yanayosigana.

 
slaa ni janga la taifa ataleta udini.iko kipengele poa kwel 2
Udini upi? Zaidi ya huu wa Kikwete anayejeruhi na kuwaua wachungaji, mapadre na hata kuwaua?
Tanzania itamkumbuka muuaji huyu milele maana hajatokea na wala hatatokea muuaji wa kiwango chake; kuanzia viongozi wa kikristo, wanahabari, wanasiasa hadi watoto wasio na hatia!
Mungu ailaani CCM hadi kizazi cha kumi.
 
Ni kifungu kinachopingana na misingi ya kikatiba hivyo hakina nafasi. Ondoa wasiwasi.
 
mmh kwa kweli lowasa na slaa watawaumiza sana ila kati yao mmoja lazima awe rais 2015
 
Huu sasa ni umbea usio na maana.Katiba kama ikipita inaanza lini kutumika effectively?Itarudi nyuma au itaanzia hapo hapo itakpotajwa?Tuache kupotosha.
 
Kifungu cha 75 cha Rasimu ya Katiba Kinasema hivi:

Sifa za
Rais
75. Mtu atakuwa na sifa ya kuchaguliwa kushika nafasi ya

madaraka ya Rais wa Jamhuri ya Muungano ikiwa:
(a) ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa
Katiba hii na sheria za nchi;
(b) ni mwenye akili timamu;
(c) angalau mmoja kati ya wazazi wake ni raia wa kuzaliwa wa
Jamhuri ya Muungano;
(d) wakati wa kugombea, ana umri usiopungua miaka arobaini;
(e) anazo sifa za kumwezesha kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri
ya Muungano kwa mujibu wa Katiba hii;
(f) anayo angalau shahada ya kwanza ya chuo kikuu
kinachotambuliwa kwa mujibu wa sheria za nchi;
(g) ni mwanachama na mgombea aliyependekezwa na chama cha
siasa au mgombea huru;
(h) sera zake au sera za chama chake si za mrengo wa kuligawa
Taifa kwa misingi ya ukabila, udini, rangi au jinsia;
(i) ni mwadilifu na anafuata maadili ya Taifa;
(j) mwenendo wake binafsi hautiliwi shaka na jamii;
(k) hajatiwa hatiani kwa kosa lolote la jinailinalohusu kukosa
uaminifu; na
(l) katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya Uchaguzi
Mkuu hajawahi kutiwa hatiani katika Mahakama yoyote kwa
kosa lolote la kukwepa kulipa kodi yoyote ya Serikali.


Naomba mnisaidie hicho kipengele anachokisema Malemo kwa mujbu wa Gazeti la Mtz ni kipi? au ni katika Rasimu ya Pili?

Mkuu kipengele chenye urata ni (e) Angalia sasa sifa za kuwa mbunge.Ni yule ambaye hajatumikia vipindi 3 vya ubunge
 
2015 for Lowassa, wengine wote ni wasindikizaji na wanatekeleza wajibu wao wa kikatiba

Acha presha yeye ndo atakua mshindikizaji tena ili awe hata wa pili itabidi mtumie nguvu za ziada yani watu wamechoshwa na polojo nimabadiliko tu.
 
Acha presha yeye ndo atakua mshindikizaji tena ili awe hata wa pili itabidi mtumie nguvu za ziada yani watu wamechoshwa na polojo nimabadiliko tu.
2015 Vote for Lowassa, vote for Hope
 
Mkuu kipengele chenye urata ni (e) Angalia sasa sifa za kuwa mbunge.Ni yule ambaye hajatumikia vipindi 3 vya ubunge

Nimekusoma mkuu, kweli hapo kuna ukimya na utatanishi. Ambalo sina uhakika nalo nikama katiba inafanya kazi kwa kurudi nyuma (retrospectively)
 
Kifungu cha 75 cha Rasimu ya Katiba Kinasema hivi:

Sifa za
Rais
75. Mtu atakuwa na sifa ya kuchaguliwa kushika nafasi ya

madaraka ya Rais wa Jamhuri ya Muungano ikiwa:
(a) ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa
Katiba hii na sheria za nchi;
(b) ni mwenye akili timamu;
(c) angalau mmoja kati ya wazazi wake ni raia wa kuzaliwa wa
Jamhuri ya Muungano;
(d) wakati wa kugombea, ana umri usiopungua miaka arobaini;
(e) anazo sifa za kumwezesha kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri
ya Muungano kwa mujibu wa Katiba hii;

(f) anayo angalau shahada ya kwanza ya chuo kikuu
kinachotambuliwa kwa mujibu wa sheria za nchi;
(g) ni mwanachama na mgombea aliyependekezwa na chama cha
siasa au mgombea huru;
(h) sera zake au sera za chama chake si za mrengo wa kuligawa
Taifa kwa misingi ya ukabila, udini, rangi au jinsia;
(i) ni mwadilifu na anafuata maadili ya Taifa;
(j) mwenendo wake binafsi hautiliwi shaka na jamii;
(k) hajatiwa hatiani kwa kosa lolote la jinailinalohusu kukosa
uaminifu; na
(l) katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya Uchaguzi
Mkuu hajawahi kutiwa hatiani katika Mahakama yoyote kwa
kosa lolote la kukwepa kulipa kodi yoyote ya Serikali.


Naomba mnisaidie hicho kipengele anachokisema Malemo kwa mujbu wa Gazeti la Mtz ni kipi? au ni katika Rasimu ya Pili?

Kipengele hii ifanyiwe nyongeza ya maneno ilikuondoa Ubaguzi huu (e) anazo sifa za kumwezesha kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa Katiba hii bila kuzingatia/kujali pingamizi dhidi ya sifa ya kuwa Mbunge kwa mujibu wa ibara ya 117;2a ya Katiba hii.

Lakini pia Ibara hii ya 117;2a nayo iko kimya kuhusu lini vipindi hivi vitaanza kuhesabiwa ?
1.Toka Tanganyika iko huru
2.Toka mapinduzi Matukufu za Zanzibar
3. Toka Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
4. Mara baada ya kuanza kwa Katiba hii
 
Back
Top Bottom