Mipango ya Mungu (Yanayomsibu Celine Dion)

Jibu langu la msingi nilikuuliza, huyo Mungu hana huruma ya kumpa mwezi kati ya misiba miwili asipate misiba inayofuatana mmoja baada ya mwingine?
Ni hivi; huo mwezi unaosema wewe ni mawazo yako. Hata ukimwuliza Celine Dion kuwa kungekuwa na interval ya mda gani kati ya msiba mmoja na mwingine, huenda angesema mda tofauti na huo mwezi mmoja.

Sasa kama kila mwanadamu ana mawazo yake kuhusu interval ya msiba na msiba, Je Mungu?

Halafu, nani alikwambia kuwa kila mtu anapokufa basi ni mapenzi ya Mungu? Kama hujui shetani naye anaua na Mungu anamwacha afanye hivyo; hasa kwa wale ambao sio wana wa Mungu, kama wewe.
 
Hujajibu swali la msingi.

Kwa nini Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kaumba ulimwengu ambao watu wanaopendana wanaweza kutenganishwa na kifo?

Hujajibu swali.
 
Kwa nini Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kaumba ulimwengu ambao watu wanaopendana wanaweza kutenganishwa na kifo?

Usimsingizie shetani, kwani unataka kusema Mungu wako angetaka kuumba ulimwengu ambao kifo hakipo na hakijulikani angeshindwa?
 
Hujajibu swali la msingi.

Kwa nini Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kaumba ulimwengu ambao watu wanaopendana wanaweza kutenganishwa na kifo?

Hujajibu swali.
Nimekujibu freshi tu, sema wewe hujaona unachotaka kuona.
 
Nimekujibu freshi tu, sema wewe hujaona unachotaka kuona.
Nakuuliza kwa nini Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote karuhusu ulimwengu ambao watu wanaopendana wanatenganishwa na kifo?

Unanijibu kifo ni hatua tu kama hatua nyingine.

Kwani mimi nilikwambia kifo si hatua?

Nakuuliza kwa nini huyu mtu anakwenda kaskazini na si kwingine?

Unanijibu kwenda kaskazini ni safari tu kama safari nyingine.

Hujajibu swali hapo.

Umedhihirisha huna jibu la swali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…