Mwaka 2026 umeendelea kuonyesha namna mitandao ya kijamii ilivyo na nguvu katika kuunda mijadala ya kisheria na kijamii barani Afrika. Kisa cha TikToker mmoja kutoka Nigeria kwa jina la
Mirabel aliyedai kuwa mwanaume mmoja alimvamia na kisha kumbaka, huku akionesha kuwa amedharirishwa kama binadamu.
Baada ya muda ushahidi ukaanza kutoka kuwa mbona hajabakwa wala kuvamia, ngoma ilivyokuwa ngumu,
Mirabel akakiri kuwa alitoa tuhuma za uongo za kubakwa kwake. Kisa hiki kimeibua mjadala mpana sana kuhusu uwajibikaji kwa pande zote mbili—wanaotenda uhalifu na wanaoutumia vibaya mfumo wa sheria.
Katika mjadala huo, msanii wa Nigeria
Simi akawasha data na kuingia Twitter na kwenda kuandika huku akisisitiza kuwa
wanaume wanaopatikana na hatia ya ubakaji wanapaswa kuadhibiwa vikali sana. Kauli yake ilizua mjadala mkubwa zaidi pale alipodokeza wazo la
“kuhasiwa” ama kitaalamu kama (castration) kwa wahalifu wa ubakaji. Kwa wema watu wakamuuliza, he wale wanawake wanaotoa ushahidi wa uongo wapewe adhabu gani?
DADA AKAJAA MOTO NA KUANZA KUTUMIA MIHEMKO KUJIBU WAJUBA.
Mashirika ya wanawake kutoka Nigeria yakaanza kufuatilia kwa karibu na kuonesha kuwa Mirabel ameathiriwa sana,
INGAWA HAWAKUWEPO WAKATI MIRABEL AKIBAKWA kama ambavyo amedanganya. Mashirika kama
the International Federation of Women Lawyers (FIDA) Nigeria, the African Women Lawyers Association (AWLA), pamoja na
the Nigerian Bar Association Women Forum (NBAWF) walishupalia hii kesi kama vile mwenyekiti wao ndio
AMEBAKWA NA WAO WALIKUWEPO WAKISHUHUDIA.
Mjadala haukuishia hapo, kwani baada ya shinikizo kubwa mitandaoni na ukosoaji mkali kutoka kwa watumiaji mbalimbali, ilidaiwa kuwa hata mume wake,
Adekunle Gold, hakuridhishwa na msimamo huo. Muda mfupi baadaye,
Simi aliibuka kupitia mtandao wa Snapchat akiomba radhi kwa lugha iliyoonekana yenye ukali wa kauli yake ya awali. Aliweka wazi kuwa hakumaanisha kuhamasisha ukatili, bali alichochewa na hasira dhidi ya vitendo vya ubakaji. Hatua hiyo ya kuomba radhi ilitafsiriwa na baadhi ya wachambuzi kama jaribio la kurekebisha taswira yake na kutuliza mvutano wa kifamilia na kijamii.
Hata hivyo, kiini cha mjadala kinabaki kwenye mfumo wa sheria. Nchi nyingi za Afrika zina sheria kali dhidi ya ubakaji ambao mara kadhaa ni wanaume. Ndani ya jamii zetu ni nadra kusikia mtoto wa kiume kabakwa na mwanamke, sio kwamba haiwezekani ila ni NADRA SANA.
Tumekuwa na sheria zilizoweka vifungo virefu kwa wanaume wanaopatikana na hatia. Lakini pia, makosa ya kutoa taarifa za uongo au kuapa kwa uongo yapo kisheria—ingawa utekelezaji wake mara nyingi huwa dhaifu.
Haswa kama anayetoa ushahidi ni mwanamke halafu Hakimu ni mwanamke pia,
AISEE HAPO UTAKUWA KAMA KITIMOTO UNAJIKAANGA NA MAFUTA YAKO. Na ni hapa ndipo hoja ya usawa inapojitokeza: Je, mfumo unapaswa kuwa mkali kwa wanaume pekee?
Kwenye jamii ni kawaida sana kuwa na msingi huu, sheria na miongozo haiwezi kutungwa kwa Mihemko ama hasira. Sheria inapaswa kusimama juu ya ushahidi, uchunguzi wa kitaalamu na kanuni za haki za binadamu. Vinginevyo, jamii inaweza kujikuta ikihama kutoka kutafuta haki kwenda kulipiza visasi.
Tusaidieni wataalamu wa Sheria pamoja na wadau,
je kama kijana akipigwa mvua ya miaka 30 jela kwa kosa la Ubakaji na akatumikia kifungo cha miaka 20 na baadaye binti ambaye ndio alifungua kesi ya ubakaji akajitokeza hadharani na kuomba msamaha, KIPI KIFANYIKE? Je Jamaa asamehe tu na maisha yaendelee? Ama Binti na yeye aende jela miaka 30?
Kama umewahi kutazama filamu ya
Section 375 utaelewa mapengo ya sheria hizi ambazo Muingereza alituachia baada ya uhuru. Ila pia kama umefuatilia kesi ya
John C. Depp, II dhidi ya
Amber Laura Heard, utaelewa kwanini kuna wakati wanawake hutumia sheria vibaya kuwaumiza wanaume kwa kile kinachoitwa
HAKI.
KUNA WAKATI MAHAKIMU WA KIKE PAMOJA WANASHERIA WA KIKE WAKIFANIKIWA KUMTUPA MWANAUME JELA WANAJISIKIA VIZURI SANA HATA KAMA KESI NI YA UONGO AU USHAHIDI WA UONGO.