Mwenge wa Uhuru unatarajia kuanza mbio zake mkoani Mara Agosti 15, 2025, ukitokea mkoani Simiyu, ambapo utazunguka katika halmashauri zote tisa za mkoa huo na kukagua, kuweka mawe ya msingi, kufungua na kuzindua miradi 68 ya maendeleo yenye thamani ya shilingi bilioni 26.54
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi, amesema mbio hizo zitapita umbali wa takribani kilomita 1,123 ndani ya mkoa huo. Amefafanua kuwa Mwenge wa Uhuru utakapokuwa Mara, utapita nyumbani kwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na kuwashwa Mwenge wa Mwitongo, tukio litakalofanyika Agosti 18, 2025
Mbio za Mwenge wa Uhuru mkoani Mara zinatarajiwa kukamilika Agosti 23, 2025, na siku inayofuata, Agosti 24, utakabidhiwa kwa mkoa wa Mwanza