Elius W Ndabila
JF-Expert Member
- Jul 17, 2019
- 324
- 649
LIJUE BOMBA LA MAFUTA LA TANZANIA UGANDA.
NA ELIUS NDABILA
0768239284
Hivi karibuni Rais wa Tanzania Mhe Mama Suluhu Hassan na Rais wa Uganda Mhe Yoweri Mseveni waliongoza utiaji wa saini ya kuanza kwa Ujenzi wa bomba la Mafuta la Tanzania mpaka Uganda.
Historia ya Ujenzi huu ni matokeo ya tamko la Pamoja la kukamilika kwa majadiliano ya vipengele vya mkataba kuhusu utekelezaji wa Mradi husika lilisainiwa tarehe 21 Mei,2017 Jijini Dae-es-Salaam na Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Jamhuri wa Uganda Mhe.Yoweri Kaguta Museveni.
Wakati huo Mhe Yoweri Mseveni “Kwa niaba ya wananchi wa Uganda ninawashukuru Rais Magufuli na ndugu zetu wa Tanzania kwa makubaliano mbali mbali yanayohusiana na bomba la mafuta. Hakutakuwa na ushuru wa kupitisha mafuta, hakutakuwa na kodi ya ongezeko la thamani, hakutakuwa na kodi ya mapato ya kampuni, wametupa msamaha wa kodi kwa miaka 20, wametupa eneo la bure ambako bomba la mafuta lipita na kuahidi kununua hisa katika bomba la mafuta” alisema Rais Museveni
Hata hivyo Rais wa awamu ya tano ya Tanzania hayati John Magufuli Rais Magufuli alisema hatua ambayo Tanzania na Uganda zimefikia katika mradi wa bomba la mafuta ni matokeo ya urafiki na udugu wa kihistoria ulioko kati ya nchi hizi mbili.
Rais Magufuli alisema mradi huo utakuwa na manufaa makubwa kwa Uganda, Tanzania, Afrika Mashariki na Afrika nzima, na kwamba pamoja na faida zilizoainishwa kwa bomba hilo kupitia Tanzania ni uwepo wa amani, uzoefu wa Tanzania katika uendeshaji wa miradi ya mabomba ya mafuta na gesi, jiografia nzuri ya usafirishaji mafuta, ardhi na ubora wa bandari ya Tanga, Tanzania inaupokea mradi huo kwa heshima kubwa na ni kumbukumbuku kubwa ya Rais Museveni na Serikali yake.
Mhe Magufuli aliyaomba mataifa yote ya Afrika Mashariki kulichukulia bomba la mafuta la Afrika Mashariki kama mali ya Afrika Mashariki, akibainisha kuwa kwa kugundulika kwa mafuta na gesi katika nchi nyingine katika eneo hilo, bomba litakuwa chombo cha kusafirishia mafuta kuelekea baharini kutoka nchi zote za Afrika Mashariki.
Mradi huu wa Bomba la Kusafirishia Mafuta Ghafi kutoka Hoima Nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga Tanzania Unajulikana kama East African Crude oil Pipeline (EACOP).
Bomba hili litakuwa na urefu wa kilometa 1,445.
Matokeo ya utafiti uliofanywa na kampuni za kimataifa za utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi za TOTAL, TULLOW na CNOOC ulibaini uwepo wa mafuta ghafi takribani mapipa bilioni 6.5. Kutokana na ugunduzi huo imebainika uwezekano wa kuvuna mapipa kati ya bilioni 1.2 hadi 1.7. Kutokana na mahusiano ya ushirikiano ya muda mrefu na faida za kupitisha bomba nchini Tanzania Serikali ya Uganda na wawekezaji wa mkondo wa juu waliamua kujenga mradi huu kupitia Tanzania kutoka Hoima Uganda hadi
Lengo la mradi huu ni kuwezesha mafuta yatakayozalishwa nchini Uganda kusambazwa katika soko la ndani na sehemu inayobaki kuuzwa nje kwenye soko la kimataifa kupitia bomba la mafuta.
Mradi wa Bomba la Kusafirishia Mafuta Ghafi kupitia Tanzania ulitangazwa na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni wakati wa Mkutano wa 13 wa ushoroba wa kaskazini ambapo alieleza kuwa Bomba hilo la Mafuta kutoka Hoima Ziwa Albert nchini Uganda litapita katika ardhi ya Tanzani kwenda bandari ya Tanga.
Zipo sababu nyingi ambazo nchi ya Uganda iliachana na kupitisha bomba hili nchini Kenya na kuleta Tanzania. Baadhi ya sababu zilizochangia bomba hilo kupita nchini Tanzania ni pamoja na:
Kwanza ubora wa bandari ya Tanga ambayo imeonekana kuwa bora zaidi ukilinganisha na bandari nyingine za Afrika Mashariki kwa kuwa ina kingo za asili (naturally sheltered) na kina cha futi 25 kwenda chini hivyo kupunguza muda na gharama za ujenzi kwa kuwa uchimbaji wa kina hauhitajiki ukilinganisha bandari zingine.Pia bandari hiyo ya Tanga itakuwa na uwezo wa kupakia mafuta katika mwaka mzima.
Sababu nyingine ni miunganiko ya njia za reli ya Tanga hadi reli ya kati ambayo kwa sasa imeboreshwa sana na bado kuna Ujenzi wa reli ya SGR inayoendelea ambayo itachangia Kasi kubwa ya usafirishaji.
Tanzania pia inatajwa kuwa na miundombinu ya barabara nyingi ambayo haipo katika njia mbadala za jirani.
Pamoja na hivyo Tanzania suala la usalama na uzoefu wa Tanzania katika ujenzi wa mabomba yakiwemo Bomba la gesi asilia kutoka kisiwa cha Songo Songo mpaka Ubungo-Dar, Bomba la gesi asilia kutoka Madimba Mtwara hadi Kinyerezi Dar-es-salaam na Bomba la kusafirisha mafuta kutoka Tanzania hadi Zambia (TAZAMA).
Jambo lingine inatajwa hali ya tambarare katika ardhi ya Tanzania hivyo gharama za utekelezaji kuwa rahisi kuliko ingepelekwa Uganda.
Njia iliyochaguliwa kujenga bomba hili inaanzia Kabaale – Hoima, Uganda na inaeelekea kusini hadi Peninsula ya Chongoleani karibu na bandari yaTanga Tanzania. Njia ya bomba ilichaguliwa na Serikali ya Uganda kwa kuwa ina gharama nafuu zaidi. Bomba hilo litaanzia Hoima, karibu na Ziwa Albert, na kuvuka mpaka wa Uganda na Tanzania kati ya Masaka na Bukoba, karibu na Ziwa Victoria, katika mpaka wake wa magharibi, nchini Tanzania, bomba litapita karibu na Kahama, Singida, Kondoa hadi Tanga. Nchini Uganda, bomba litakuwa na urefu wa kilomita 296.
Gharama za kukamilisha ujenzi wa mradi wa bomba zinatarajia kufikia takribani Shilingi Trilioni 8 za Kitanzania. Bomba hili litajengwa na kuendeshwa na kampuni za TOTAL ya Ufaransa, CNOOC ya China na TULLOW ya Uingereza, kwa ubia na Kampuni ya Taifa ya Mafuta ya Uganda (UNOC) na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).
Wachunguzi wa mambo wanasema huu ni mradi mkubwa ambao Tanzania itapata fedha nyingi. Bomba hili la mafuta likikamiliki Tanzania litakuwa sehemu ya miradi mikubwa ambayo Tanzania itakuwa imejiwekea heshima ikiwepo SGR na Mradi wa kuzalisha Umeme wa Nyerere.
Ardhi ya mradi imetengwa katika maeneo makuu matatu ambayo ni maeneo ya kipaumbele, eneo la bomba (mkuza) na sehemu ya matenki ya kuhifadhi na kusafirisha mafuta. Mradi una fursa nyingi za kiuchumi na kijamii na unatarajia kuleta mabadiliko makubwa na manufaa kwa nchi zote mbili pamoja na wawekezaji. Mradi unatarajia kuzalisha ajira na kuwezesha jumla ya wananchi watakaonufaika na fursa zaidi ya 10,000 wakati wa ujenzi ukilinganisha na wakati wa shughuli za awali kabla ya ujenzi na wakati wa uendeshaji. Mradi wa Bomba utawezesha pia kutoa fursa mbalimbali za biashara zitakazotokana na mradi huu.
Maeneo ya kipaumbele yatazingatia kambi za wafanyakazi (12), hifadhi za mabomba na kiwanda cha kuweka plastiki (1); eneo la mkuza litakuwa ni eneo litakapolazwa bomba pamoja na miundombinu mingine kama vituo vya kuongeza msukumo (4), kupunguza msukumo (2), vituo vya umeme n.k; sehemu ya kuhifadhi na kusafirisha mafuta – patakapojengwa matenki na jeti ya kupakia mafuta kwenye meli.
Inawezekana mradi huu hauzungumzwi sana na Wachambuzi wa mambo ya kiuchumi, lakini ni mradi ambao utaenda kutengeneza Uchumi mkubwa kwa nchi yetu kwani utatengenezeza ajira nyingi kwa Wananchi.
Moja ya kazi kubwa na legacy ambayo Hayati Magufuli ameacha ni kubuni miradi mikubwa na ya kimkakati kwa ajili ya Maendeleo makubwa ya Taifa. Aliweza kuibua miradi ambayo ilitazamwa katika ugumu wa kuitekeleza, lakini yeye alisema atafanya.
Hivi karibuni Rais Samia amenukuliwa kuwa miradi yote iliyoasisiwa na mtangulizi wake Hayati Dkt Magufuli ataitekeleza na kuisimamia mpaka ikamilike. Watanzania wengi wamefarajika na kauli hii ya Mhe Rais kwa kuwa walikuwa hawajui hatima ya miradi hii mikubwa.