Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
SERIKALI imeweka wazi miradi ya umeme ya kipaumbele, itakayotoa matokeo ya haraka ifikapo 2015/2016, na kunufaisha wananchi katika mikoa 13 nchini.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, alisema hayo jana mbele ya wadau waliokusanyika
katika mkutano wa siku moja wa kukusanya maoni kuhusu utekelezaji wa miradi hiyo.
Alisema wizara hiyo imedhamiria kuhakikisha miradi hiyo kwa kipindi hicho, inaleta matokeo muafaka
yatakayoonekana wazi kwa Watanzania wote.
Miradi Aliitaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na bomba la gesi kutoka Mnazibay hadi Dar es Salaam, lenye
urefu wa Kilometa 534, ambalo litagharimu dola za Marekani bilioni 1.2.
Nasisitiza acheni malumbano ya kipuuzi na malalamiko yasiyo na tiba, bomba hili lazima likamilike ndani ya miezi 18, alisema Muhongo.
Alisema wote wanaopinga kutandikwa kwa bomba hilo, hawaitakii mema Tanzania na wananchi wake na kwamba hoja zao zimejaa ubaguzi.
Naomba tusipoteze muda kujadili bomba hili, wapo watu wana sababu zao, hii gesi itanufaisha Watanzania
wote wakiwemo wa Mtwara, tusikubali ujinga wa mtu mmoja uwe wa taifa zima, alisisitiza.
Alitaja miradi mingine kuwa ni mitambo saba mipya ya Kinyerezi, itakayozalisha megawati za umeme 1,310,
itakayozalisha megawati 990, na mradi wa upepo wa Singida wa megawati 50 na Kiwira wa megawati 200.
Miradi mingine ni ya ujenzi wa njia za usambazaji umeme, ambazo ni Iringa-Shinyanga yenye kilometa 657
utakaosambaza umeme wa KV 400 na Dar es Salaam-Chalinze-Tanga- Same-Arusha, wenye kilometa 682
utakaosambaza umeme wa KV 400.
Pia upo mradi wa Singida-Arusha wa kilometa 414 utakaosambaza umeme wa KV 400, Somanga-Fungu-
Somanga-Kinyerezi wa kilometa 300, utakaosambaza umeme wa KV 220.
Mradi mwingine ni wa Nyakanazi-Kigoma-Mpanda-Sumbawanga- Mbeya, wenye kilometa 340
utakaosambaza umeme wa KV 400 na Dar es Salaam-Morogoro-Dodoma wenye urefu wa kilometa 530,
utakaosambaza umeme wa KV 400.
Viapo
Ili kuhakikisha kila mradi, utekelezaji unasimamiwa vilivyo, wakurugenzi wanne walioko chini ya Wizara ya
Nishati na Madini, watakaowajibika kutekeleza miradi hiyo, wameapa mbele ya wananchi kuwa
watafanikisha matokeo ya miradi hiyo, vinginevyo wako tayari kutimuliwa kazi.
Wakurugenzi hao ni pamoja na Mkurugenzi wa Shirika la Umeme (Tanesco), Felchesmi Mramba na
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC), Yona Killagane.
Wengine ni Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Usambazaji Umeme Vijijini (REA), Lutengano Mwakahesya
pamoja na Kamishna wa Nishati na Petroli, Hosea Mbise ambaye ndiye msimamizi mkuu wa miradi hiyo.
Wakurugenzi hao walitoa kiapo hicho mbele ya wadau waliokusanyika katika mkutano wa siku moja
ulioandaliwa na wizara hiyo, kwa ajili ya kukusanya maoni juu ya utekelezaji wa miradi hiyo yenye matokeo
makubwa nchini ifikapo mwaka 2015/2016.
Akizungumza mara baada ya kuapa mbele ya wadau hao, Mbise, alisema wizara hiyo imedhamiria
kuhakikisha kuwa miradi hiyo kwa muda huo, inaleta matokeo muafaka yatakayoonekana wazi kwa
Watanzania wote.
Ni kweli kumekuwepo na miradi mingi ya wizara hii kwa muda mrefu, lakini sasa nawaahidi kuwa tunakuja
na njia mpya ya kuzingatia miradi michache, lakini matokeo yake pamoja na kuonekana haraka, yatanufaisha
Watanzania wengi. Ninawaahidi katika utekelezaji wa miradi hii, tutaachana kabisa na tabia ya kufanya kazi
kwa mazoea, alisisitiza.
Kwa upande wake Mramba, alisema miradi hiyo, sehemu kubwa itatekelezwa na shirika lake. Nawaahidi
Tanesco haitowaangusha, ninaamini uwezo wa kuleta matokeo haya makubwa ninao, nikishindwa niko radhi
mnichukulie hatua.
Killagane naye alisema ili kufanikisha miradi yote hiyo, jambo la msingi ni kuhakikisha gesi inapatikana kwa
haraka, ambapo kwa mujibu wa maelekezo ya TPDC, ni lazima bomba la gesi kutoka Mnazibay mkoani
Mtwara hadi Dar es Salaam, liwe limetandikwa na kukamilika ifikapo Juni mwakani.
Hili nitasimamia kwa dhati kuhakikisha gesi hii inafika jijini hapa mwakani kama ilivyopangwa, TPDC
tumejipanga ili kuhakikisha hii kazi haikwami, alisisitiza.
Mwakahesya ambaye ni Mkurugenzi wa REA, alisUema jukumu lake katika utekelezaji wa miradi hiyo, ni
kushirikiana na sekta binafsi na ya umma, ili umeme ufike vijijini. Si maneno bali ni vitendo, niwajibisheni
kama sitafanikisha haya.
Muhongo alisema anaamini watendaji hao hawawezi kumdanganya yeye wala Watanzania, kwa kuwa anao
uzoefu wa kutosha kubaini iwapo anadanganywa.
Naomba mkiona mtu anafanya kazi chini ya wizara yangu hii kinyume na taratibu, mleteni kwangu na nina
ahidi mbele ya wananchi hawa kuwa sababu zitakazomuondoa mtumishi wa wizara hii kazini, ni pamoja na
rushwa, wizi, utendaji mbovu na ubababishaji, hapa hakutakuwa na mjadala, nyie mtaona tu watu
wakipukutika, alisisitiza.
Kuhusu umeme vijijini, Muhongo alisema kupitia mpango wao walioainisha wa umeme vijijini, watahakikisha
kila mwaka kwenye kila mkoa, vijiji kadhaa vitakavyobainishwa kulingana na idadi ya watu wake, vitapatiwa
umeme na tayari Sh bilioni 330 zimetengwa kwa ajili ya kazi hiyo.
Alisema miradi hiyo ikikamilika, Tanzania itakuwa inazalisha megawati za umeme 2,780 na lengo ni
kuhakikisha ifikapo mwaka 2025, megawati za umeme 3,000 zinazalishwa na asilimia 56 ya Watanzania
wana umeme. Kwa sasa megawati za umeme zinazozalishwa ni 1,430.24 wakati mahitaji ni megawati 850.
Tanesco kubomolewa
Ili kufanikisha malengo hayo, Muhongo alisema tayari hatua za kubomoa Tanesco zimeshaanza kuchukuliwa,
kwa sasa mchakato wa kumtafuta mshauri kwa ajili ya kufanyia kazi ripoti ya menejimenti ya shirika hilo,
juu ya namna liwe, umeanza kwa ufadhili wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB).
Mapendekezo ya awali yanaonesha shirika hilo litabomolewa na kugawanywa, ambapo sehemu za uzalishaji,
usambazaji na usafirishaji umeme zitajitegemea, kwa kuwa na kampuni zaidi ya tatu, ambazo hazitotegemea
ruzuku ya Serikali.
Kwa upande wa TPDC, Muhongo alisema Serikali pia italifumua shirika hilo kutoka kwenye muundo wake
wa sasa, na kuwa shirika kubwa litakalofanya utafiti na uvunaji wa gesi na mafuta, kama kampuni kubwa za
kigeni zinavyofanya ili kuondoa malalamiko ya nishati hiyo kuibiwa na wageni.
Katibu ahongwa
Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi, alisema tayari
alishafuatwa na watu kadhaa ambao walitaka kumpa rushwa, ili miradi yao mibovu itekelezwe na Serikali.
Kuna mtu alikuja akaniambia nikiweka saini kwenye mradi wake, atanipa dola za Marekani 200,000
ambazo ni sawa na Sh milioni 350, nikamkatalia na kumtaka aondoke haraka na mradi wake uchwara,
alisema.
Kuhusu kusafisha Tanesco, alisema hadi kufikia Desemba mwaka
jana na Juni mwaka huu, Shirika la Umeme (Tanesco), tayari limefukuza kazi watumishi 49 wanaotuhumiwa
kuhusika na rushwa na kulihujumu shirika hilo.
SOURCE: HABARI LEO