Miradi mikubwa ya umeme kuinufaisha mikoa ya Tanzania...!

Miradi mikubwa ya umeme kuinufaisha mikoa ya Tanzania...!

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
SERIKALI imeweka wazi miradi ya umeme ya kipaumbele, itakayotoa matokeo ya haraka ifikapo 2015/2016, na kunufaisha wananchi katika mikoa 13 nchini.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, alisema hayo jana mbele ya wadau waliokusanyika

katika mkutano wa siku moja wa kukusanya maoni kuhusu utekelezaji wa miradi hiyo.


Alisema wizara hiyo imedhamiria kuhakikisha miradi hiyo kwa kipindi hicho, inaleta matokeo muafaka

yatakayoonekana wazi kwa Watanzania wote.


Miradi Aliitaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na bomba la gesi kutoka Mnazibay hadi Dar es Salaam, lenye

urefu wa Kilometa 534, ambalo litagharimu dola za Marekani bilioni 1.2.


“Nasisitiza acheni malumbano ya kipuuzi na malalamiko yasiyo na tiba, bomba hili lazima likamilike ndani ya miezi 18,” alisema Muhongo.

muhongo4_300_172.jpg


Alisema wote wanaopinga kutandikwa kwa bomba hilo, hawaitakii mema Tanzania na wananchi wake na kwamba hoja zao zimejaa ubaguzi.


“Naomba tusipoteze muda kujadili bomba hili, wapo watu wana sababu zao, hii gesi itanufaisha Watanzania

wote wakiwemo wa Mtwara, tusikubali ujinga wa mtu mmoja uwe wa taifa zima,” alisisitiza.


Alitaja miradi mingine kuwa ni mitambo saba mipya ya Kinyerezi, itakayozalisha megawati za umeme 1,310,

itakayozalisha megawati 990, na mradi wa upepo wa Singida wa megawati 50 na Kiwira wa megawati 200.


Miradi mingine ni ya ujenzi wa njia za usambazaji umeme, ambazo ni Iringa-Shinyanga yenye kilometa 657

utakaosambaza umeme wa KV 400 na Dar es Salaam-Chalinze-Tanga- Same-Arusha, wenye kilometa 682

utakaosambaza umeme wa KV 400.


Pia upo mradi wa Singida-Arusha wa kilometa 414 utakaosambaza umeme wa KV 400, Somanga-Fungu-

Somanga-Kinyerezi wa kilometa 300, utakaosambaza umeme wa KV 220.


Mradi mwingine ni wa Nyakanazi-Kigoma-Mpanda-Sumbawanga- Mbeya, wenye kilometa 340

utakaosambaza umeme wa KV 400 na Dar es Salaam-Morogoro-Dodoma wenye urefu wa kilometa 530,

utakaosambaza umeme wa KV 400.


Viapo

Ili kuhakikisha kila mradi, utekelezaji unasimamiwa vilivyo, wakurugenzi wanne walioko chini ya Wizara ya

Nishati na Madini, watakaowajibika kutekeleza miradi hiyo, wameapa mbele ya wananchi kuwa

watafanikisha matokeo ya miradi hiyo, vinginevyo wako tayari kutimuliwa kazi.


Wakurugenzi hao ni pamoja na Mkurugenzi wa Shirika la Umeme (Tanesco), Felchesmi Mramba na

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC), Yona Killagane.


Wengine ni Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Usambazaji Umeme Vijijini (REA), Lutengano Mwakahesya

pamoja na Kamishna wa Nishati na Petroli, Hosea Mbise ambaye ndiye msimamizi mkuu wa miradi hiyo.


Wakurugenzi hao walitoa kiapo hicho mbele ya wadau waliokusanyika katika mkutano wa siku moja

ulioandaliwa na wizara hiyo, kwa ajili ya kukusanya maoni juu ya utekelezaji wa miradi hiyo yenye matokeo

makubwa nchini ifikapo mwaka 2015/2016.


Akizungumza mara baada ya kuapa mbele ya wadau hao, Mbise, alisema wizara hiyo imedhamiria

kuhakikisha kuwa miradi hiyo kwa muda huo, inaleta matokeo muafaka yatakayoonekana wazi kwa

Watanzania wote.


“Ni kweli kumekuwepo na miradi mingi ya wizara hii kwa muda mrefu, lakini sasa nawaahidi kuwa tunakuja

na njia mpya ya kuzingatia miradi michache, lakini matokeo yake pamoja na kuonekana haraka, yatanufaisha

Watanzania wengi. “Ninawaahidi katika utekelezaji wa miradi hii, tutaachana kabisa na tabia ya kufanya kazi

kwa mazoea,” alisisitiza.


Kwa upande wake Mramba, alisema miradi hiyo, sehemu kubwa itatekelezwa na shirika lake. “Nawaahidi

Tanesco haitowaangusha, ninaamini uwezo wa kuleta matokeo haya makubwa ninao, nikishindwa niko radhi

mnichukulie hatua.”


Killagane naye alisema ili kufanikisha miradi yote hiyo, jambo la msingi ni kuhakikisha gesi inapatikana kwa

haraka, ambapo kwa mujibu wa maelekezo ya TPDC, ni lazima bomba la gesi kutoka Mnazibay mkoani

Mtwara hadi Dar es Salaam, liwe limetandikwa na kukamilika ifikapo Juni mwakani.


“Hili nitasimamia kwa dhati kuhakikisha gesi hii inafika jijini hapa mwakani kama ilivyopangwa, TPDC

tumejipanga ili kuhakikisha hii kazi haikwami,” alisisitiza.


Mwakahesya ambaye ni Mkurugenzi wa REA, alisUema jukumu lake katika utekelezaji wa miradi hiyo, ni

kushirikiana na sekta binafsi na ya umma, ili umeme ufike vijijini. “Si maneno bali ni vitendo, niwajibisheni

kama sitafanikisha haya.”


Muhongo alisema anaamini watendaji hao hawawezi kumdanganya yeye wala Watanzania, kwa kuwa anao

uzoefu wa kutosha kubaini iwapo anadanganywa.


“Naomba mkiona mtu anafanya kazi chini ya wizara yangu hii kinyume na taratibu, mleteni kwangu na nina

ahidi mbele ya wananchi hawa kuwa sababu zitakazomuondoa mtumishi wa wizara hii kazini, ni pamoja na

rushwa, wizi, utendaji mbovu na ubababishaji, hapa hakutakuwa na mjadala, nyie mtaona tu watu

wakipukutika,” alisisitiza.


Kuhusu umeme vijijini, Muhongo alisema kupitia mpango wao walioainisha wa umeme vijijini, watahakikisha

kila mwaka kwenye kila mkoa, vijiji kadhaa vitakavyobainishwa kulingana na idadi ya watu wake, vitapatiwa

umeme na tayari Sh bilioni 330 zimetengwa kwa ajili ya kazi hiyo.


Alisema miradi hiyo ikikamilika, Tanzania itakuwa inazalisha megawati za umeme 2,780 na lengo ni

kuhakikisha ifikapo mwaka 2025, megawati za umeme 3,000 zinazalishwa na asilimia 56 ya Watanzania

wana umeme. Kwa sasa megawati za umeme zinazozalishwa ni 1,430.24 wakati mahitaji ni megawati 850.


Tanesco kubomolewa


Ili kufanikisha malengo hayo, Muhongo alisema tayari hatua za kubomoa Tanesco zimeshaanza kuchukuliwa,

kwa sasa mchakato wa kumtafuta mshauri kwa ajili ya kufanyia kazi ripoti ya menejimenti ya shirika hilo,

juu ya namna liwe, umeanza kwa ufadhili wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB).


Mapendekezo ya awali yanaonesha shirika hilo litabomolewa na kugawanywa, ambapo sehemu za uzalishaji,

usambazaji na usafirishaji umeme zitajitegemea, kwa kuwa na kampuni zaidi ya tatu, ambazo hazitotegemea

ruzuku ya Serikali.


Kwa upande wa TPDC, Muhongo alisema Serikali pia italifumua shirika hilo kutoka kwenye muundo wake

wa sasa, na kuwa shirika kubwa litakalofanya utafiti na uvunaji wa gesi na mafuta, kama kampuni kubwa za

kigeni zinavyofanya ili kuondoa malalamiko ya nishati hiyo kuibiwa na wageni.



Katibu ahongwa



Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi, alisema tayari

alishafuatwa na watu kadhaa ambao walitaka kumpa rushwa, ili miradi yao mibovu itekelezwe na Serikali.


“Kuna mtu alikuja akaniambia nikiweka saini kwenye mradi wake, atanipa dola za Marekani 200,000

ambazo ni sawa na Sh milioni 350, nikamkatalia na kumtaka aondoke haraka na mradi wake uchwara,”

alisema.


Kuhusu kusafisha Tanesco, alisema hadi kufikia Desemba mwaka



jana na Juni mwaka huu, Shirika la Umeme (Tanesco), tayari limefukuza kazi watumishi 49 wanaotuhumiwa


kuhusika na rushwa na kulihujumu shirika hilo.


SOURCE: HABARI LEO



 
2015/16 si mbali tusubiri mazingaombwe ya CCM kama itawezekana, maana hawa jamaa kwa ahadi utafikiri wanajali kweli. Utaona watu wanafanya vitu visivyojulikana then baada ya muda kila kitu kinakufa ghafla na visingizio kibaooooooooo.
 


Katibu ahongwa


Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi, alisema tayari

alishafuatwa na watu kadhaa ambao walitaka kumpa rushwa, ili miradi yao mibovu itekelezwe na Serikali.


“Kuna mtu alikuja akaniambia nikiweka saini kwenye mradi wake, atanipa dola za Marekani 200,000

ambazo ni sawa na Sh milioni 350, nikamkatalia na kumtaka aondoke haraka na mradi wake uchwara,”

SOURCE: HABARI LEO




kweli bongo tambarare, Sasa hiyo inayoitwa vita ya rushwa itashinda vp kama wakuu hawa badala ya kuwapeleka mahakamani watoa rushwa eti " nikamkatalia na kumwambia aondoke zake" hahahahaha!!! na vp zile alizochukua? halafu toka lini wizara ikatoa viapo?
 
Back
Top Bottom