UTPC
Journalists' Union
- Apr 17, 2026
- 51
- 38
Kwa zaidi ya miaka miwili, wananchi wa Jiji la Mbeya wanaoishi na kufanya shughuli zao kando kando ya barabara ya njia nne kutoka Nsalaga hadi Ifisi, wameendelea kusubiri kukamilika kwa mradi huo waliyotarajia ungekuwa suluhisho la msongamano wa magari na kurahisisha usafiri, lakini badala yake wamejikuta wakikabiliwa na foleni, mashimo, vumbi na ajali.
Uchunguzi wa Bomba FM uliofanywa kwa zaidi ya miezi mitatu umebaini kuwa kuchelewa kwa mradi huo kumeongeza adha kwa wananchi, wafanyabiashara na watumiaji wa barabara, huku baadhi ya maeneo ya mradi huo yakiwa katika hali inayohatarisha usalama na kuathiri shughuli za kila siku.
Mradi huo wenye urefu wa kilomita 29 ulianza kutekelezwa Machi mwaka 2023 kwa gharama ya shilingi bilioni 184 na ulipangwa kukamilika ndani ya miezi 24. Hata hivyo, muda huo umepita huku ujenzi ukiwa bado unaendelea.
Barabara hiyo ni muhimu kwa Jiji la Mbeya kutokana na nafasi yake katika kurahisisha usafiri wa watu na mizigo, lakini kuchelewa kwake kumewaweka wananchi katika mazingira ambayo hawakutarajia baada ya kuanza kwa mradi.
Katika eneo la Mama John baadhi ya wananchi wanasema sehemu za barabara hiyo zimeachwa na mashimo makubwa yanayofanya usafiri kuwa mgumu na kuongeza hatari kwa watumiaji.
Katika maeneo yanayopitiwa na mradi huo, foleni imekuwa sehemu ya maisha ya kila siku ya wananchi. Mkaazi mmoja wa Mbeya anasema msongamano wa magari umeambatana pia na ajali za pikipiki na bajaji.
Meneja wa Wakala wa Barabara Mkoa wa Mbeya, Mhandisi Suleiman Bishanga, anabainisha kuwa mkandarasi ameanza kazi mara baada ya kulipwa stahiki zake.
Sehemu ya pili ~ Nini kinachokamisha Mradi wa Njia 4 Mbeya kukamilika? Sababu zimekuwa nyingi na zinazokinzana
Sehemu ya tatu ~ Wachimbaji madini wadogo wa Saza - Songwe hawatendewi haki, leseni imetolewa mara 2 ili mkubwa awaondoe
ANDIKO LA: Heneliko Malo
Makala imeandaliwa na Mwandishi anayeshiriki katika programu maalum ya kukuza uandishi wa maslahi kwa umma (Public Interest Journalism Fellowship) inayoratibiwa na UTPC kwa kushirikiana na IMS
Uchunguzi wa Bomba FM uliofanywa kwa zaidi ya miezi mitatu umebaini kuwa kuchelewa kwa mradi huo kumeongeza adha kwa wananchi, wafanyabiashara na watumiaji wa barabara, huku baadhi ya maeneo ya mradi huo yakiwa katika hali inayohatarisha usalama na kuathiri shughuli za kila siku.
Barabara hiyo ni muhimu kwa Jiji la Mbeya kutokana na nafasi yake katika kurahisisha usafiri wa watu na mizigo, lakini kuchelewa kwake kumewaweka wananchi katika mazingira ambayo hawakutarajia baada ya kuanza kwa mradi.
Katika eneo la Mama John baadhi ya wananchi wanasema sehemu za barabara hiyo zimeachwa na mashimo makubwa yanayofanya usafiri kuwa mgumu na kuongeza hatari kwa watumiaji.
Mkaazi mwingine anasema hali hiyo imekuwa ikiathiri pia wafanyabiashara wanaofanya shughuli zao kando kando ya barabara.“Hapa walikuja walitoa nondo, tukajua labda wanatoa nondo hizi ndiyo mpango umeanza, kumbe wametoa na nondo wameenda nazo basi ndiyo wametuachia shimo kama hivi. Ni bora wangeacha hii lami ili usafiri uwe unapitika tu. Yaani mambo mengine haya wanaenda wakikaa fresh wamalizie.”
Mbali na hali ya barabara, wananchi wanaendelea kuhusisha mazingira ya usafiri katika maeneo hayo na ongezeko la hatari za ajali. Katika uchunguzi wake, Bomba FM ilibaini matukio ya ajali yaliyoongeza hofu miongoni mwa wananchi kuhusu usalama wa barabara katika Jiji la Mbeya. Juni 8 mwaka 2025 watu 28 walifariki dunia na wengine 12 kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari manne kwenye mteremko wa Mlima Iwambi jijini Mbeya, na hii ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya.“Huu mtaa ni wa kibyabiashara, kwa hiyo wafanyabiashara wako wengi sana. Kwa hiyo watu wanauza chakula, mama ntilie wako hapa wanauza chakula, kwa hiyo unakuta mavumbi hayo, magari asubuhi foleni inakuwa kubwa, watu wanahama barabara kuu wanakuja mpaka huku, wanatibua vumbi, ndiyo hivyo tena yaani adha ipo nyingi sana.”
Madereva wa daladala nao wanasema foleni zimekuwa zikiongeza muda wa safari na kuathiri ratiba zao za kila siku.“Vile vile hapa ndiyo kuna foleni kubwa sana. Na hata ukiangalia pale barabarani utaona kwamba kuna barabara imetengamaa kidogo. Bajaji zinaanguka sana hapa, watu wanaumia sana. Juzi juzi mama mmoja kaumia, mara nyingi bajaji zinaanguka kwa sababu ya barabara. Tunaomba tusaidiwe.”
Mhandisi Rajabu Ngulikwa, Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Mbeya, anasema utaratibu wa kuyapitisha magari kwa zamu umewekwa ili kupunguza uwezekano wa kutokea kwa ajali zaidi.“Foleni hii inasubiriwa kwa muda mrefu sana hapa. Unafika hapa saa 12:00 jioni jam imeanza. Nyumbani umetoka saa 11:00, hapa unakuta wanamaliza saa nzima jam. Tusaidie tu.”
Kwa upande wa uchumi, mtaalamu wa uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe kampasi ya Mbeya, Dkt. Stewart Mbegu, anasema foleni zinaongeza gharama kwa wananchi, wafanyabiashara, na hata wasafirishaji.“Huwa tunakuwa tunaweka muda maalum wa kupishanisha magari. Yanapita malori kwanza, lakini baadaye yatapita magari madogo. Hii ni kwa sababu ya kupunguza ah ajali au matukio ambayo yanaweza yakawa yanasababisha ah matokeo makubwa mabaya. Mfano kama malori yanapishana hata likifeli breki, madhara yake sio makubwa kama yalikuwa yanaenda kugonga gari ndogo iliyobeba abiria.”
“Foleni inaathiri sehemu kubwa ya uchumi wa Mbeya kwa sababu kwanza, inapoteza pesa. Mafuta wote tunafahamu lita saa hizi ni zaidi ya 4,000, ukikaa kwenye foleni mafuta yanatumika mengi na gharama ya maisha inaongezeka kwa mtu mmoja mmoja na kwa uchukuzi na gharama ya kibiashara inaongezeka.
Muda; sehemu ambayo ulitakiwa utumie dakika tano unajikuta umetumia saa nzima kwa sababu ya ya ya foleni, nayo unakuwa umepoteza sana na kwa jamii nzima na kwa mzunguko mzima wa Mbeya. Lakini pia foleni hii kwa staili hii imeambatana na vumbi ambayo pia inaathiri pia afya za watu ambao ukigusa afya ya mtu pia unaathiri uchumi.
Nyongeza ya hapo ya mwisho kabisa mji wetu pia pamoja na kwamba tuna foleni lakini pia hauna hauna mpangilio mzuri wa parking. Kwa hiyo watu pia tunapaki barabarani, barabara ikiwa na changamoto na watu wanapaki barabarani, maduka yame-face barabara, kwa hiyo unakuta inachangia kuongezeka kwa foleni lakini pia kukosa ile mvuto wa jiji.
Mfanyabiashara na msafirishaji wa mizigo, Salim Asas, anasema athari za barabara hiyo hazibaki Mbeya pekee kutokana na umuhimu wake katika usafirishaji wa mizigo kuelekea nchi zilizopo kwenye ukanda wa SADC.Kwa hiyo mimi kwangu mimi naona inaathiri kwa kubwa kabisa kiuchumi, na kama tungekuwa na mbunge wetu wa Mbeya anasikia hii tunavyoongea, angejitahidi kwa kweli kabisa hii barabara ya katikati ya mji eh ikumbukwe na iweze kusukumwa kwa haraka.”
“Hii barabara haina manufaa kwa ajili ya watu wa Mbeya tu. Labda ni-declare interest: mimi ni msafirishaji. Barabara ikiwa na changamoto hata wasafirishaji nao wanakuwa na changamoto. Kwa sababu hii ni ufunguo wa SADC. Magari yote yanayoenda huko yanapita hapa. Kwa hiyo hii ni interest, ni ni ni national interest. Kwa hiyo taifa lina lina manufaa na hii barabara.
Wakati foleni zikiongeza muda na gharama za usafiri, vumbi nalo limekuwa tatizo jingine kwa wakazi na wafanyabiashara. Mfanyabiashara anayefanya shughuli zake kando kando ya barabara hii anasema:Kwa mtu akitoka Iringa, akitoka Morogoro, akitoka Dar es Salaam, akitoka Songea, ana manufaa na hii barabara. Kwa hiyo barabara hii isichukulie wana Mbeya tu peke yao. Na ninafikiri katika miradi ambayo ni mikubwa mikubwa kila mikoa, ambayo labda hata kumwamsha Mheshimiwa Rais ukamwambia bwana katika miradi ambayo unaifikiria, Mkoa wa Mbeya hatahutaja huu.”
Mkaazi mwingine anasema taswira ya Jiji la Mbeya imeanza kubadilika kutokana na uwepo wa vumbi.“Vifua tunasumbuliwa, tunakohoa mara kwa mara. Kwa hiyo tunaomba mtusaidie barabara kutengeneza jamani, wananchi inatuathiri vifua. Sasa wamama kama wajasiriamali maisha yetu tumetegemea kwenye biashara tuuze, tulelee familia zetu.”
Wafanyabiashara wengine wanasema vumbi linafunika bidhaa, nyumba na maeneo yao ya biashara.“Saa hizi Mbeya siyo ile Mbeya ya Green City, saa hizi Mbeya imekuwa Mbeya ya mavumbini. Kwa hiyo unayetoka Arusha, unayetoka Mwanza ukija Mbeya usiseme naenda Green City, sema naenda Mbeya ya mavumbini. Rai yangu serikali naiomba tu ituangalie sisi wakazi wa eneo hili kwanza husika kwamba maana tunapata shida sana. Mpaka sometime tunawaza kwamba he, mbona mafua yanazidi kuongezeka?”
Dkt. Emmanuel Buberwa, daktari wa magonjwa ya ndani kutoka Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Mbeya, anasema vumbi linaweza kuathiri mfumo wa upumuaji wa binadamu.“Vumbi ni nyingi sana hivi hapa. Gari ukiosha dakika mbili tu limechafuka. Kwenye maduka humu ndio usiseme yaani. Kuoga vumbi tu! Tunaenda nyumbani unafikiri tulikuwa kulima. Sasa tunalima kweli mjini au kuna mashamba? Tunaomba Mama Samia aliangalie hili swala, tunamtegemea. Yeye ndo Rais wa wanyonge anasema haya, au aonyeshe unyonge wake hapa.”
“Vumbi linaweza kuathiri mfumo wa hewa kupitia mdomo au kupitia pua, na likiingia kwenye njia ya hewa huwa kuna vinyeleo vidogo vidogo ambavyo kazi yake ni kukamata vitu vyote ambavyo ni vigeni kwenye mwili ambavyo havihitajiki, kama moshi, kama hivyo vumbi, na kadhalika.
Kwa hiyo linapokuwa lipo vumbi la kawaida huwa mwili unaweza kuliteka kimya kimya alafu baadaye ukaweza kulitoa nje pengine hata bila bila kuwa na taarifa, lakini likiwa limekuwa jingi maanake mwili lazima kiasi kwamba lazima mwili u-initiate mechanism mbalimbali ili liweze kutoka, ambapo ya kwanza ni kuzalisha maji maji mengi ambapo inapelekea mtu kupata mafua, lakini pia mwili unakufanya mtu usikie chafya za mara kwa mara ili kuweza kuli-expel out.
Na lile ambalo litafanikiwa kuingia mpaka kwenye mapafu, litaenda kuyafanya yale mapafu yaumwe, tunaita inflammation kwa sababu ni kitu kipya, ndo mtu anaweza akapata hata nimonia ya watu wazima. Pamoja na hayo, bado pia hata mle mle tu kwenye njia ya hewa ambapo linapita inaweza ikasababisha ile njia ikawa inaumwa inapata inflammation za mara kwa mara kupelekea mtu kupata kikohozi na mafua ya kujirudia, na wakati mwingine inaweza ikatengeneza kitu kinaitwa pumu ya watu wazima.
Kwa hiyo ina madhara makubwa, kwa hiyo tunashauri watu kama mazingira walipo kuna watu wanauza bidhaa zao pembezoni mwa barabara, wengine ndo hivyo madereva, makondakta, wavae barakoa ili kwa lengo la kukinga vumbi lisiingie kwenye njia zao za hewa. Kwa sababu hatuwezi tukawashauri watu waache kutoka, watu watoke wakapambane ila wavae barakoa japo haiondoi 100% ila inapunguza kwa kiwango ambacho ni kizuri.
Kwa wananchi wa Mbeya, mradi uliotarajiwa kupunguza changamoto za usafiri umeendelea kuwa chanzo cha gharama nyingine: muda unaopotea kwenye foleni, ongezeko la matumizi ya mafuta, mazingira yenye vumbi, usumbufu kwa biashara na hatari za usalama.Pamoja na hayo mtu akijisikia dalili zote za magonjwa haya ya hewa awahi kutumia dawa ili kuepusha mwili kutengeneza magonjwa mengine kama ambavyo nimekwambia, hiyo pumu ya ukubwani.”
Meneja wa Wakala wa Barabara Mkoa wa Mbeya, Mhandisi Suleiman Bishanga, anabainisha kuwa mkandarasi ameanza kazi mara baada ya kulipwa stahiki zake.
Wakati serikali ikiahidi kuendelea na mradi huo, wananchi wa Jiji la Mbeya bado wanataka kujua ni lini hasa barabara hiyo itakamilika, na lini watakapoanza kuona manufaa yaliyokusudiwa tangu ujenzi wake ulipoanza mwaka 2023.“Plani ya mkandarasi kwa daraja hili atafanya usiku na mchana ili liweze kurudi kwenye normal kuondoa adha ambayo iko kwenye maeneo haya ya vumbi lakini na adha ya watu kuwa na foleni. Tunashukuru Mheshimiwa Rais kwa sababu zile fedha amezileta kwa wakati ambao sasa mvua imekatika lakini na kazi ndo zinatakiwa kuanza.”
Sehemu ya pili ~ Nini kinachokamisha Mradi wa Njia 4 Mbeya kukamilika? Sababu zimekuwa nyingi na zinazokinzana
Sehemu ya tatu ~ Wachimbaji madini wadogo wa Saza - Songwe hawatendewi haki, leseni imetolewa mara 2 ili mkubwa awaondoe
ANDIKO LA: Heneliko Malo
Makala imeandaliwa na Mwandishi anayeshiriki katika programu maalum ya kukuza uandishi wa maslahi kwa umma (Public Interest Journalism Fellowship) inayoratibiwa na UTPC kwa kushirikiana na IMS