Miradi ya Barabara kutokamilika kumesababisha Athari nyingi Mbeya, kiuchumi, afya na Kijamii

UTPC

Journalists' Union
Joined
Apr 17, 2026
Posts
51
Reaction score
38
Kwa zaidi ya miaka miwili, wananchi wa Jiji la Mbeya wanaoishi na kufanya shughuli zao kando kando ya barabara ya njia nne kutoka Nsalaga hadi Ifisi, wameendelea kusubiri kukamilika kwa mradi huo waliyotarajia ungekuwa suluhisho la msongamano wa magari na kurahisisha usafiri, lakini badala yake wamejikuta wakikabiliwa na foleni, mashimo, vumbi na ajali.

Uchunguzi wa Bomba FM uliofanywa kwa zaidi ya miezi mitatu umebaini kuwa kuchelewa kwa mradi huo kumeongeza adha kwa wananchi, wafanyabiashara na watumiaji wa barabara, huku baadhi ya maeneo ya mradi huo yakiwa katika hali inayohatarisha usalama na kuathiri shughuli za kila siku.
​
Mradi huo wenye urefu wa kilomita 29 ulianza kutekelezwa Machi mwaka 2023 kwa gharama ya shilingi bilioni 184 na ulipangwa kukamilika ndani ya miezi 24. Hata hivyo, muda huo umepita huku ujenzi ukiwa bado unaendelea.

Barabara hiyo ni muhimu kwa Jiji la Mbeya kutokana na nafasi yake katika kurahisisha usafiri wa watu na mizigo, lakini kuchelewa kwake kumewaweka wananchi katika mazingira ambayo hawakutarajia baada ya kuanza kwa mradi.

Katika eneo la Mama John baadhi ya wananchi wanasema sehemu za barabara hiyo zimeachwa na mashimo makubwa yanayofanya usafiri kuwa mgumu na kuongeza hatari kwa watumiaji.

Mkaazi mwingine anasema hali hiyo imekuwa ikiathiri pia wafanyabiashara wanaofanya shughuli zao kando kando ya barabara.

Mbali na hali ya barabara, wananchi wanaendelea kuhusisha mazingira ya usafiri katika maeneo hayo na ongezeko la hatari za ajali. Katika uchunguzi wake, Bomba FM ilibaini matukio ya ajali yaliyoongeza hofu miongoni mwa wananchi kuhusu usalama wa barabara katika Jiji la Mbeya. Juni 8 mwaka 2025 watu 28 walifariki dunia na wengine 12 kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari manne kwenye mteremko wa Mlima Iwambi jijini Mbeya, na hii ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya.
​
Katika maeneo yanayopitiwa na mradi huo, foleni imekuwa sehemu ya maisha ya kila siku ya wananchi. Mkaazi mmoja wa Mbeya anasema msongamano wa magari umeambatana pia na ajali za pikipiki na bajaji.

Madereva wa daladala nao wanasema foleni zimekuwa zikiongeza muda wa safari na kuathiri ratiba zao za kila siku.

“Foleni hii inasubiriwa kwa muda mrefu sana hapa. Unafika hapa saa 12:00 jioni jam imeanza. Nyumbani umetoka saa 11:00, hapa unakuta wanamaliza saa nzima jam. Tusaidie tu.”
Mhandisi Rajabu Ngulikwa, Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Mbeya, anasema utaratibu wa kuyapitisha magari kwa zamu umewekwa ili kupunguza uwezekano wa kutokea kwa ajali zaidi.

Kwa upande wa uchumi, mtaalamu wa uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe kampasi ya Mbeya, Dkt. Stewart Mbegu, anasema foleni zinaongeza gharama kwa wananchi, wafanyabiashara, na hata wasafirishaji.




Kwa hiyo mimi kwangu mimi naona inaathiri kwa kubwa kabisa kiuchumi, na kama tungekuwa na mbunge wetu wa Mbeya anasikia hii tunavyoongea, angejitahidi kwa kweli kabisa hii barabara ya katikati ya mji eh ikumbukwe na iweze kusukumwa kwa haraka.”
Mfanyabiashara na msafirishaji wa mizigo, Salim Asas, anasema athari za barabara hiyo hazibaki Mbeya pekee kutokana na umuhimu wake katika usafirishaji wa mizigo kuelekea nchi zilizopo kwenye ukanda wa SADC.


Wakati foleni zikiongeza muda na gharama za usafiri, vumbi nalo limekuwa tatizo jingine kwa wakazi na wafanyabiashara. Mfanyabiashara anayefanya shughuli zake kando kando ya barabara hii anasema:

“Vifua tunasumbuliwa, tunakohoa mara kwa mara. Kwa hiyo tunaomba mtusaidie barabara kutengeneza jamani, wananchi inatuathiri vifua. Sasa wamama kama wajasiriamali maisha yetu tumetegemea kwenye biashara tuuze, tulelee familia zetu.”
Mkaazi mwingine anasema taswira ya Jiji la Mbeya imeanza kubadilika kutokana na uwepo wa vumbi.

Wafanyabiashara wengine wanasema vumbi linafunika bidhaa, nyumba na maeneo yao ya biashara.

Dkt. Emmanuel Buberwa, daktari wa magonjwa ya ndani kutoka Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Mbeya, anasema vumbi linaweza kuathiri mfumo wa upumuaji wa binadamu.





Pamoja na hayo mtu akijisikia dalili zote za magonjwa haya ya hewa awahi kutumia dawa ili kuepusha mwili kutengeneza magonjwa mengine kama ambavyo nimekwambia, hiyo pumu ya ukubwani.”
Kwa wananchi wa Mbeya, mradi uliotarajiwa kupunguza changamoto za usafiri umeendelea kuwa chanzo cha gharama nyingine: muda unaopotea kwenye foleni, ongezeko la matumizi ya mafuta, mazingira yenye vumbi, usumbufu kwa biashara na hatari za usalama.

Meneja wa Wakala wa Barabara Mkoa wa Mbeya, Mhandisi Suleiman Bishanga, anabainisha kuwa mkandarasi ameanza kazi mara baada ya kulipwa stahiki zake.

Wakati serikali ikiahidi kuendelea na mradi huo, wananchi wa Jiji la Mbeya bado wanataka kujua ni lini hasa barabara hiyo itakamilika, na lini watakapoanza kuona manufaa yaliyokusudiwa tangu ujenzi wake ulipoanza mwaka 2023.

Sehemu ya pili ~ Nini kinachokamisha Mradi wa Njia 4 Mbeya kukamilika? Sababu zimekuwa nyingi na zinazokinzana
Sehemu ya tatu ~ Wachimbaji madini wadogo wa Saza - Songwe hawatendewi haki, leseni imetolewa mara 2 ili mkubwa awaondoe

ANDIKO LA: Heneliko Malo
Makala imeandaliwa na Mwandishi anayeshiriki katika programu maalum ya kukuza uandishi wa maslahi kwa umma (Public Interest Journalism Fellowship) inayoratibiwa na UTPC kwa kushirikiana na IMS
 

Attachments

Tanroads na TECU ni baba mmoja mama mmoja unamwacha Dullah amsimamie Abdallah.
 
Duh!
Mradi umechukua muda!
Sasa kutokana na ajali za mara kwa mara, nawashauri Tanroads, pale Iwambi mpaka Mbalizi, bara bara ya kati kati wanyanyue tuta urefu wa mita moja ili magari madogo ya kwenda na kurudi yapite juu ya tuta na malori ya kwenda na kurudi bara bara yake itakuwa ya chini.
Hii itaepusha maroli kuyagonga magari madogo pindi yanapofeli breki au yanapofeli kupanda mlima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…