MIRADI YA ELIMU INAENDELEA KUTEKELEZWA NA AWAMU YA SITA

MIRADI YA ELIMU INAENDELEA KUTEKELEZWA NA AWAMU YA SITA

Nyabukika

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2022
Posts
1,440
Reaction score
1,046
Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imetenga shiligi bilioni 752 kwa ajili ya kutekeleza shughuli mbalimbali kupitia Mradi wa Elimu ya juu kwa mageuzi ya kiuchumi (HEET).
Shughuri zitakazotekelezwa kupitia mradi huu ni ujenzi wa miundombinu mipya na kukarabati iliyopo ikiwemo, Kumbi za mihadhara na madarasa 130, maabara na karakana 108, mabweni 34 na ofisi 23.

Pia kupitia mradi huu serikali imepanga kujenga kampasi mpya 14 katika mikoa ya Dodoma, Kagera, Katavi, Kigoma, Lindi, Manyara, Mwanza, Rukwa, Ruvuma, Simyu, Singida, Shinyanga, Tabora na Tanga.

Vilevile serikali imepanga kujenga chuo kikuu cha kisasa cha TEHAMA mkoani Dodoma na chuo kikuu cha kilimo na Teknolojia cha Mwalimu Julius Nyerere mkoani Mara pamoja na kusomesha wahadhiri katika shahada za uzamivu wa shahada za umahiri ili kuwajengea uwezo katika fani.
Rais Samia Suluhu Hassan anaendelea kuimarisha sekta ya elimu
 
Back
Top Bottom