Nyanswe Nsame
Senior Member
- Jul 9, 2019
- 165
- 181
Miradi ya Meli, SGR na Maji yakwama Mwanza, pesa zinapigwa na Serikali yagoma kupeleka pesa
Miradi mikubwa mitatu ya kimkakati iliyopo jijini Mwanza iliyoanzishwa na Serikali ya awamu ya tano chini ya hayati John Pombe Magufu, imekwama kutokana na ukosefu wa fedha.
Miradi iliyokwama ni pamoja na mradi wa ujenzi wa meli kubwa ya ghorofa ya MV Victoria, Ujenzi wa kipande cha Reli ya Mwanza - Isaka na mradi wa maji Butimba.
Mradi wa meli hiyo yenye uzito wa tani 3500 itakayotoa huduma katika Ziwa Victoria imejegwa kwenye chelezo chenye uwezo wa kubeba meli yenye uzito wa hadi tani 4,000.
Chelezo hicho pia kitatumika kujengea meli mpya ya mizigo yenye uwezo wa kubeba tani 3,000 na kukarabati meli ya mafuta ya MT. Nyangumi yenye uwezo wa kubeba lita 410,000 pamoja na kukarabati meli ya msaada ziwani ya MT. Ukerewe.
Mikataba yote ya ujenzi inagharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 160 kutoka shilingi bilioni 84 iliyokuwa katika mkataba wa awali kabla ya kusimama mara kwa mara serikali ikidunduliza pesa za mikopo na walipa kodi.
Kuhusu ujenzi wa Reli ya kisasa ya mwendo kasi (SGR) kutoka Mwanza - Isaka wakandarasi wa kichina wanaojenga reli hiyo wameondoka site, leo lakini siku leo Mei 27 Kamati ya siasa ya CCM imefika kukagua mradi huo na kusifia kwamba kasi ya ujenzi ni kubwa jambo ambalo ni la uongo.
CCM imepita katika miradi hiyo tajwa hapo juu na kusifia ujenzi huo, licha ya wakandarasi kuondoka eneo la kazi kutokana na kukosekana kwa fedha licha ya kusingizikio kikubwa kikiwa ni ucheleweshaji wa vifaa kutoka nje.
Kipande hicho cha tano cha Mwanza - Isaka, kwa ujumla kilipaswa kukamilika mwezi huu (bado siku 4) mwezi kuisha tunasubiri kuona je, utakamilika?
Mradi mwingine ni mradi wa maji Butimba, mradi ambao unasifiwa kila kukicha lakini nao haujakamilika.
Mradi huo ulianza kutekelezwa februari 2021 na ulitakiwa kuwa kukamilika mwaka jana Oktoba cha kushangaza mradi umekwama licha ya kufanyiwa majaribio.
Mradi huo umegharimu shilingi bilioni 70, ambapo pia leo Mei 27, kamati ya siasa mkoa, imepita kukagua na kuusifia huku watanzania wakiambulia maji ya chumvi na tope kutoka ziwa Victoria.
Watu wanauliza pesa zinazotolewa na Serikali na 'machawa' ya CCM kusifia pesa hizo zinaenda wapi, miradi inakwama na hakuna hatua zozote zilizopo za kuikwamua.