Miradi ya Meli, SGR na Maji yakwama Mwanza, pesa zinapigwa na Serikali yagoma kupeleka pesa

Miradi ya Meli, SGR na Maji yakwama Mwanza, pesa zinapigwa na Serikali yagoma kupeleka pesa

Watu wanasosomola tu hawajali, hata hela za mikopo na misaada wao wanasosomola tu.

Ndio yule Mwamba aliwaambia hela zipo tukamuona mwehu kumbe anajua mengi.

Wizi, Rushwa, Incompetency kila mahala hivi sasa, warsha, makongamano, ziara za hovyohovyo, mikutano, mafunzo hivi sasa vimetamalaki kila kona.
Hakuna kipindi ufisadi mkubwa ulifanyika kama kipindi cha magufuuli
 
Meli inasubiri vifaa kama viti, fenicha za ndani za finishing, zimeagizwa ughaibuni, viko kwenye meli baharini vinakuja, asilimia 95 imekamilika.

Miradi inaenda vizuri sana.

Halafu umejiandaa kusafirisha bishara gani katika SGR? Au ndio wale hawalimi pamba, tumbqku, hawavui samaki wqpeleke nje yabukanda wa ziwa, wanataka tu kuona treni inatembea halafu haimsaidii kiuchumi
CCM ni laana
 
Jengo la uwanja wa ndege lilisainiwa mkataba kwa gishindo na magreda sasa hivi kimya Msukuma na Tabasamu tokezeni tuwasikie vinginevyo mtajivunjia heshima uchaguzi unakuja
Tutamkumbuka Jiwe Kwa mabaya yake
 
Kama wanaokula pesa Ni hao hao wasukuma walengwa, sisi tuseme Nini.
Kwa kuwasaidia tu msukuma mwenzao makonda apelekwe huko asimamie.
 
Hakuna kipindi ufisadi mkubwa ulifanyika kama kipindi cha magufuuli
Hizo ni nadharia tu ambazo tunalazimishwa kuzikubali, lakini hakuna uhalisia wowote.

Serikali ilibana matumizi, serikali ilidhibiti rushwa na wizi, matokeo yake serikali ikapata hela zakufanya mambo meengi ambayo Leo hii yanasuasua maana wizi umetamalaki kila kona na serikali haina hela inaishia kukopakopa na kuomba misaada huku na kule.
 
Miradi ya Meli, SGR na Maji yakwama Mwanza, pesa zinapigwa na Serikali yagoma kupeleka pesa

Miradi mikubwa mitatu ya kimkakati iliyopo jijini Mwanza iliyoanzishwa na Serikali ya awamu ya tano chini ya hayati John Pombe Magufu, imekwama kutokana na ukosefu wa fedha.

Miradi iliyokwama ni pamoja na mradi wa ujenzi wa meli kubwa ya ghorofa ya MV Victoria, Ujenzi wa kipande cha Reli ya Mwanza - Isaka na mradi wa maji Butimba.

Mradi wa meli hiyo yenye uzito wa tani 3500 itakayotoa huduma katika Ziwa Victoria imejegwa kwenye chelezo chenye uwezo wa kubeba meli yenye uzito wa hadi tani 4,000.

Chelezo hicho pia kitatumika kujengea meli mpya ya mizigo yenye uwezo wa kubeba tani 3,000 na kukarabati meli ya mafuta ya MT. Nyangumi yenye uwezo wa kubeba lita 410,000 pamoja na kukarabati meli ya msaada ziwani ya MT. Ukerewe.

Mikataba yote ya ujenzi inagharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 160 kutoka shilingi bilioni 84 iliyokuwa katika mkataba wa awali kabla ya kusimama mara kwa mara serikali ikidunduliza pesa za mikopo na walipa kodi.

Kuhusu ujenzi wa Reli ya kisasa ya mwendo kasi (SGR) kutoka Mwanza - Isaka wakandarasi wa kichina wanaojenga reli hiyo wameondoka site, leo lakini siku leo Mei 27 Kamati ya siasa ya CCM imefika kukagua mradi huo na kusifia kwamba kasi ya ujenzi ni kubwa jambo ambalo ni la uongo.

CCM imepita katika miradi hiyo tajwa hapo juu na kusifia ujenzi huo, licha ya wakandarasi kuondoka eneo la kazi kutokana na kukosekana kwa fedha licha ya kusingizikio kikubwa kikiwa ni ucheleweshaji wa vifaa kutoka nje.

Kipande hicho cha tano cha Mwanza - Isaka, kwa ujumla kilipaswa kukamilika mwezi huu (bado siku 4) mwezi kuisha tunasubiri kuona je, utakamilika?
Mradi mwingine ni mradi wa maji Butimba, mradi ambao unasifiwa kila kukicha lakini nao haujakamilika.

Mradi huo ulianza kutekelezwa februari 2021 na ulitakiwa kuwa kukamilika mwaka jana Oktoba cha kushangaza mradi umekwama licha ya kufanyiwa majaribio.

Mradi huo umegharimu shilingi bilioni 70, ambapo pia leo Mei 27, kamati ya siasa mkoa, imepita kukagua na kuusifia huku watanzania wakiambulia maji ya chumvi na tope kutoka ziwa Victoria.

Watu wanauliza pesa zinazotolewa na Serikali na 'machawa' ya CCM kusifia pesa hizo zinaenda wapi, miradi inakwama na hakuna hatua zozote zilizopo za kuikwamua.
Maza kazidiwa na majangili
 
Meli inasubiri vifaa kama viti, fenicha za ndani za finishing, zimeagizwa ughaibuni, viko kwenye meli baharini vinakuja, asilimia 95 imekamilika.

Miradi inaenda vizuri sana.

Halafu umejiandaa kusafirisha bishara gani katika SGR? Au ndio wale hawalimi pamba, tumbqku, hawavui samaki wqpeleke nje yabukanda wa ziwa, wanataka tu kuona treni inatembea halafu haimsaidii kiuchumi
Story nyingi vitendo zero, kwani hawakujua hivyo viti na finishing vinahitajika wakati wana design hiyo meli, acheni excuses za kipuuzi, ni wizi na uzembe tuu au hakuna pesa, uwongo wa kifala kama huu unaudhi sana
 
Subiri mambo mazuri, watu wenye laana huwa wanapenda kulalamika
 
Back
Top Bottom