Miradi ya PPP iliyopo katika tovuti ambayo yahitaji wawekezaji wa nje, kwanini wawekezaji wakimbilia Tanesco pekee ambayo haimo hata kwenye orodha?

Baada ya ujenzi wa JNHPP na uzalishaji wa umeme kutosheleza, sasa mipango ya kula jasho la watanzania kupitia wageni inaanzishwa.
Kwa akili ndogo kabisa, kama tumeweza kujenga bwawa, miundombinu ya kusafirisha ipo kwa kiasi fulani, kwa nini tusiendelee kujenga na kuboresha miundombinu ya kusambaza wenyewe?
Kuhalalisha utapeli huu, umeme utaanza kukatwa mara kwa mara.
PPP itumike kwenye ujenzi wa barabara, viwanda vya kufua vyuma na umeme kwa makaa ya mawe, kilimo n. k.
Hii ni sawa na kuwapa mbwa chakula cha watoto.
Mikataba ya IPTL, Richmond na hata SONGAS imetoa faida au hasara?
Kwa nini isiwe ni wale wale wanazunguka pale palepale wakitegemea maamuzi yale yale ya kuingia mikataba ya kipuuzi yakipambwa na nyimbo nzuri za PPP?
 
SAMIA NI KIBARAKA WA WAHALIFU ALIYE FANIKIWA KUWA KIONGOZI ...HIVYO ATATUMIKA NA HSO WAHALIFU AMBAO WENGI WAO NI RAIA FEKI ...KUFSNIKISHA KILA AINA YA UHUNI
 
SAMIA NI KIBARAKA WA WAHALIFU ALIYE FANIKIWA KUWA KIONGOZI ...HIVYO ATATUMIKA NA HSO WAHALIFU AMBAO WENGI WAO NI RAIA FEKI ...KUFSNIKISHA KILA AINA YA UHUNI
Ni pale unaposikia wakisema tunakuwa na amani na serikali yenye sheria na masharti rafiki.
 
Ppp haijazuia wawekezaji wa ndani
 
Kamishina wa PPP ni Kafulila naungana na. Mbunge Muhongo akiwa waziri aliyemuita Kafulila tumbili
 
Ppp haijazuia wawekezaji wa ndani
Lakini mabadiliko ya sheria inohusiana na wawekezaji imefanywa kwa kuweka mazingira mazuri zaidi kwa wawekezaji wa nje kupata direct access kwa miradi iliyopo.

Kwa mfano ukisoma kwa makini maono ya PPP ni kwamba benki ya Dunia imepewa access ya kuona regulations na miongozo au Guidelines zinooongoza wawezekaji wa nje zaidi kuliko wa ndani.

Pia mfano mwingine ni kurekebisha sheria (PPP Act Amendment) ambapo makampuni ya nje yatapeleka madai yoyote ya kisheria kwenye mahakama za kimataifa, kupewa unafuu wa kulipa kodi, kupata access ya kupata myaji ambao upo kwenye mfuko uitwao Viability Gap Funding VGF, fedha ambazo kiufundi au techically zotoka moja kwa moja Benki ya Dunia.

Sasa wadhani Benki ya Dunia itaipatia kampuni ya Kitanzania fedha za VGF kama mtaji, wakati tuna benki ya maendeleo ya Afrika ambayo nimeona haizungumziwi kabisa katika uwekezaji unozungumziwa na PPP na ingeweza kutumia kama kiungo kwa wawekezaji wa kitanzania?

Hapo juu pia kuhusu kurekebisha sheria kunazipa hizi kampuni uwezo wa kuidai fedha nyingi serikali ya Tanzania endapo utawala mpya utajaribu kurekebisha sheria za uwekezaji huko mbele.

Hivyo ni kweli wawekezaji wa ndani hawajazuiwa lakini hawana nafasi ya kushindana na wawekezaji wa nje wenye vifua vinene vilojaa madola ya kuja kuwekeza kama mitaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…