Miranda rights Tanzania

Miranda rights Tanzania

femalepilot

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2014
Posts
258
Reaction score
118
Habari zenu humu ndani,ningependa kujua kama kwa Tanzania,unapowekwa chini ya ulinzi unakua entitled to miranda rights?
 
Miranda rights ni sehemu ya utaratibu wa police wa marekani wakati wa ukamataji wa mtuhumiwa,kumjulisha haki zake kabla ya kukamatwa ikiwapo haki ya kubaki kimya wakati wote na kuwa ana haki ya mwanasheria(kuwakilishwa) na iwapo atazungumza chochote basi kinaweza kutumika kama ushahidi dhidi yake mbele ya mahakama.

Miranda rights zilitokana na maamuzi ya mahakama ya juu ya marekani kwenye shauri la Miranda v Arizona, 384 U. S, 436 ambapo mahakama iliamua kuwa, tamko lolote la mtuhumiwa mbele ya askari,wakati wa kukamatwa kwake na kipindi chote kabla ya kufikishwa mahakamani vitapokelewa na mahakama kama ushahidi, ikiwa tu mtuhumiwa alijulishwa haki zake(Miranda rights)...pia alizielewa, isipokuwa aliamua kuzipuuza.

Miranda rights(warning) ilianza kutumika zaidi marekani mara baada ya mapinduzi (American revolution-1770s) ambapo wamarekani walianza kuzibadili sheria nyingi za mtawala wao wa zamani(muingereza). Hivyo, Miranda rights hutumika zaidi kwenye nchi za anglo-american na baadhi zilizoamua kufuata utaratibu kama wa marekani.

Kwa Tanzania, sawa na nchi nyingine zilizocopy na kufuata utaratibu wa sheria wa muingereza (commonwealth countries), haki ya kubaki kimya, haki ya kuwakilishwa na mwanasheria kwa mtuhumiwa zimeendelea kuwepo japo si kwa umakini wa sheria. Hivyo, kwasababu Tanzania hatukurithi na kupokea utaratibu wa sheria za marekani kama tulivyozipokea zile za uingereza tarehe 22nd July 1920, unapoamatwa/kuwekwa chini ya ulinzi hauwi-entitled to miranda rights/warnings bali haki za mtuhumiwa au mtu anayekamatwa na polisi zinatajwa kwenye katiba(Bills of rights), hivyo unakuwa entitled to Right to equality before the law.

Kwa Tanzania, matamko yote ya mktuhumiwa wakati wa kuwekwa kwake chini ya ulinzi hayasimami na kupokelewa kama ushahidi kamili,ni lazima matamko yote yathibitishwe na kuambatana na ushahidi mkuu,tofauti na marekani ambapo matamko pia huunda sehemu ya ushahidi wa kujitegemea (Ref.Miranda v Arizona).

Hii imetajwa kwenye Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977, Ibara ya 13 (6) (b), pia kifungu cha 117 cha sheria ya utaratibu wa makosa ya jinai (Cap 20 R.E 2002)-kuwa,mtu kabla ya kuwekwa chini ya ulinzi anapaswa kujulishwa sababu za yeye kuwekwa chini ya ulinzi,pia kuoneshwa hati ya kuwekwa kwake chini ya ulinzi, pia kwenye sheria za kimataifa ambapo Tanzania imeridhia-kwa mfano Geneva Convention, the Covenant on civil and political rights na nyinginezo...kuwa kila mtu ana haki ya kuwakilishwa na mwanasheria huru na mbele ya chombo huru cha haki.

Kwa ujumla, Tanzania hatuna Miranda rights, tuna Bill of Rights...yenye baadhi ya matamko yafananayo na Miranda rights.
 
Asante ndugu,nimeelewa vizuri sana
 
Nashukuru kwa literature nzuri iliyotelewa na mchangiaji aliyepita na kwa ufasaha wake pia wa kunukuu baadhi ya vifungu vya sheria zetu. Lakini kwa maana ya sasa hivi Miranda ni yale maelezo mtuhumiwa anachukuliwa akiwa kituo cha polisi au mbele ya mlinzi wa amani na ambayo yanaweza kutumika kama ushahidi dhidi yake. Kuna vitu vya kuzingatia wakati wa kuchukua maelezo hayo na yaweze kuwa na nguvu ya kisheria kama vile haki ya kuwa na ndugu au mwanasheria, yatolewe mtu akiwa huru , akishatoa maelezo hayo asome au asomewe na asaini etc. Tuna vifungu vya sheria vya namna ya kuchukua maelezo hayo kama ss 57 na 58 vya mwenendo wa makosa ya jinai sura ya 20 mapitio ya mwaka 2002. Taratibu zikifuatwa vizuri na kama mtuhumiwa alikiri kosa basi hakuna ushahidi mzuri zaidi ya huo , ila kama pengine aliteswa au kunyimwa haki nyingine na maelezo hayo yakiletwa mahakamani anaweza omba mahakama itupilie mbali maelezo hayo chini ya kifungu 169 cha CPA. Hivyo sheria ya Miranda ipo hapa Tanzania na inafanya kazi. Hapa nimeeleza kwa uchache tuu
 
much oblige
 
kama kawa
 
Back
Top Bottom