Miranda warning

kishumbaz

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2015
Posts
1,183
Reaction score
1,619
hivi hii kitu haiapply kwenye sheria zetu! mtuhumiwa anahojiwa na polisi publicly... anaropoka! coercive interrogation tactics kwa mtuhumiwa....inatufundisha nini kwa RAIA juu ya haki za mtuhumiwa? wataalam wa sheria naomba msaada wa elimu.
 
Miranda haipo rasmi katika sheria zetu, japokuwa indirectly ipo, kwa maana kwamba Kinachotetewa ua kulindwa katika mirara (mfano ya marekani) hata hapa tanzania kinalindwa na kutetewa, ila kwa sheria na taratibu tofauti.

Mtu kuhojiwa publicly ni kinyume kabisa na taratibu za interrogation na hata intelligence ya jeshi. Hii inatokea tu kwa sababu ya ulimbukeni wa baadhi ya watawala wenye mamlaka hayo. aina hii ya mahojiano haina nguvu yeyote kisheria na mazungumzo au matamko ya mtuhumiwa hayawezi kutumiwa kama ushahidi mahakamani.

Mbinu hii si nzuri hata kidogo kwa mtuhumiwa. Mtuhukiwa ananyimwa haki yake ya usiri (confidence) na inamwondolea imani ya kutendewa haki pale anapopelekwa mahakamani. Ingawa mtuhumiwa anayo haki na kinga kisheria kutokuongea chochote (kunyamaza) katika mahojiano ya namna hii, raia wengi hawalifahamu hili kwa hiyo wanajikuta wananaswa na na washitaki wao bila wao kutarajia.

aina hii ya mahojiano ni udhalilishaji na kinyume cha haki za kiraia. Mahojiano ya namba hii ni halali pale tu yanapoendeshwa katika sehemu maalum au mahakamani. Mahojiano haya yanaipa jamii mtazamo hasi dhidi ya mtuhumiwa, hata kama ikitokea mahakama ikamkuta hana hatia. kwa kifupi mahojiano haya ni batili katika misingi ya sheria.
 
shukran sana mkuu..kwa elimu...ubarikiwe!
 
hivi hii kitu haiapply kwenye sheria zetu! mtuhumiwa anahojiwa na polisi publicly... anaropoka! coercive interrogation tactics kwa mtuhumiwa....inatufundisha nini kwa RAIA juu ya haki za mtuhumiwa? wataalam wa sheria naomba msaada wa elimu.
Haha Mkuu uko Deep sana....

Kumbe Police hakuna jamaa Miranda zake?

Vp alimuanza na Terry Stop au?

Hahah wacha America aendelee kutawala dunia bana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu ww kama Attorney sio wa kutakiwa kulalamika ...go there n change the Law...set precedents!

Fanya suppression hearing ...si kuna section 169 inaongelea exclusion of evidence obtained in violation of the law??

Use it. Advance your arguments under Reg 56(1) za ettiquette

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…