Mirathi kwa watoto nje ya Ndoa

Kwenye kesi moja huko Kenya kuanzia kadhi hadi mahakama kuu walikuwa na mtazamo Kama wako lakini maamuzi yao yalikuja kutupiliwa mbali na mahakama ya rufaa.Mke mkatoliki na watoto wake wakatoliki waliokuwa na baba muislamu bila ndoa ,waliamuliwa kumrithi baba yao.Katiba ya Kenya ni Kama yetu inahimiza usawa na kupinga ubaguzi.
 
Mzigo huo,soma kama Kuna ugumu wapo wajuba hapa watasaidia
 
Oya hukumu mbona haifunguki hii
 
Mzigo huo,soma kama Kuna ugumu wapo wajuba hapa watasaidiaView attachment 1666201
Huo mfano wako hauingii hapo kwa sababu nimeshasema issue sio marehemu kuwa Mwislamu, na ndo maana nikasema kabla ya kutumika sheria ya Kiislamu, mahakama inatakiwa kujiridhisha ikiwa marehemu alikuwa Mwislamu anayeuishi Uislamu alikuwa ni Mwislamu Jina tu na kwahiyo kuna watu wanataka kutumia kete ya Uislamu ili kuwatupa wengine nje!!

Huo mfano wako haujitoshelezi kwa sababu ulitakiwa kuonesha marehemu alikuwa ni mwislamu aliyekuwa anaishi kwenye misingi ya Uislamu na sio just because he's a muslim! Lakini kwa upande mwingine, pia ulitakiwa kueleza sheria za mirathi nchini Kenya zinasemaje kwa sababu Tanzania kuna sheria za aina tatu zinatumika ambazo ni sheria ya serikali/secular law, sheria ya kimila na sheria ya kiislamu!!
 
Google hiyo kesi usome utapata kila kitu.
 
Google hiyo kesi usome utapata kila kitu.
Sioni sababu ya ku-Google kwa sababu ni wewe mwenyewe ndie umeweka hiyo screenshot na kwahiyo ni wewe mwenyewe ndie ulitakiwa kuweka taarifa zilizokamilika! Binafsi sina haja ya kufanya hivyo kwa sababu tayari nafahamu, linapokuja suala la mirathi, moja ya sheria zinazotambulika Tanzania ni Islamic Law!!! Aidha, nimeshasema ni mazingira yapi Islamic Law inaweza kupigwa chini hata kama marehemu alikuwa Mwislamu!
 
Matakwa ya katiba ya nchi inayozuia ubaguzi,sheria ya mtoto inatambua usawa wa watoto wote ,matamko ya haki za binadamu yote yanatambua usawa na haki za binadamu.Katika kesi ya hizo mirathi zenye kuhusu mtoto wa out of wedlock yatapelekwa pale ambapo mtoto anatambulika na mahakama inayomtambua.Nikukumbushe pia kwamba sheria namba moja ya nchi ni katiba ya nchi,sheria nyingine yoyote inayokinzana nabkatiba itawekwa kando popote pale.
 
Matakwa ya katiba ya nchi inayozuia ubaguzi,sheria ya mtoto inatambua usawa wa watoto wote ,matamko ya haki za binadamu yote yanatambua usawa na haki za binadamu.Katika kesi ya hizo mirathi zenye kuhusu mtoto wa out of wedlock yatapelekwa pale ambapo mtoto anatambulika na mahakama inayomtambua.Nikukumbushe pia kwamba sheria namba moja ya nchi ni katiba ya nchi,sheria nyingine yoyote inayokinzana nabkatiba itawekwa kando popote pale.Najua hapa utabisha na mimi sitatumia tena muda wangu kufafanua ila siku ukikutana nayo utanikumbuka.
 
Inapokinzana na katiba ,hata sheria iliyotungwa na bunge ikikinzana na katiba inapigwa chini.
 
Inapokinzana na katiba ,hata sheria iliyotungwa na bunge ikikinzana na katiba inapigwa chini.
Unaweza kutaja sheria inayokiukwa kwenye katiba?! Wakati I doubt kama unaweza kutaja hicho kifungu, katiba hiyo hiyo ibara ya 19 inazungumzia uhuru wa mtu kuamini dini atakayo! Na hapo hapo ndogo ya 1 inasema "Kila mtu anastahili kuwa na uhuru wa mawazo, imani na uchaguzi katika mambo ya dini.."

Sasa unaweza kuwakataza vipi Waislamu wasitumie sheria ya kiislamu kwenye mirathi kama inavyotakiwa na imani yao wakati pia katiba imewapa uhuru wa uchaguzi wa mambo ya dini?
 
Tuzae wisely.

Mtoto hujacheza naye, hajakufulia nguo, hujamtuma dukani, n.k anakuja kugawana sawa na wale waliokunywesha dawa ukiwa mgonjwa, kukufulia, kukupikia, kuzungumza nawe daily, kukuchekesha, kukutoa stress n.k
Na hisi hoja yako ni swali lingine hili kutokana na matakwa ya kisheria, hapa inaongelewa haki za mtoto awe amekuhudumia au hajakuhudumia, awe ameishi nawe hajaisgi nawe enzi za uhai wa marehemu basi juwa watoto hao wana haki ya msingi ya kurithi mali,


Swali lako labda sasa ukaliweka kwa michepuko yani marehemu aliishi vizuri sana mchepuko kuliko mke wake na kukawa na wosia basi mke halali wa ndoa atatolewa katika wale watakaorithi mali maana wosio utachukua nafasi kubwa kuliko matakwa ya sheria ya kumuangalia mke wa ndoa
 
Bahati nzuri sheria zetu za dini zinasema mtoto aliezaliwa nje ya ndoa halali (mwanaharamu) huyo ni mtoto wa mama yake na harithi chochote kwa baba.
Dini ipi ya kikristo au Kiislamu

Lakini pia kama dini inatambua hivyo ni Kwanini sasa mahakama inaenda kinyume ilihali mahakama inatambua sheria za mila, sheria za kidini nk
 
Wengine mnajibu ilimradi mmejibu lakini hamna knowledge kwenye mambo ya kisheria, tuwaachie wanasheria watolee ufafanuzi zaidi, kuliko kubishana
 
Nadhani Mahakama zetu zilitakiwa kuzingatia na misingi ya Dini zetu. Angekua mwislam hao watoto wangejijua toka mwanzo kua hawapaswi kurithi chochote. Pengine wanapewa kama zawadi . Na kama wale watoto wa ndani ya ndoa wanahuruma basi wanaweza kuwatengea nusu ya mali ya urithi. Sio kugawa sawa kwa sawa.
 
Acha porojo soma ibara ya 12 na 13 ya katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania.
 
Bahati nzuri sheria zetu za dini zinasema mtoto aliezaliwa nje ya ndoa halali (mwanaharamu) huyo ni mtoto wa mama yake na harithi chochote kwa baba.
hilo neno mwanaharamu halipo kwenye hadithi wala qurani,
 
Acha porojo soma ibara ya 12 na 13 ya katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania.
Umeshindwa kujibu kwanini Waislamu uwanyime haki ya ku-practice dini yao wakati katiba imewapa haki hiyo, hali kadhalika sheria ya mirathi inawapa hiyo haki. Na kwavile umeshindwa kujibu, better nikupuuze kwa sababu ibara ulizotaja hazijibu maswali niliyokuuliza!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…