Mirathi mtoto wa nje

Mirathi mtoto wa nje

popbwinyo

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
4,986
Reaction score
3,615
Wadau samahani na mniwie radhi kama ntakosea jambo.

Naomba wanaojua sheria na wenye uzoefu katika hili kwa kulipitia wanisaidie.

Hivi unaweza kumpa mirathi mtoto ambae ulizaa kabla haujaoa?

Namaanisha yule ambae mkeo alikukuta nae, sheria inasemaje juu ya hili.
 
mtoto wa nje ya ndoa anaweza kurithi tu pale kama alihalalishwa kimila ambapo mtoto (kwa kumlipia mahari mtoto katika jamii zinazofanya hivo, au kwa kumtambulisha katika ukoo wa baba kwa jamii zinazofanya ivo.. au kwa kumuoa mama yake) hizi ni aina mbali mbali za kumrecognize huyo mtoto ili apate kurithi mali.
i stand to be challenged or corrected if any.
 
Boss lakini kifungu cha 10 cha sheria ya mtoto ya mwaka 2009 kipo wazi kabisa, ,

'A person shall not deprive a child of reasonable enjoyment out of the estate of a parent'.

kwa tafsiri yake huwezi ukamnyima au kupokonya mtoto haki yake katika mali za mzazi wake..... mtoto wa nje na yeye si mtoto
 
Kitu cha kwanza kabisa ni lazima mahakama itathmini au ijue kama kuna ndoa inayotambulika kisheria, ingawaje hatakama haukufunga ndoa rasmi(formal marriage) kwa mujibu wa sheria ya ndoa ya mwaka 1971 aidha ya kiislam,kikristo au kimila lakini ulikutana na mwanamke mahakama yenye mamlaka inaweza kusema au kutoa tamko la ndoa ya dhana(presumption of marriage) ambayo kwa mujibu wa sheria ya ndoa chini ya kifungu cha 160(1) ila endapo tu kuwa umeishinae kwa mda usiopungua miaka miwili na jamii iwe inatambua kuwa uhusiano wenu ulikuwa ni kama wa mke na mume.Hivyo mtoto anaweza kuwa halali endapo mahakama imetoa tamko la ndoa hiyo ya dhana na endapo mwanandoa yoyote ameshindwa kukana(rebutt) ndoa hiyo,na mtoto anakuwa na haki zote kama mtoto aliezaliwa ndani ya ndoa rasmi ikiwamo haki ya mirathi kwa mujibu wa sheria za mirathi.
 
Rejea pia kifungu cha 160(2) cha sheria ya Ndoa iliofanyiwa marekebisho mwaka 2010
 
Back
Top Bottom