Mirathi ya Celebrities Bongo kizungumkuti

Umekomaa na mtoto wa afande sele utasema ni yeye tu aliyekaa kwenye mstari
Inawezekana hufahamu wengine ama una maslahi
 
Wasanii/ macelebs wengi wanafake maisha Kwenye mitandao bt in real life Mambo Ni tofauti kbsa.
 
Asilimia kubwa ya makazi dar es salaam hasa kino,sinza,mabibo,tbt ,manzese nk ni duni sana,kwa kuhalisia nyumba nyingi ni za urithi, wengi wameshindwa kuendeleza na wanasubiri kuziuza, je ndio lilikua lengo la mtoa urithi? Matatizo ni mengi, sio kila mtu atakua tajiri awe na vya kugawa,,nchi hii maskini sana elimu kwanza haya yakuacha legacy kama ya kina mengi, aboud,mo,bakhressa nk ni ya wachache sana, elimu sio degree tu,rithisha hata ujuzi kwa wanao
 
Celebrities anaabudu pombe na Mademu. Siku likimkuta Jambo anaaibika hadharani kabla na baada ya Maziko, watoto wanabaki kugawana makochi na harrier old model.

NB: Tengeneza future ya wategemezi wako ukiwa na nguvu.
Hicho siyo celebrities tu watu wengi bongo
 
Hayo maisha watayatafutia wapi pasipo kuwaandalia wewe mzazi?
Acha kukimbia majukumu yako wewe. Kama hutaki kuwaachia watoto wako urithi, basi usizae.
Ndo maana bongo kila mtu ni mwizi mwizi tuu. Akipewa dhamana yoyote ni kuiba tuu. Ni kwa sababu ya hii mindset ya kutafuta mali za wizi kurithisha watoto.

Ukweli ni kwamba kama wengi tungekuwa tunapata kipato kihalali, haya mawazo ya kurithisha mali tusingekuwa nayo. Maana tungekuwa tunapata kiasi kututosha na kuhudumia familia zetu.

Imagine, una viwanja..Mbande, Mapinga, Bunju, Tegeta, Ununio, Kimara, Kiluvya……nk. Ukitazama vizuri hizi plots zote ni za wizi. Na bahati mbaya sana…mali za namna hiyo…hata ukirithisha watoto…wanazipiga kiberiti asubuhi Mapema.

Ukiwa na mali za halali, kama unaweza wape Urithi watoto wako. Lakini kibongo bongo…unaiba urithi wa walipa kodi kurithisha watoto wako. Siyo Sawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…