sajo
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 3,474
- 6,195
Mahakama ya Rufaa ya Tanzania iliyo na vikao Dar es Salaam, kesho tarehe 11.07.2022 itatoa hukumu juu ya uhalali au ubatili wa wosia ulioachwa na marehemu Dk. Mengi. Hukumu hiyo katika rufaa ya madai namba 332/01/2021 iliyofunguliwa na mjane wa Dk. Mengi, Jackline Mengi itasomwa na majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa ambao ni Fikirini J.A, Mwambegele J.A na Makungu J.A.
Ikumbukwe, Mahakama kuu iliutupilia mbali wosia wa Dk. Mengi ambao ulimpa mali zote Jackline Mengi na watoto wake wawili, huku ukiwapa Tshs. 1,000/= tu watoto wengine wa marehemu. Mahakama kuu ilisema wosia huo ni batili kwa kuwa wakati wa kuandika wosia huo, Dk. Mengi alikuwa na ugonjwa wa akili.