Mirathi ya Kiislamu

Mirathi ya Kiislamu

AbuuMaryam

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2015
Posts
2,577
Reaction score
4,637
Nipo hapa kujibu masuala mbalimbali kuhusu miiraathi ya kiislaam.

Mambo ya kuzingatia kwenye miiraathi.
1. Undugu wa karibu(nasaba)
2. Ndoa

Niulize nitakujibu kwa uwezo na elim atakayonipa Allaah. Inshaa Allaah.

Kama kuna suala jingine la dini... Njoo kistaarabu kwa hoja nzito zenye akili... Sio kejeli. Ukibisha basi kaa na ubishi wako. Usiulize ili ubishe.

NA NDOA..

NA NIMEONA NIONGEZE NA NIJIBU NA MASUALA YA NDOA NA FAMILIA ZA KIISLAAM NA CHANGAMOTO ZAKE NA NAMNA UISLAAM UNAWAELEKEZA NAMNA YA KUISHI.

Allaah atuongoze.
Abuu Maryam
 
Mtoto wa Nje ya Ndoa anaruhusiwa kurithi na kusimamia mirathi?
 
Uislaam hakunaga kitu kinaitwa kusimamia miiraathi. Uislaam unaamrisha maiti atakapothibitika amekufa...

Iangaliwe mali yake yote, kutoka kwenye mali zake ITOLEWE KIASI CHA KUGHARAMIA MAITI YAKE MPAKA KUZIKA(Sanda na mpaka gharama za kaburi)...

Baada ya hapo tunaangalia MADENI YAKE TUNAMLIPIA...

Tukishatoa madeni... Tunaangalia wosia alioacha Maiti... Na mali inayotoka kwenye wosia haitakiwi kuzidi 1/3 ya MALI YOTE... Mfano maiti alitoa wosia kuwa akifa mali yake yote itolewe swadaqa msikitini... TUNAUPUUZIA WOSIA WAKE... TUNATOA TU 1/3 YA MALI YAKE NDIO TUNATOA SWADAQA ALIYOKUSUDIA...

BAADA YA HAPO MALI INAGAWIWA WA WAHUSIKA WA KURITHI KAMA WALIVYOTAJWA KATIKA QURAN...

KATIKA VIGEZO VYA KURITHI NA KURITHIANA KATIKA YA MIRATHI YA KIISLAAM NI NDOA... KAMA NDOA HAIKUWEPO BASI HATA WATOTO WAKE HAWAWEZI KUMRITHI BABA YAO... LABDA KWA MAMA YAO.
 
Mtoto wa Nje ya Ndoa anaruhusiwa kurithi na kusimamia mirathi?
Msimamizi wa mirathi anakuja pale ambapo MAITI AMEACHA WATOTO WADOGO YATIMA... Na umri wao bado wa kujitambua... Atateuliwa mtu ambaye ni muadilifu mchamungu na ikipendeza akiwa ndugu wa karibu na maiti ila sio lazima kuwalea hao watoto pamoja na kuichunga mali yao na kuiendeleza kwa kheri... Haifai kula hata kidogo katika mali yao... Mpaka wakue.
 
Urithi inatakiwa wapewe watoto wadogo, watu wazima kila mtu atafute mali zake...haiwezekani jitu zima una miaka40 Kisha upewe mali za bure alizotafuta baba yako, tafuta zako.
 
Nipo hapa kujibu masuala mbalimbali kuhusu miiraathi ya kiislaam.

Mambo ya kuzingatia kwenye miiraathi.
1. Undugu wa karibu(nasaba)
2. Ndoa

Niulize nitakujibu kwa uwezo na elim atakayonipa Allaah. Inshaa Allaah.

Kama kuna suala jingine la dini... Njoo kistaarabu kwa hoja nzito zenye akili... Sio kejeli. Ukibisha basi kaa na ubishi wako. Usiulize ili ubishe.

Allaah atuongoze.
Abuu Maryam
Vipi kama mwanaume wa kiislamu akizaa na binti wa dini nyingine, mfano mkristo na wale watoto wakapewa majina ya kiislamu.

Je Quran inasemaje juu ya umiliki wa watoto hawa kwa baba yao?, vipi kama baba atafariki, hawatakuwa na haki ya kurithi?

Sent from my SM-N916S using JamiiForums mobile app
 
Leo inabidi watu fulan wapate elimu, maana upande wao migogoro ya mirathi kila siku Yan
 
Basi subiri msaada wa tende na nyama ya ngamia.
Tuliwahi kukuomba wewe msaada? Tuliwahi kukuita kupokea wote msaada... Wewe tafuta hela sisi tunasubiri misaada... Full stop...

Fanya mambo yako. Sisi tunafanya yetu.
 
Vipi kama mwanaume wa kiislamu akizaa na binti wa dini nyingine, mfano mkristo na wale watoto wakapewa majina ya kiislamu.

Je Quran inasemaje juu ya umiliki wa watoto hawa kwa baba yao?, vipi kama baba atafariki, hawatakuwa na haki ya kurithi?

Sent from my SM-N916S using JamiiForums mobile app
Kwanza hapo hakuna ndoa, hata kama watapewa majina na watatumia jina la "baba" yao huyo. Watoto hao hawawezi kumrithi "baba yao huyo" na pia "huyo baba" hawezi kurithi mali za hao watoto. Ila kama "huyo baba" anataka hao watoto wapate mali yake, inabidi awape kama zawadi katika sehemu ya mali yake.
 
Urithi inatakiwa wapewe watoto wadogo, watu wazima kila mtu atafute mali zake...haiwezekani jitu zima una miaka40 Kisha upewe mali za bure alizotafuta baba yako, tafuta zako.
Babu yangu alifariki 2016 wakati marehemu baba yangu anamiaka 61 baba zangu wote wanne walipewa urithi wao kabla Babu hajafariki. Ilikuwa hivyo na itakuwa hivyo kwa yoyote anaetoka kwenye nyumba ya baba yangu.
 
Kwanza hapo hakuna ndoa, hata kama watapewa majina na watatumia jina la "baba" yao huyo. Watoto hao hawawezi kumrithi "baba yao huyo" na pia "huyo baba" hawezi kurithi mali za hao watoto. Ila kama "huyo baba" anataka hao watoto wapate mali yake, inabidi awape kama zawadi katika sehemu ya mali yake.
Na vipi kama uislam unatambua kuwa wale ni wanake katika imani?

Sent from my SM-N916S using JamiiForums mobile app
 
Tuliwahi kukuomba wewe msaada? Tuliwahi kukuita kupokea wote msaada... Wewe tafuta hela sisi tunasubiri misaada... Full stop...

Fanya mambo yako. Sisi tunafanya yetu.
Mnakera kulilia urithi.
 
Urithi inatakiwa wapewe watoto wadogo, watu wazima kila mtu atafute mali zake...haiwezekani jitu zima una miaka40 Kisha upewe mali za bure alizotafuta baba yako, tafuta zako.
Katika uislaam kigezo cha kurithi ni UNDUGU(NASABA) na NDOA...

Hakuna kigezo cha umri... HAKIPO.

HUO NDIO UISLAAM. HESHIMA TARATIBU ZAKO... Mawazo yako tunayaheshimu... Ila kwenye sheria yetu hayana nafasi
 
Vipi kama mwanaume wa kiislamu akizaa na binti wa dini nyingine, mfano mkristo na wale watoto wakapewa majina ya kiislamu.

Je Quran inasemaje juu ya umiliki wa watoto hawa kwa baba yao?, vipi kama baba atafariki, hawatakuwa na haki ya kurithi?

Sent from my SM-N916S using JamiiForums mobile app
Kigezo cha kurithi katika UISLAAM ni NDOA HALALI.

KAMA HAKUKUWA NA NDOA... HATA WATOTO HAWAWEZI KURITHI HATA KAMA WAKIWA NI WAISLAAM HAO WATOTO NA HUYO MWANAUME.
 
Leo inabidi watu fulan wapate elimu, maana upande wao migogoro ya mirathi kila siku Yan
Katika uislaam... Ingekuwa watu wanamcha Allaah haki ya kumcha... Na wakatekeleza sheria ya Mola wao... Basi migogoro ya mirathi na ndoa isingekuwepo.
 
Mnakera kulilia urithi.
Kwani tunakurithi wewe... Tunarithiana wenyewe kwa wenyewe... Wewe utarithiwa na na unayemtaka... Hakuna atakayekuja kulilia urithi wako zaidi ya wanao na ndugu zako... Sio sisi. Ishi maisha yako... Jali mambo yako.
 
Back
Top Bottom