nina ndugu yangu mtoto wa nje ya ndoa babake alipofariki aliitwa mahakamani kwa ajili ya kwenda kutambua msimamizi wa mirathi pamoja na mali za marehemu baada ya hapo mali zilipoanza kugawanywa alipewa sawa sawa na watoto wengine.
Sio kweli, mtoto wa nje ya ndoa hana haki ya kurithi mali ya baba yake labda awe amempa kabla ya kufa aweke wazi kuwa atapata kadhaaa wa kadhaaa. Na ikumbukwe hampi kama mrithi bali rafiki!!!! kwa vile yeye hayumo katika warithi wa mali ya baba yake. Nilishawahi kujadili suala hili humu na gazeti la Majira jumapili zilizopita huko nyuma imefafanua sana jambo hili. Angalia kesi ya Violet kahangwa v Eudokia kahangwa and administrator general (angalia kama nimesite correct respondents) Court of appelal 1996 something like that ilitoa msimamo wa kisheria ambao unasimama mpaka sasa
inategemeana na aina ya ugawaji mirathi (mirathi inayogawanywa kiislam, kimila au kiserikali). kwa waislam, huyo hatambuliki, vilevile kimila kama atakuwa hakukombolewa/tambulishwa kabla. vivyohivyo kiserikali kama hakukombolewa/tambulishwa etc. kwa ufafanuzi zaidi kupata vitabu kuhuru hili bofya SHERIA TANZANIANaomba kujua haki ya Mirathi kwa mtoto wa nje wakati mzazi anapofariki hasa baba mwenye taarifa nzuri tafadhari nazisubiri kwa hamu.Asanteni