Misafara ya viongozi wa kitaifa: Kwanini iwe na mwendokasi ule?

Misafara ya viongozi wa kitaifa: Kwanini iwe na mwendokasi ule?

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,307
Reaction score
25,932
Kuanzia pikipiki ya askari wa usalama barabarani hadi gari ya mwisho ya kwenye msafara, mwendokasi unaogofya. Mwendokasi wa msafara kama wa Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na wengineo huwa kati ya 120-180 km/saa.

Wakati wa msafara husika barabara husafishwa na kuwa nyeupe na isiyo na msongamano wowote. Halafu msafara huwa na mwendokasi nilioukisia. Kwanini mwendokasi huo?
 
Karibuni kwa mjadala wakuu. Nadhani kuna haja ya kutafakari upya juu ya suala hili.
 
Tujadili nini sasa? na umeshasema misafara yao huwa inakwenda spidi kali.

Umesahau, Ari zaidi, Nguvu zaidi, Kasi zaidi?

Dada FaizaFoxy huoni kuwa ni hatari kwa viongozi wetu?

Honestly, niliwaza juzi kuanzisha topic kama hii kushauri kuangaliwa upya hili. Lilinipita juzi hapa Morogoro mjini gari la waziri na speed iliyokuwa inaendeshwa ( ni eneo lenye msongamano wa watu na magari ambalo speed limit ni 50) ni hatari sana. Mpaka watu tuliokuwepo tuliishia tu kusema hii si njema na inaweza kutusababishia ajali kwa viongozi wetu

Ni kweli wanakuwa na ratiba ngumu na zilizobanana lakini uhai na afya zao ni muhimu sana kwa taifa letu na katika kutekeleza majukumu hayo

Kwa kweli tunawaombea afya njema na safari njema watekeleze majukumu yao, lakini tahadhari ni muhimu
 
Last edited by a moderator:
Sababu zinaweza kuwa moja katu ya hizi au zaidi...

..Kuwahi

...Wafanyakazi wanajua Ndo utaratibu (Kwani hata kama haendi sehemu inayomuhitaji kuwahi huwa spidi inakuwa kasi)

....Usalama (kuepuka zengwe la wananchi)

Nimejibu kwa kujitahi kutafakari.....
 
Mwendo kasi ni mwendo kasi, mjadala wa nini sasa? barabara zinaruhusu. Thubutu uende mwendo kasi kabla ya Kikwete kutandaza lami.

Huyu bibi ana mahaba yaliyopitiliza kwa Kikwete mpaka anajitoa ufahamu. Me nadhani sababu ni za kiusalama hasa issue ya snipers.
 
mtoa mada una uhakika gani kuwa spidi huwa kati ya 120-180
 
Tatizo kuna watu wanadhan wanajua kila kitu au wanataja kujua kila kitu. Mambo haya ni yakiusalama na wanaofanya ivyo ni wataalam wa mambo hayo. Wanajali usalama wa viongozi kuliko wewe na ndio kazi yao.
 
Spidi 120 bado misafara yao inatuchelewesha kwenye mishe zetu, wakitembea spidi 50 si uchumi utakufa kabisa?? we waache wakimbie tu...
 
fikiria msafara wa raisi au waziri mkiu au makamu wa raisi utembee taratibu sana, sisi walala hoi si tutakaa foleni masaa matano tukisubiri msafara upite? Wacha tu wakimbia hata km 200 kwa saa, maana inaonesha wana madereva wazuri, ni nadra kusikia msafara umetatizika kwa ajali. Pia kuna issiue ya kiusalma zaidi. Petro Mselewa kwa hili namuunga mkono dada angu faizaFoxy
 
unaona huruma vongozi kufa au speed hiyo inaweza sababisha madhara kwa raia wengine kama ni kuhusu haya mafisadi ondoa shaka yafe tu.
 
Kuanzia pikipiki ya askari wa usalama barabarani hadi gari ya mwisho ya kwenye msafara, mwendokasi unaogofya. Mwendokasi wa msafara kama wa Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na wengineo huwa kati ya 120-180 km/saa.

Wakati wa msafara husika barabara husafishwa na kuwa nyeupe na isiyo na msongamano wowote. Halafu msafara huwa na mwendokasi nilioukisia. Kwanini mwendokasi huo?

Speed kali ni security feature ya kuwalinda viongozi. Kama kuna mtu amejificha kwa mbali na ana high-powered rifle ili amuue kiongozi ni rahisi kumlenga kama gari linatembea taratibu kulilo kama linakwenda kwa mwendo wa kasi. Hizi kasi ulizotoa ngoja tuwe na perspective nyingine:

120 km/saa = 2,000 mita/dakika = 33 mita/sekunde
180 km/saa = 3,000 mita/dakika = 50 mita/sekunde

Kwa hiyo kama gari linalopita perpendicular na muuaji lina pita kwa kasi ya mita 30 hadi 50 kwa sekunde, hata kama huyo muuaji ana shabaha ya aina gani itakuwa vigumu kuipiga target yake.

NI KWA AJILI YA USALAMA WA KIONGOZI.
 
Wadunguaji haijalishi speed ya chombo, kama ikitumika technolojia ya kudungua ndege iyo speed si chochote,sasa misafara huenda kasi kwanza wanajua tu mbele hakuna kizuizi kunakuwa na sweepers tayari pili ni kuwahi ratiba tu,, issue ya security hapo ni ndogo sana kwa sababu ya technolojia.. Mfano linaweza tegwa bomu mahali kulenga chombo aina moja tu kikipita kingine bomu halitalipuka mpaka chombo hicho kifike linalipuka.
 
Speed kali ni security feature ya kuwalinda viongozi. Kama kuna mtu amejificha kwa mbali na ana high-powered rifle ili amuue kiongozi ni rahisi kumlenga kama gari linatembea taratibu kulilo kama linakwenda kwa mwendo wa kasi. Hizi kasi ulizotoa ngoja tuwe na perspective nyingine:

120 km/saa = 2,000 mita/dakika = 33 mita/sekunde
180 km/saa = 3,000 mita/dakika = 50 mita/sekunde

Kwa hiyo kama gari linalopita perpendicular na muuaji lina pita kwa kasi ya mita 30 hadi 50 kwa sekunde, hata kama huyo muuaji ana shabaha ya aina gani itakuwa vigumu kuipiga target yake.

NI KWA AJILI YA USALAMA WA KIONGOZI.

Snippers pia wana mahesabu yao mkuu so hata speed iweje anafanya calculation ya speed yako na mahali ulipo, so bullet inakufuata while you are moving na hii technology inatumika kuangusha ndege.
 
Back
Top Bottom