Misamiati mipya hii hapa

Mwita25

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2011
Posts
3,831
Reaction score
1,169
Nimekutana nayo kwenye kamusi ya BAVIZA nikaona si vibaya tuambizane:
1. Chegari: Sehemu inayotumika kunyoa nywele wanaume (barber shop)
2.Tabaharia:Kubobea katika uelewa au utaalam wa jambo fulani
3.Kicheche:Mwanamke anayefanya biashara ya mama ntilie.
4.Kinyunguriko:Mwanaume anayetoka nje ya ndoa yake.
5.Mkuchuku:Mwanamke anayependa kupigwapigwa na mumewe.
 
Kwenye Red pananifanya nihisi kuwa hiyo kamusi imesimamiwa na Chacha, Mwita
n.k
 
Kuna maneno hapo yakitumika tangia zamani na wala si msamiati mpya.

Tabaria ni hali ya kutokwa na jasho.
Kicheche ni mnyama mdogo wa Afrika alaye nyama. Ana milia myeupe na myeusi na anatoa maji yanukayo sana kutoka matezi yake.
Vilevile neno Kicheche linatumika sana haswa kwa mtu mwenye tabia ya kufanya uhuni, kama vile umalaya... mtu asiye jiheshimu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…