Hujambo? Vipi mzigo unasonga?1. Hila ya kikwapa, kunuka pasipo kidonda.
2. Elfu huanza na moja.
3. Achanikaye kwa mpini, hafi njaa.
4. Wakati wa hatari, mguu niponye.
5. Aendaye kwa mganga, hakosi jambo.
6. Bahiri hali mali.
7. Achekaye kilema, hata kwao kipo.Hu
8. Cheka uchafu, usicheke kilema.
9. Jawabu la kesho, huandikwa leo.
10. Haja huzaa hoja.
11. Sheria ni msumeno, hukata mbele na nyuma.
12. Pango ulimojistiri, usilidharau.
13. Fua chuma kingali moto,
14. Hakuna kiumbe asiye na akili.
Nakumbuka tulivyokuwa chuo kwenye somo la wayahudi kuna kipengele cha maswali ilikuwa mi methali alafu majibu unachagua nakumbuka nilikuwa napiga ana ana do yani watu walikula supp za maana