babacollins
JF-Expert Member
- Dec 23, 2010
- 901
- 212
Huwa najiuliza hii misamiati inayotumika katika uchambuzi hutumiwa na wachambuzi "kiufundi" na "kimbinu" au kama misemo ya msimu tu. Mfano neno "mikimbio" karibu kila mchambuzi alikua analitumia katika siku za hivi karibuni, kwa sasa wamepunguza sijui wachezaji hawana "mikimbio" tena. Kadhalika neno "huu ni mchezo wa kimkakati" kwa sasa limeachwa kutumika kama vile hakuna michezo hiyo ya " kimkakati". Neno mchezaji " kuku-offer" wachambuzi wengi kweli walikuwa wanalitumia kwa sasa sijui nini kimetokea kwa wachezaji "ku-offer". Yapo na mengine ambayo hayana ulazima wa kuyatumia lakini bado utasikia wachambuzi wengi wanayatumia kwa mfano neno "yes".
Mimi naamini ni kuiga au kuigilizia ndiko kunakoleta mambo kama haya.
Ni mimi mchezaji kiongozi.
Mimi naamini ni kuiga au kuigilizia ndiko kunakoleta mambo kama haya.
Ni mimi mchezaji kiongozi.