Misemo kama ya aina hii inafaa kufutwa

Misemo kama ya aina hii inafaa kufutwa

Mokaze

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2018
Posts
14,370
Reaction score
14,929
Ni mambo ya kushangaza kuona watu na akili na busara zetu bado tunashikilia misemo isiyokuwa na maana bali kupotosha jamii, eti utasikia ikisemwa; "Mpe mchawi alee mwanao" au utasikia; "Mnyonge mnyongeni lakini mpeni haki yake".

Mchawi ni mtu mbaya sasa iweje umpe mwanao amlee?!--- je akimfundisha uchawi au akimlisha nyama za watu utamlaumu nani??-- kama neno mchawi ni tamathali kwanini tamathali hiyo inathibishwa na kitu kibaya?

Pia utasikia Mnyonge mnyongeni lakini apewe haki yake, sasa mtu kisha nyongwa (kawa marehemu) ni kwa vipi atapewa haki yake?--- au atapenyezewa akiwa kaburini?

Misemo mingine ilitungwa na Wahenga waliotoka kunywa Pombe na katika zama hizi za haifai kuendelea kutumika kwani inafanya jamii iamini ujinga kuwa ni busara na hekima.
 
Kama sikosei kuna tasnifu ya uzamili (Masters) iliyoandikwa na mwanafunzi wa chuo kikuu cha Osaka au Leiden (sikumbuki vizuri) kuhusu Methali za Kiswahili na Mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia. Ukienda pale Mlimani unaweza kuibahatisha au ukigoogle pia waweza kuipata. Nitajaribu pia kuisaka na nikiipata nitaiweka hapa.

Misemo na methali ni sehemu ya lugha, na lugha ni sehemu ya jamii. Lugha ni kiumbe hai na huakisi maendeleo ya jamii husika katika uhalisia wake nayo hubadilika badilika kulingana na maendeleo hayo. Si jambo la ajabu basi kuona kuwa baadhi ya misemo, methali na nahau zikipigwa dafrau na maendeleo ya jamii husika na hulazimu ama kubadilishwa na jamii lugha au kuachwa kabisa. Ni jambo la kawaida katika lugha zote duniani.

Ni wazi methali kama pole pole ndiyo mwendo na haraka haraka haina baraka katika dunia ya sasa inabidi ziangaliwe kwa jicho jipya. Mambo ya aliye juu mngoje chini...mh! Kizazi cha sasa hakina muda wa kumngoja mtu mpaka ashuke mwenyewe bali kinamfuata huko huko na kumshusha kwa nguvu au kinampopoa mawe tu anashuka mwenyewe bila kupenda.

Na kabla ya kuzitolea kauli ya mwisho methali hizi, inabidi kwanza kuelewa vizuri muktadha na utamaduni zilimotumika na lengo kuu la kuanzishwa kwake. Ukiongea na wazee watakwambia hasa lengo la methali/misemo kama mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni lilikuwa ni nini na ukijua mazingira halisi ya matumizi yake ndiyo utaona busara kuu iliyojificha katika methali hiyo; na nyinginezo.

Lugha, katika ujumla wake, ni tata mno na imebeba historia, mila, falsafa na utamaduni wa watu japo tunaichukulia kijuu juu tu...
 
Una uhakika hujalewa?

Mie tena nimelewa na sio hao wahenga waliotunga misemo/ methali za ajabu??!!.

"Mchawi mpe mwanao amlee"-- hata kama haina maana ya moja kwa moja (literally) lakini msingi wake ni huu kwamba mtu mbaya ndiye anayetakiwa apewe dhamani juu ya kitu ambacho katika hali fulani angeweza kukitendea ubaya, mfano ukiwa na pesa na kuna wezi na unahofia kuibiwa basi chukua hiyo pesa umkabidhi mwizi mmoja akulindie.

Sasa wewe unaweza kufanya jambo hilo???!!, na kama utafuata huo msema na kumkabidhi huyo mwizi pesa basi wewe jamii yote itakuona sio tu ni mlevi bali hamnazo.

Misemo mingine ni ya kufutwa na kupuuzwa kwani inachafua lugha na kupotosha jamii badala ya kujenga.
 
... kajifunze maana ya fasihi hususan methali na tamathali za semi Mkuu.

Tamathali za semi ni lazima ziwe "conceivable".---- inatakiwa ziendane na hali halisi ya tungo mama.

Hivi kiuhalisia, wewe unaweza kumpa mchawi amlee mwanao??!, mchawi ni shetani iweje umkabidhi ili amlee??.

Hii inaweza kusababisha watu wengine nao walete tungo zao mfano; "Ukitaka kujua ubaya wa dhambi mfuate shetani". ---je tamathali kama hiyo inaingia akilini???.

Tafakari.
 
Ndo umedahiliwa BA.KISWAHILI nini unataka kujitia umemaliza kamusi yote?

Kwann mchawi?
Kwasababu kwa hofu ya kuwa wanamjua yeye mchawi,hawezi kumdhuru maana jamii inajua akipata matatizo tu basi yeye ndo muhusika.kwa kujua hilo mchawi hatomgusa huyo mtoto kwa ubaya kwa kuogopa vidole vya jamii.

Mnyonge mnyongeni,kwanini?
Hii ikiwa na maana,mfanye mfanyavyo ila panapo haki,mtu apewe haki yake.Kwa unyonge wa mtu unaweza kumfanya utakavyo ikiwa pamoja na kumyonga,lakin linapokuja swala la haki,usitumie unyonge wake kumnyima,hivyo mnyonge mnyongeni kwa udaifu wake ila kama ana haki,apewe haki yake.

Fasihi zina maana nyingi,kuna uwezekano wa kutolewa maana 10 katika sentensi moja na ndio maana ikaitwa fasihi..
 
Tamathali za semi ni lazima ziwe "conceivable".---- inatakiwa ziendane na hali halisi ya tungo mama.

Hivi kiuhalisia, wewe unaweza kumpa mchawi amlee mwanao??!, mchawi ni shetani iweje umkabidhi ili amlee??.

Hii inaweza kusababisha watu wengine nao walete tungo zao mfano; "Ukitaka kujua ubaya wa dhambi mfuate shetani". ---je tamathali kama hiyo inaingia akilini???.

Tafakari.
Hahahahahaa we jamaa bwana,yani na unajiona umeandika kitu maikini[emoji1787][emoji1787][emoji1787]...okey hata huo mfano uliotolea unamaana kifasihi.

Ni kweli huwezi kujua ubaya wa kutenda mabaya kwa kumfata mtu ambaye hatendi mabaya.kwa lugha nyepesi ukitaka kuujua ubaya wa wizi mfate mwizi,siku atakapokamatwa na kupigwa mawe ndipo utakapojua kuwa wizi una ubaya huu.

Shetani ametumika kama mtu ambae ni mtenda maovu,anaweza kuwa yeyote ie mwizi,malaya,nk.
 
"Mficha uchi hazai" hii methali imesababisha dada zetu kuvaa nguo za ajabu ajabu ilimradi wasiwe wagumba.
Mmeona tatizo lenu.Yan unaamini wadada wanavaa nguo za wazi ili kuonesha nyuchi zao ili wazae?ni upungufu wa akili kuamini hivi.
Jiulize kufucha uchi kwa namna gani?
Mbona wanaume wanaonesha nyuchi zao na hawazai?
Mbona malaya wanaoonesha nyuzi zao kwa watu wengi sio hao wenye watoto wengi mitaani?

Jibu ni moja,ukitaka matokeo unayoyahitaji,lazima vitendo viendane na uhitaji wa matokeo hayo.

Mwanamke atamaniye kupata mtoto,ni lazima uchi wake auoneshe(wasex) ili apate mtoto.

Unaumwa na unatamani kupona,lakin hutaki kudhihirisha ugonjwa wako kwa daktari,unategemea kupona vip?nro hapa tunasema mficha magonjwa kifo humuumbua,maana umeshindwa kuonesha ugonjwa ili upone
 
Kwann mchawi?
Kwasababu kwa hofu ya kuwa wanamjua yeye mchawi,hawezi kumdhuru maana jamii inajua akipata matatizo tu basi yeye ndo muhusika.kwa kujua hilo mchawi hatomgusa huyo mtoto kwa ubaya kwa kuogopa vidole vya jamii.

Sio lazima iwe hivyo, inawezekana ikawa ni kinyume chake, yaani inawezekana kwa kumpa huyo mtoto mchawi ikawa ndiyo easy access kwake kumdhuru (nimechukua literally).

Ninachotaka kusema ni kwamba; hiyo tamathali ni tata kitu kikishakuwa tata kitaleta utata ya nini kukuchukua???.

Misemo / methali lazima zijenge na kufundisha jamii hekima (philosophy) zisizokuwa tata na sio kupotosha, misemo/methali ni sehemu ya lugha, sasa iweje tushike lugha potofu.

Ponder in that broder line.
 
Hahahahahaa we jamaa bwana,yani na unajiona umeandika kitu maikini[emoji1787][emoji1787][emoji1787]...okey hata huo mfano uliotolea unamaana kifasihi.

Ni kweli huwezi kujua ubaya wa kutenda mabaya kwa kumfata mtu ambaye hatendi mabaya.kwa lugha nyepesi ukitaka kuujua ubaya wa wizi mfate mwizi,siku atakapokamatwa na kupigwa mawe ndipo utakapojua kuwa wizi una ubaya huu.

Shetani ametumika kama mtu ambae ni mtenda maovu,anaweza kuwa yeyote ie mwizi,malaya,nk.
... asante Mkuu kwa ufafanuzi murua! Pia ni muhimu kuelewa kwamba wakati mwingine fasihi hutumia lugha ya kinyume ili kutimiza lengo kusudiwa iwe ni kufunza, kuonya, kuadabisha, n.k. Ni sawa na mzazi anamkabidhi kijana wake ada ya shule huku akimwambia "chukua hii ada ukaile tena kama ulivyokula ile nyingine"; sasa hapa Ndugu Mokaze angetuambia mzazi amemruhusu mwanae akale ada! Hataki kushirikisha ubongo ajue maana ya mzazi ni kuonya na sio kuruhusu.
 
Mmeona tatizo lenu.Yan unaamini wadada wanavaa nguo za wazi ili kuonesha nyuchi zao ili wazae?ni upungufu wa akili kuamini hivi.
Jiulize kufucha uchi kwa namna gani?
Mbona wanaume wanaonesha nyuchi zao na hawazai?
Mbona malaya wanaoonesha nyuzi zao kwa watu wengi sio hao wenye watoto wengi mitaani?

Jibu ni moja,ukitaka matokeo unayoyahitaji,lazima vitendo viendane na uhitaji wa matokeo hayo.

Mwanamke atamaniye kupata mtoto,ni lazima uchi wake auoneshe(wasex) ili apate mtoto.

Unaumwa na unatamani kupona,lakin hutaki kudhihirisha ugonjwa wako kwa daktari,unategemea kupona vip?nro hapa tunasema mficha magonjwa kifo humuumbua,maana umeshindwa kuonesha ugonjwa ili upone
... tatizo wanachukua maana mzobemzobe jinsi inavyosomeka au kutamkwa bila kushirikisha ubongo! Tatizo la msingi liko hapo Mkuu.
 
Ni mambo ya kushangaza kuona watu na akili na busara zetu bado tunashikilia misemo isiyokuwa na maana bali kupotosha jamii, eti utasikia ikisemwa; "Mpe mchawi alee mwanao" au utasikia; "Mnyonge mnyongeni lakini mpeni haki yake".

Mchawi ni mtu mbaya sasa iweje umpe mwanao amlee?!--- je akimfundisha uchawi au akimlisha nyama za watu utamlaumu nani??-- kama neno mchawi ni tamathali kwanini tamathali hiyo inathibishwa na kitu kibaya?

Pia utasikia Mnyonge mnyongeni lakini apewe haki yake, sasa mtu kisha nyongwa (kawa marehemu) ni kwa vipi atapewa haki yake?--- au atapenyezewa akiwa kaburini?

Misemo mingine ilitungwa na Wahenga waliotoka kunywa Pombe na katika zama hizi za haifai kuendelea kutumika kwani inafanya jamii iamini ujinga kuwa ni busara na hekima.
Kabla hujaandika huu uzi ulitakiwa uwaulize Waswahili wanaitumiaje misemo hii. Uzi wako uneonyesha ni kwa namna gani hukijui unacho kiandika na hili ni tatizo kubwa. Mathalani msemo wa kwanza ulio unukuu, huwezi ukamkuta Mswahili anautumia bila kuzingatia muktadha wa hali,, muktadha wa hali ambao akiutumia msemo huo unaleta maana ya wazi kabisa, huo msemo wa pili, ndio daaah, uko wazi na kuwatahadharisha watu juu ya kutenda haki hata kwa mtu mnyonge wa namna gani,bali mpaka kwa mtu unaye mchukia.

Kwa ushauri wangu ni bora ututake radhi sisi Waswahili kisha uufute huu uzi.

Ahsante.
 
"Mambo ya kumpa mwanangu mchawi amlee"??!!🤣

Kama ukubwa ndio akili za aina hiyo basi naomba nisikue.
Kuna mtu nimeona kajaribu kukudadavulia.Kama na hapo hujaelewa basi acha kufuatilia methali kabisa.
 
Back
Top Bottom