Uzi mfupi**
Wachawi wanapatia changamoto nying wanapotaka kukuroga, kwanza inabidi atafute pesa ya kununulia Vifaa Vya kazi
Kununua Vifaa Vya kazi ni gharama kubwa na Muda mwingine itamlazimu kusafiri ata nje ya Mkoa ili akanunua kifaa icho cha kukurogea
Kwa mfano Kuna uchawi mwingine ili ufanyike mchawi ataitaji maji ya maiti
upatikanaji wa maji ya maiti ni mgumu sana,
Yani inabidi uwe na koneksheni ya kufa mtu ili upate maji ya maiti na maana muda mwingine unaweza uziwa maji feki
Kwaiyo katika hali kama iyo mchawi inabidi atoe pesa ndefu ili kufanikiwa
Mchawi ni mtu mbishi sana yana hakubali kushindwa kabisa
Kitu ambacho kinamuumiza sana mchawi ni pale anapotumia nguvu nying kukuroga alafu ww unaleta dharau
Yani yeye anapokuroga anataka kuona matokeo yani anataka kukuona umepaniki
Mchawi Anaskia raha sana pale anapoona kwamba umepaniki alafu umekimbilia kwa mganga
Changamoto kubwa kwa mchawi ni kuona kwamba badala ya kupaniki lakini ww ukamua kufanya ibada yan ukasimama na MUNGU
Mda mwingine mchawi inabidi akijifunze teknolojia ambayo itamsaidia kukuroga
Hapa inabid aende kozi iyo maalumu na inabidi alipie pesa kwa ajili ya kupata utaalamu
Upatikanaji wa Vifaa Vya kurogea imekuwa changamoto kubwa kwa Wachawi
Maana katika maduka ya kawaida ya asili havipatikani
Madalali wanaouza Vifaa Vya kurogea wamekuwa wakiwauzia wachaw Vifaa ivyo kwa bei juu sana
Kwa mfano mchawi ili aingie kwako lazima awe na testa ili aone kama kuna mtego au hamna
Testa ya kichawi inauzwa bei juu sana maana bila ya testa unaweza jikuta unaingia mtegoni
Kama ulishawai ona mchawi Kanasa juu ya bati au ameanguka basi jua uyo ameingia bila testa
Wachawi wanatumia pesa nyingi sana kununua Vifaa Vya kurogea pande za mahospitali na makaburini
Mara nyingine mchawi anajikuta anamadeni mengi sababu anataka afanikiwe kukuroga
Akishakuroga itambidi afatilie mara kwa mara maendeleo yako ili aone kama uchawi unafanya kazi
Muda mwingine inabidi afanye update yani kama vile Ana update windows
Asanteni
View attachment 1495584