Misemo na majibu ya makondakta

Misemo na majibu ya makondakta

Huwa nacheka sana misemo na majibu ya makondakta:

- Shemeji twende ya kuwahi kaka kesha rudi.
- Konda kuna siti? "Siti zipo ila wenzio wamekalia"
- Mama mkwe kamata bomba
- Oyaaa, wakusoma tulieni sio skuli basi hii
- Hapo nyuma fungua nauli
- Konda una mia nikupe mia tano? "Sina we unayo"

*Tupia mengine...
*Dada cheupe fungua zipu ya pochi yako-checheche (angongagonga coins)
 
1. Dereve kanyaga twende
2. dereva kuna mchawi nyuma mpukuchulie
 
KWELI WENYE MAGARI BINAFSI WANAKOSA UHONDO NA MAJIBU UA MAKONDA!
utasikia!
MABISHOO: dah! humu ndani joto!
konda; kapandeni friji!
mlokole; dereva toa taarab weka nyimbo za yesu!
konda; yesu bado hajatoa albamu!
sista duu; konda kuna siti humo?
konda; kwani wenzio wamekalia madumu! 🙂
 
Ukimkuta dereva anapiga reverse huku konda anamuelekeza..

Utasikia..
LETE NYUMA HUKU UNAKATA

Ukimkuta dereva anapiga reverse huku teja anamuelekeza..

Utasikia..
NJOO, NJOO, MPAKA USIKIE PUUUH...
Konda: Naomba nauli yangu
Abiria: Ikisimama nitakupa, au nilivyokaa hivi nitakupaje?!!! Hahahahaha!!!!
 
ha ha haaaaa!, naomba niendelee kucheka kwanza. Maana nimemisi kauli za makondakta, kitambo sana sijapanda, hii mikoa mingine tunayokuja yaani shida tupu; hakuna daladala aisee!. leteni kauli niendelee kucheka
 
Nimecheka sana kuna vituo utasikia banana,magereza,tazara,buguruni ......kariakoo....akifika makaburini utasikia kondakta kwa nguvu ....MWISHO WA MARINGO...SHUSHA
 
Back
Top Bottom