Misemo ya kiswahili inayo viza maendeleo

Misemo ya kiswahili inayo viza maendeleo

MVUMBUZI

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2011
Posts
5,182
Reaction score
2,308
Hali ya umaskini tuliyo nayo imechangiwa kwa kiasi fulani na utamaduni wetu wa kiswahili haswa kutokana na kuwepo kwa misemo mingi inayochochea uzembe kuliko kujibidisha. Baadhi ya misemo ya Kiswahili zikiwepo methali zina maudhui hasi ambayo yamewafanya watu wengi kuridhika au ku maintain status quo kuliko kutafuta upenyo wa tatizo alilo nalo. Kwa mfano; Mithali zifuatazo:

1."Kulenga siyo kufuma"
2."Mipango siyo Matumizi"
3."Kutangulia siyo kufika"
4."Mpanda ngazi hushuka"
5."Polepole ndio mwendo"
6."Harakaharaka haina baraka"[/B]

Misemo 1na 2 ina mkatisha tamaa mtu kupanga au kujiwekea malengo kwa sababu utekelezaji wake siyo lazima uwe kama ulivyopanga au sawasaw na shabaha yako. Kwa maaana nyingine kupanga na kutopanga haina tofauti.
Hiii misemo kwa ufupi ina viza fikra za watu kuwa eti hutakiwi uwe na haraka wala kutangulia na kwamba eti kwenda taratibu basi ndiyo mwendo muafaka.

Wenzetu wa magharibi wangezaliwa katika mazingira ya utamaduni kama huu wasingegundua magari wala ndege kwani polepole ndio mwendo na haraka haraka haina baraka. Pia wasingekuwa na utaratibu wa kuweka mipango na malengo ya baadaye kwani kulenga siyo kufuma na mipango siyo matumizi.

Kwa mtazamo wangu misemo hii ya waswahili imewafanya wenye utamaduni huu kuridhika na kile anachopata bila kujishughulisha sana na ukimwuuliza kwa nini hutaki kujishughulisha anaanza kukukebehi na vimafumbo, mithali na nahau za kiswahili" Mtakuja, mtaondoka na mtatuacha hivihivi!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom