Misemo ya zamani mitamu sana

green rajab

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2015
Posts
12,387
Reaction score
39,119
Nakumbuka miaka ya 80s - 90s wakati nakua nlikuta maneno ya zamani baadhi ni kama kuita Polisi, Mamwela au Manjagu na Mapongo sasa hv tunawaita Tigo au....Wanawake zamani tuliwaita Ngaya.

Kufanya mapenzi zamani tuliita kufanya matusi kusuuza...Mshamba zamani tulimuita Ngoima, Goloko, Ndezi, Pimbi, sa hivi wanaitwa Makolo au kinega

Kula vinono tuliita kujichana..bishoo tulimwita mtanashati...tu anayekumbuka ladha za enzi hizo atupatie tu enzi wakati ule
 
Miaka ya 1980 kushuka chini Malaya wanaojiuza tulikua tunawaita wazalendo
 
Yanga iliitwa YEBOYEBO kwa maneno ya kisasa inaitwa Utopolo.kwa sauti ya msemaji wao tikitimaji
 
Sikuhizi Inaitwa NGONGINGO au MZIGO, miaka ile ndugu zetu waliita JOYCE WOWOWO! au mshindo nyuma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…