Mishahara marais wa Afrika: Huu wa ugonjwa wa akili!

Kama wewe hujawahi kufanya kazi serikalini tafadhali usijidhalilishe kwenye mitandao, kanuni za utumishi ni kwamba mshahara ni siri kati ya mwajiri na mwajiriwa, kama ilivyo daktari na mgonjwa, hairuhusiwi mwajiri kutaja mshahara mwa mwajiriwa bila ruhusa yake, au daktari haruhusiwi kutaja ugonjwa wa mgonjwa bila ridhaa yake, ila kama mwajiri ataamua kutaja kwa ridhaa yake, lakini halazimiki kuutaja wala kushinikizwa kufanya hiivyo

Kazi za watumishi wa serikali kwanza ndio huwa rahisi sana kujua mishahara yao maana hulipwa kulingana scales ambazo zinakua gazetted, sijui kwanini huwa unatumia nguvu nyingi hivi kuhadaa wadau humu, hata kama unalipwa.
 
Kama kweli rais Magufuli analipwa 400,000 Kshs hapo binafsi amenikosha na anadhihirisha mzalendo wa kweli. Lakini naona Wabongo wanambishia kwenye mitandao, wengi wanasema aanike payslip yake, maana wanasiasa wanafahamika kwa matamko yasioendana na uhalisia.
Hata hyo naona nyingi.mzalendo unachukua mshahara mil 9?

Apunguze afanye hata laki 2.au aache kabisa huo ndo uzalendo.
 
Kama wewe hujawahi kufanya kazi serikalini tafadhali usijidhalilishe kwenye mitandao, kanuni za utumishi ni kwamba mshahara ni siri kati ya mwajiri na mwajiriwa, kama ilivyo daktari na mgonjwa, hairuhusiwi mwajiri kutaja mshahara mwa mwajiriwa bila ruhusa yake, au daktari haruhusiwi kutaja ugonjwa wa mgonjwa bila ridhaa yake, ila kama mwajiri ataamua kutaja kwa ridhaa yake, lakini halazimiki kuutaja wala kushinikizwa kufanya hiivyo
Wewe ndio upo mtupu kabisa..
Jibu hoja usiwe kama Taahira..
Mshahara ni siri kati ya mwajiri na mwajiriwa ni statement tu ambayo haina ulinzi wowote kisheria..
Tuambie basi Magufuli alivyotangaza mshahara wake hivi karibuni amevunja hiyo sheria..!?
 
Kipindi Magufuli anaiingia madarakani kuna wakurugenzi wa mashirika ya umma walikua wanavuta mpaka over Tsh 30 m per month, ni kweli sheria zili waruhusu ila kwa upande wa serikali hali ni tofauti. Kwa kuliona hilo Magufuli alishusha na kuweka kima cha juu cha 15m!! Kama hutaki acha kazi. Sasa hvi hamna mtu anaekula zaidi ya 15m iwe serikalini au kwenye mashirika ya umma. Kwa hoja hiyo tu unaeza ukapata picha kama huo mshahara wa 9m ni waukweli au ni uongo.
hapo safi sana kwa kweli maana kama unaona kulipwa 15m ni ndogo basi unaacha kazi...hii imekaa poa sana lazima kuwe na misimamo kama hii ili mambo ya kwende...
 
Wewe ndio upo mtupu kabisa..
Jibu hoja usiwe kama Taahira..
Mshahara ni siri kati ya mwajiri na mwajiriwa ni statement tu ambayo haina ulinzi wowote kisheria..
Tuambie basi Magufuli alivyotangaza mshahara wake hivi karibuni amevunja hiyo sheria..!?
Nimekuambia ni kanuni na masharti ya utumishi wa umma sijasema ni sheria, pili nimesema mtumishi mwenyewe anaweza kutaja kwa ridhaa yake kama alivyofanya Magufuli ila halazimishwi, uwe unaelewa na usome vizuri pimbi wewe
 
Kazi za watumishi wa serikali kwanza ndio huwa rahisi sana kujua mishahara yao maana hulipwa kulingana scales ambazo zinakua gazetted, sijui kwanini huwa unatumia nguvu nyingi hivi kuhadaa wadau humu, hata kama unalipwa.
Kama ambavyo ni rahisi kwa watumishi kula rushwa, hiyo haina maana imehalalishwa, au ni haki yao kufanya hivyo
 
Kama Raisi Magufuli anakataa Mialiko nje ya ili kuokoa fedha kwa nini adanganye mshahara wake? UN deligation yetu imekaa cheapest hotel na Raisi wetu hakwenda haya yote ni kuokoa fedha ambazo tunazihitaji hapa nyumbani!

Isitoshe Sheria ya Tanzania hairuhusu Raisi kuanika Mshahara wake hivyo kama ameweza kutekeleza yote kwa nini adanganye hili la Mshahara?
Raisi wa JMTZ kwanza hahitaji Mshahara mkubwa kwa maana anapata kila kitu na hata baada ya Uraisi mpaka nyumba anajengewa na kuhudumiwa na Serikali mpaka siku yake ya mwisho, sasa kwa nini adai Mshahara mkubwa?

Kitu ambacho sielewi ni kwa Raisi Uhuru Kenya, huyu jamaa ni Bilionea huo Mshahara wala sidhani hata kama anautumia, kwa nini hata hautoi sadaka tu kwa Hospitali au sehemu yoyote yenye mahitaji?

Eti Cheapest Hotel, unajua walifikia hotel gani? na ni bei gani?
Wacha porojo za vijiweni.
 
Binadamu huwezi kumridhisha hata ufanye nini, kwani mishaara ya marais wengine wote wanakubali na hawaombi kuona pay slip lakini kwa Magufuli wanaomba kuona?, kwanza walisema wanataka rais atangaze mshaara wake hadharini, kinyume kabisa na sheria ya utumishi wa ume ambayo inasema mshaara ni siri kati ya muajiri na muajiriwa, lakini alikubali na ametaja mshaara wake, bado wanataka salary slip, kwani kama lengo ni kudanganya hawezi kutoa fake salary slip?, hawana hoja.
Wanataka payslip kutoka kwa Raisi wao sio raisi wa wengine, wakikumbuka sukari kushuka kutoka 5000 mpaka 3000 ndo wanapoona kuna shida mahali fulani, lakini hiyo 9mln inalipiwa kodi kiasi gani? Au nini maana ya uzalendo????
Bunduki za nini, tubishane kwa hoja
 
Hivi unawezaje kusema unapokea milioni sita halafu tunajua kabisa unamabilioni ya hela isiyofanyiwa Auditing kwenye mfuko wa Rais
 
Eti Cheapest Hotel, unajua walifikia hotel gani? na ni bei gani?
Wacha porojo za vijiweni.
Walifikia Double Tree Hotel kwa mujibu wa mtangazaji wa TV ya Marekani iliyofanya upelelezi huo, hii Hotel inagharimu $250 -350 per day, na ujumbe wa Tanzania ulikuwa na watu wanne (4) tu
 
Hivi unawezaje kusema unapokea milioni sita halafu tunajua kabisa unamabilioni ya hela isiyofanyiwa Auditing kwenye mfuko wa Rais
Mbona unaunganisha hoja tofauti?, watu walitaka kujua mshahara wake, walimtaka ataje hadharani ili wananchi wajue anachopata, ndicho alichokifanya, asingetangaza mngesema anaficha, ametangaza mnaleta mengine. Hilo la kwanza ameshatimiza, kama kuna lingine liwekwe mezani ili lifanyiwe kazi, wacha kuchanganya files.
 
Binafsi, hata rais akipokea 100M kwa mwezi sio mbaya.. Kazi ni ngumu mnoo, ila akubali kuwe na uwazi katika utendaji wake, raia waruhusiwe kuhoji.. Huwezi kujisifia kupata 9M wakati unafanya manunuzi ya mabilioni yasiyofuata taratibu.
 
Huo ni utumbo mshahara haujashuka huo huo ndio waliopata walitangulia kwasababu kwake huo hauna kazi yoyote ni kama hata angekataaa kabisa
 
Nani aliyesema mshahara ulishuka?, mbona inaonekana ina hasira na umepanic?, hajasema mshahara umeshuka, wala hajataja waliomtangulia walikua wanalipwa kiasi gani, yeye amesema kila anacholipwa tu, hayo mengine unayofikiria ni kichwa chako ndiyo kinakutuma ufikirie hivyo, yeye ametaja kile anacholipwa, hajasema ameshusha mshahara wake. Usiwe na chuki kupitiliza, utapata abdominal ulcers bila sababu.. relax kidogo.
 
Kwani kajisifia au kataja anachopata kama alivyoombwa na baadhi yetu?, kwani kulipwa 9M kwa mtu kama rais, chini ya mshahara wa rais wa Rwanda na Burundi unaita ni kujisifia?, huko ni kujidhalilisha kwa maoni yangu
 
Kwanini tudanganywe analipwa kidogo wakati tunajua Pesa ya posho yake ni milioni 800 kwa mwaka
 
Nani kasema hiyo 9M ni kidogo?, wewe kichwa chako ndiyo kinachanganua na kuja na majibu yako na unataka utuaminishe, wewe unachokijua endelea kuamini hivyo hivyo, yeye ameombwa ataje na ametaja kile anachopokea yeye, kama wewe unajua tofauti, nenda kaitishe press conference na wewe utaje hizo 800M unazojua wewe...Relax brother, ugumu wa maisha usiuendekeze sana, utakusababishia uwe na hasira kila siku hadi watoto wako watakukimbia
Nani aliyesema mshahara ulishuka?, mbona inaonekana ina hasira na umepanic?, hajasema mshahara umeshuka, wala hajataja waliomtangulia walikua wanalipwa kiasi gani, yeye amesema kila anacholipwa tu, hayo mengine unayofikiria ni kichwa chako ndiyo kinakutuma ufikirie hivyo, yeye ametaja kile anacholipwa, hajasema ameshusha mshahara wake. Usiwe na chuki kupitiliza, utapata abdominal ulcers bila sababu.. relax kidogo.
 
Kwa akili yako milioni 9 ni hela hiyo ambayo Meneja tu wa tawi la Bank anapewa au kwakuwa unapunjwa mwalimu unaiona myingi

Mbona unaunganisha hoja tofauti?, watu walitaka kujua mshahara wake, walimtaka ataje hadharani ili wananchi wajue anachopata, ndicho alichokifanya, asingetangaza mngesema anaficha, ametangaza mnaleta mengine. Hilo la kwanza ameshatimiza, kama kuna lingine liwekwe mezani ili lifanyiwe kazi, wacha kuchanganya files.
Huo ni utumbo mshahara haujashuka huo huo ndio waliopata walitangulia kwasababu kwake huo hauna kazi yoyote ni kama hata angekataaa kabisa
Nani kasema hiyo 9M ni kidogo?, wewe kichwa chako ndiyo kinachanganua na kuja na majibu yako na unataka utuaminishe, wewe unachokijua endelea kuamini hivyo hivyo, yeye ameombwa ataje na ametaja kile anachopokea yeye, kama wewe unajua tofauti, nenda kaitishe press conference na wewe utaje hizo 800M unazojua wewe...Relax brother, ugumu wa maisha usiuendekeze sana, utakusababishia uwe na hasira kila siku hadi watoto wako watakukimbia
 
Mwalimu alipata kusema ....hata sigara alizokua akitumia zilikua ni pesa za serikali....sasa hiyo 9 million ni nyingi sana coz haina kazi ni hela inaingia tu cjui hata kama ina mchanganuo......kila kitu bure bure mpka unakufa na bado unalipwa?......hivi kazi yake haswa huwa ni nini? Nani anampangia majukumu...nani anamkagua...taarifa anamuandikia taarifa.....nani ana...na n.k.nk.......tusidanganyane
 
Kwa akili yako milioni 9 ni hela hiyo ambayo Meneja tu wa tawi la Bank anapewa au kwakuwa unapunjwa mwalimu unaiona myingi

Huo ni utumbo mshahara haujashuka huo huo ndio waliopata walitangulia kwasababu kwake huo hauna kazi yoyote ni kama hata angekataaa kabisa
Sasa ulipaswa ulete mada ya hilo la mshahara kwamba ni mdogo au vipi ili tuchangie, sasa wewe umeshaamua kuwa ni mdogo, wakati huyo mjumbe hapo juu anaona huo kwa rais ni mkubwa sana, ninarudia tena hili jukwaa lengo lake ni ili watu wachangie, sio wewe kile unachokifikiria ndiyo unataka kila mtu afikirie kama wewe, na aanzie kuchangia pale unapofikiria wewe ndiyo hivyo, nani aliyekuambia kwamba ni lazima rais apokee mshahara mkubwa kuliko mfanyakazi wa benki?, kwa taarifa yako, hata Gavana wa Benk kuu anapokea pesa nyingi kuliko rais, kwa sababu yeye kazi yake ni professional, Kimei wa CRDB na wengine wengi tu wanamzidi, toa utando kwenye ubongo wako wa kufikiria rais ni lazimwa apokee mshahara mkubwa kuliko watu wote nchini, una mawazo ya kizamani sana
 
Back
Top Bottom