Chapakazi
JF-Expert Member
- Apr 19, 2009
- 2,874
- 316
Mchukia Fisadi,
Nilipoanzisha mjadala wa hoja ya mishahara na marupurupu makubwa ya Wabunge, nilikuwa nikilenga hoja ya kuwa kunajengeka Gap kubwa sana kati ya watu mbalimbali katika Taifa letu. Kwa bahati mbaya wengi hawakuelewa hoja yangu wakati ule. Kimsingi hoja ile ililenga kuwa na mjadala wa kitaifa, na kufikia mahali tufunge hii gap kwa namna ambayo tutakubaliana, keki ndogo ya Taifa igawanywe kwa uwiano wenye mantiki, lakini pia wale wa chini waweze kunyanyuliwa ili nao waweze kuishi maisha yenye hadhi ya ki-utu na kibinadamu. Huu ndio mjadala unaotakiwa kuendelea. Nimetamka hadharani, hakuna soko la Wabunge au viongozi wa juu wa Serikali. Wote tunapata mahitaji yetu muhimu ya kibinadamu kwenye soko hilo hilo. Hivyo hakuna justification ya kundi fulani kuwa na mshahara au marupurupu makubwa ya kupindukia.Tunaachiana kwa majukumu kweli, lakini sote tunahitajiana. Tunaishi katika mfumo wa "chain". Pingili mmoja likidondoka, hakuna chain. Hivyo hata mhudumu mwenye jukumu la kufagia ofisini ni muhimu, akikosekana si Gavana, wala Kamishna Mkuu wa TRA au Spika anayeweza kufanya kazi kwa ufanisi. Kama tunahitajiana, ni lazima kuwe na uwiano fulani, unaojali nafasi, hadhi, lakini pia unajali ubinadamu wa wale wa chini sana. Vipi tutapata uwiano huu, ndio msingi wa mjadala wa kitaifa!
Mh, wengi tupo nyuma yako, na tungependa uendeleze huu mjadala kwa hali na mali kwa kusudi la kufikia wananchi wote. Lakini tatizo nionalo mimi sio kuwa na gap kubwa, bali ni matumizi mabovu ya pesa za umma. Pesa yetu itumike katika kutuwezesha, na sio kuhakikisha ugawaji wa mishahara kwa umakini zaidi. Kodi ni mali ya umma na sio ya serikali. Na katika Katiba, tuna wajibu wa kupigania na kulinda mali yetu kutoka ubadhilifu.
Ivi kweli mbunge anahitaji mil. 7 kwa mwezi?
Kamishna wa TRA je? - mil 18
Gavana - mil 16?
Mshahara wa mwalimu - je ni kiasi gani?
Tusipoangalia, tutatengeneza matabaka ya watawala na watawaliwa. Hivyo ningependa/tungependa kuona pesa yetu ikitumika kwa umakini zaidi, hasa kwa kutuletea maisha bora, sio kuishia mikononi mwa viongozi wetu.