kindili kindili
JF-Expert Member
- May 27, 2013
- 242
- 54
Naandika kwa niaba ya rafiki:
Ninafanya kazi kwenye moja ya international schools Dar es Salaam. Agizo la waziri mkuu kwamba shule zifunge lilipotoka tulianza likizo na mwezi wa tatu tulilipwa, tulikua tukifundisha kutokea nyumbani.
Sasa week iliopita mwajiri aliandika ujumbe kwa baadhi ya wafanyakazi, Watanzania tu (Wageni hawajaguswa) kuwa shule inajiendesha kwenye mazingira magumu na hasara, kwamba wanafunzi waliotakiwa kulipa ada hawajalipa na gharama za uendeshaji ni kubwa hivyo anatuomba tuchukue likizo bila malipo hadi hapo serikali itakapotanganza kufunguliwa kwa shule tena.
Na kwamba tutarejea kwenye nafasi zetu na tutaendelea na mikataba yetu. Tukajaribu kuhoji kwamba ni uamuzi wa ghafla sana na sijajiandaa, Mwajiri akasema au kuchukua option ya kukaa pending au kuacha kazi kabisa. Na jana ametuma mkataba wa kukubaliana kuchukua likizo isiyo na malipo(hatujakubaliana ni maamuzi tu tuliletewa tuyajue).
Naomba ushauri wa kisheria, makataba wangu unatakiwa kuisha mwakani mwezi wa tisa.