Mishahara Sekta Binafsi Corona (covid 19): Mwajiri analazimisha likizo bila malipo

Mishahara Sekta Binafsi Corona (covid 19): Mwajiri analazimisha likizo bila malipo

No production, no income.. Ni vyema serikali ikazipatia bailouts shule za binafsi kwa kuzikopesha kiasi cha pesa kitakachotosha kuwalipa wafanyakazi wake kiasi cha mshahara kisichozidi 75% ya mishahara yao na shule hizo kupewa miezi 60 ya kurejesha fedha hizo za Bailout.
 
Mkuu hukusikia mdau huku aliilakamiki CWT iwawekee kifua posho zinakaribia kufungiwa kipindi hichi cha mpito
 
Hii ishu imeikumba mataifa mengi hata kule kwenye upande wa soka La Liga kuna kesi kama hizi,ila uzuri mikataba ya kazi mwisho wa siku ndio inaamua kila kitu mikataba ya kazi bongo ni ya kimagumashi tupu 90% haina vipengere kama hivi vinavyozungumzia majanga kama COVID 19 n.k

Ila ulaya mikataba ya kazi inagusa kila kona na ina favour pande zote mbili ndio maana liliibuka swala la wachezaji kukatwa mishahara likapingwa kisheria mpk leo kina Messi wanavuta mshahara wao km kawa licha ya COVID 19.

Mimi sijasomea sheria,mhandisi by professional na dalali by passion ila naamini kuna vipengere vya sheria vinavyozungumzia utaratibu wa kutoa likizo kwa mwajiriwa bila malipo kutokana na biashara kutoingiza faida au kufilisika pia anaweza hata kupunguza wafanyakazi inapobidi ila afuate taratibu za kisheria zote akibugi tu inaweza kula kwake kisheria.

Likizo bila malipo ni taratibu wa kisheria naamini hivyo ila ni vizuri mkazungumza kama mtashindwana hapo ndio linakuja swala la vyama vya wafanyakazi,vizuri ukawashirikisha chama chako cha wafanyakazi hao ndio watetezi wako pekee.

Mwisho ni malizie kusema kubali likizo bila malipo harakati hazina ishu kuwa mpole hali ni ngumu kwa sasa kutokana na hili janga ambalo hakuna anayeju linaisha lini.
 
Ugumu ninaouona mwingine ni pale wazazi/walezi watakapoambiwa walipe ada ya term inayofuata...huku wakilalamika term iliyopita wanafunzi hawakuwa mashuleni/vyuoni.
 
Naandika kwa niaba ya rafiki:

Ninafanya kazi kwenye moja ya international schools Dar es Salaam. Agizo la waziri mkuu kwamba shule zifunge lilipotoka tulianza likizo na mwezi wa tatu tulilipwa, tulikua tukifundisha kutokea nyumbani.

Sasa week iliopita mwajiri aliandika ujumbe kwa baadhi ya wafanyakazi, Watanzania tu (Wageni hawajaguswa) kuwa shule inajiendesha kwenye mazingira magumu na hasara, kwamba wanafunzi waliotakiwa kulipa ada hawajalipa na gharama za uendeshaji ni kubwa hivyo anatuomba tuchukue likizo bila malipo hadi hapo serikali itakapotanganza kufunguliwa kwa shule tena...
Kwa akili za kawaida tu mkuu
Kama ni wewe ungekuwa unaendesha hiyo shule husingekuwa na uwezo wa kulipa mishahara kama wazazi hawalipi ada
 
Nakushauri kubali kuchkua likizo bila malipo, sheria zetu za kazi especially za Zanzibar ambazo mimi nazijua, katika hili zinambeba muajiri.
 
Hii ishu imeikumba mataifa mengi hata kule kwenye upande wa soka La Liga kuna kesi kama hizi,ila uzuri mikataba ya kazi mwisho wa siku ndio inaamua kila kitu mikataba ya kazi bongo ni ya kimagumashi tupu 90% haina vipengere kama hivi vinavyozungumzia majanga kama COVID 19 n.k
Hahaaaaa Dalali by Passion..
kuna hali gani huko dalali mwenzangu?
 
No production, no income.. Ni vyema serikali ikazipatia bailouts shule za binafsi kwa kuzikopesha kiasi cha pesa kitakachotosha kuwalipa wafanyakazi wake kiasi cha mshahara kisichozidi 75% ya mishahara yao na shule hizo kupewa miezi 60 ya kurejesha fedha hizo za Bailout.
Serikali ina mambo mengi tuionee huruma jamani.!
 
Bado nauliza wewe ungekuwa mwajiri ungefanyaje ?

Wafanyakazi ni kama assets, au kwa mfano mwingine ukiwa kwenye bahari jahazi lako likapigwa na dhoruba ikabidi uanze kupunguza mizigo kwenye mashua yako utaanza kupunguza zile mali unazoona you can live without (huenda hao foreigners ni muhimu zaidi kwake) au kama ulivyosema angefukuza hao foreigners huenda lawsuits n.k. zikapelekea shule ikafirisika..., kwahio ni bora kupumzika mwezi bila mshahara au kuendelea kuwalipa wote kwa mwezi na mwisho wa siku kila mtu kukosa kazi ? Na maji yakizidi unga na hao foreigners wataguswa.., na ikizidi kuwa mbaya wote wataguswa hadi panya waliokuwa wanadokoa chakula jikoni... (by the way huenda ameanza kujigusa yeye mwenyewe kwa kuweka rehani mali zake zote na kukopa mpaka kwa ndugu jamaa na marafiki)

Narudia tena ungekuwa wewe mwajiri ungefanyaje ?

Ushauri wako unaukweli kidogo. Lakini walimu wa Kitanzania katika shule hizi almost ni watumwa katika nchi yao. Walimu hawa ni professional wazuri sana (hakuna international school inayochukuwa walimu wenye uwezo mdogo) ukilinganisha na wageni ambao wengi wao wanajua lugha vizuri, kidogo au ya kuunga unga. Mishahara ya hawa wageni ni mikubwa mno na wanamazingira mazuri ya kazi kuliko wabongo wabebao mzigo mkubwa wa kuwanufaisha kwa mapato makubwa yatokanayo na karo kubwa za wanafunzi. Mfano mwalimu mtanzani graduate katika shule hizi mshahara tsh 500,0000/-+zero allowance, wakati mwalimu wa kigeni analipwa tsh 4,000,000.00 na zaidi + house& transport allowances nk. Karo ya mwanafunzi mmoja katika mashule haya iko juu sana (mwl atusaidie makadrio) uwiono uko wapi hapa?

Je kama ni kubana matumizi kwa nini wasianze na hawa wageni wenye mishahara mikubwa au wote wahusishwe?

Kama tumemwelewa mwalimu vizuri, mara baada tu ya tangazo la kufunga shule (chini ya mwezi mmoja) mwajiri naye anatangaza kutowalipa mishahara wa kitanzania tu kwa kisingizio cha corona!!

Je wakati wa likizo walimu huwa hawalipwi na wanafunzi hawajalipa karo? Likizo ulikuwa ni lazima hata bila corona na wanafunzi wamwlipa karo tayari.

Wakati umefika serikali ichukuwe hatua dhabiti kuwaokoa walimu hawa wa hizi international schools, nk..

Waajiri tuache fikra za kudhani kuwa wageni tu ndio wawezao kufanya kazi kwa ufasaha hata watanzania wanaweza sana.

Ndugu zangu walimu hawa ni watanzania na ndugu zetu, tuwasikilize na kuwasaidia kupaaza sauti zao maana ni kweli wananyanyaswa.
 
Naandika kwa niaba ya rafiki:

Ninafanya kazi kwenye moja ya international schools Dar es Salaam. Agizo la waziri mkuu kwamba shule zifunge lilipotoka tulianza likizo na mwezi wa tatu tulilipwa, tulikua tukifundisha kutokea nyumbani.

Sasa week iliopita mwajiri aliandika ujumbe kwa baadhi ya wafanyakazi, Watanzania tu (Wageni hawajaguswa) kuwa shule inajiendesha kwenye mazingira magumu na hasara, kwamba wanafunzi waliotakiwa kulipa ada hawajalipa na gharama za uendeshaji ni kubwa hivyo anatuomba tuchukue likizo bila malipo hadi hapo serikali itakapotanganza kufunguliwa kwa shule tena.

Na kwamba tutarejea kwenye nafasi zetu na tutaendelea na mikataba yetu. Tukajaribu kuhoji kwamba ni uamuzi wa gafla sana na sijajiandaa, mwajiri akasema au kuchukua option ya kukaa pending au kuacha kazi kabisa. Na jana ametuma mkataba wa kukubaliana kuchukua likizo isiyo na malipo(hatujakubaliana ni maamuzi tu tuliletewa tuyajue).

Naomba ushauri wa kisheria, makataba wangu unatakiwa kuisha mwakani mwezi wa tisa.
MWAMBIE atume taarifa zake kwenye uongozi wa Chama cha Walimu Shule Binafsi contact zinapatikana kupitia tovuti www.tptu.or.tz
 
Huu ni ubaguzi dhahiri. Tatizo ni kuwa mfanyakazi anaweza kudai sheria ichukue mkondo wake na akashinda lakini haina maana atapata haki. Ni kwa sababu sheria si sawa na haki. Ni vitu viwili tofauti - law and justice vitu tofauti
 
Back
Top Bottom