Mikopo Chefuchefu
JF-Expert Member
- May 15, 2017
- 3,373
- 6,795
Kwa akili za kawaida tu mkuuNaandika kwa niaba ya rafiki:
Ninafanya kazi kwenye moja ya international schools Dar es Salaam. Agizo la waziri mkuu kwamba shule zifunge lilipotoka tulianza likizo na mwezi wa tatu tulilipwa, tulikua tukifundisha kutokea nyumbani.
Sasa week iliopita mwajiri aliandika ujumbe kwa baadhi ya wafanyakazi, Watanzania tu (Wageni hawajaguswa) kuwa shule inajiendesha kwenye mazingira magumu na hasara, kwamba wanafunzi waliotakiwa kulipa ada hawajalipa na gharama za uendeshaji ni kubwa hivyo anatuomba tuchukue likizo bila malipo hadi hapo serikali itakapotanganza kufunguliwa kwa shule tena...
Hahaaaaa Dalali by Passion..Hii ishu imeikumba mataifa mengi hata kule kwenye upande wa soka La Liga kuna kesi kama hizi,ila uzuri mikataba ya kazi mwisho wa siku ndio inaamua kila kitu mikataba ya kazi bongo ni ya kimagumashi tupu 90% haina vipengere kama hivi vinavyozungumzia majanga kama COVID 19 n.k
Kama kawa!!Hahaaaaa Dalali by Passion..
kuna hali gani huko dalali mwenzangu?
Serikali ina mambo mengi tuionee huruma jamani.!No production, no income.. Ni vyema serikali ikazipatia bailouts shule za binafsi kwa kuzikopesha kiasi cha pesa kitakachotosha kuwalipa wafanyakazi wake kiasi cha mshahara kisichozidi 75% ya mishahara yao na shule hizo kupewa miezi 60 ya kurejesha fedha hizo za Bailout.
Bado nauliza wewe ungekuwa mwajiri ungefanyaje ?
Wafanyakazi ni kama assets, au kwa mfano mwingine ukiwa kwenye bahari jahazi lako likapigwa na dhoruba ikabidi uanze kupunguza mizigo kwenye mashua yako utaanza kupunguza zile mali unazoona you can live without (huenda hao foreigners ni muhimu zaidi kwake) au kama ulivyosema angefukuza hao foreigners huenda lawsuits n.k. zikapelekea shule ikafirisika..., kwahio ni bora kupumzika mwezi bila mshahara au kuendelea kuwalipa wote kwa mwezi na mwisho wa siku kila mtu kukosa kazi ? Na maji yakizidi unga na hao foreigners wataguswa.., na ikizidi kuwa mbaya wote wataguswa hadi panya waliokuwa wanadokoa chakula jikoni... (by the way huenda ameanza kujigusa yeye mwenyewe kwa kuweka rehani mali zake zote na kukopa mpaka kwa ndugu jamaa na marafiki)
Narudia tena ungekuwa wewe mwajiri ungefanyaje ?
MWAMBIE atume taarifa zake kwenye uongozi wa Chama cha Walimu Shule Binafsi contact zinapatikana kupitia tovuti www.tptu.or.tzNaandika kwa niaba ya rafiki:
Ninafanya kazi kwenye moja ya international schools Dar es Salaam. Agizo la waziri mkuu kwamba shule zifunge lilipotoka tulianza likizo na mwezi wa tatu tulilipwa, tulikua tukifundisha kutokea nyumbani.
Sasa week iliopita mwajiri aliandika ujumbe kwa baadhi ya wafanyakazi, Watanzania tu (Wageni hawajaguswa) kuwa shule inajiendesha kwenye mazingira magumu na hasara, kwamba wanafunzi waliotakiwa kulipa ada hawajalipa na gharama za uendeshaji ni kubwa hivyo anatuomba tuchukue likizo bila malipo hadi hapo serikali itakapotanganza kufunguliwa kwa shule tena.
Na kwamba tutarejea kwenye nafasi zetu na tutaendelea na mikataba yetu. Tukajaribu kuhoji kwamba ni uamuzi wa gafla sana na sijajiandaa, mwajiri akasema au kuchukua option ya kukaa pending au kuacha kazi kabisa. Na jana ametuma mkataba wa kukubaliana kuchukua likizo isiyo na malipo(hatujakubaliana ni maamuzi tu tuliletewa tuyajue).
Naomba ushauri wa kisheria, makataba wangu unatakiwa kuisha mwakani mwezi wa tisa.