Wakati serikali iko katika mchakato wa uhakiki pamoja na maboresho ya mishahara kwa watumishi wa umma ningependa kuchangia kidogo juu ya haya makundi mawili tajwa ya watumishi wa umma.
Nianze tu kwa kusema hapa duniani hakuna mshahara unaotosha na ndio maana watumishi wanajiongeza kwa kufanya shughuli mbali mbali ili maisha yaende na mkono uende kinywani lakini katika makundi haya mawili ya watumishi mishahara yao ni midogo sana kulinganisha na wenzao wa taasisi na mashirika ya umma.
Mfano mdogo tu chukulia watumishi wenye elimu sawa ya shahada ya sheria na linganisha kati ya mwanasheria wa halmashauri na mwanasheria wa taasisi kama TPDC, TANROAD au mifuko ya hifadhi unaweza kuona hawa wengine wanamzidi mshahara mwenzao wa halmashauri kwa zaidi ya 200% ingawa wote walisoma miaka 4.
Hii ilitokana na hizi taasisi kuwa na loophole ya kujipangia mishahara kitu ambacho ni tofauti kwa watumishi wa serikali kuu na tamisemi hii inapelekea kuwa na tabaka kati ya watumishi na pia watumishi kuhama kwenda kufuata malipo mazuri kwenye taasisi mbalimbali.
sio kitu cha kushangaza kumwona afisa utumishi au muhasibu wa halmashauri kapanga foleni akisubiri interview ya kazi kwenye mifuko ya hifadhi au taasisi za umma. Na pia sio kitu cha kushangaza kuona daktari aliyesoma kwa miaka 5 na intership 1 jumla 6 kuzidiwa mshahara na katibu mukhtasi/secretary mwenye diploma ya miaka 2 anayefanyia kwenye taasisi X ya umma.
Wito wangu kwa serikali kusiwe na tofauti kubwa sana ya malipo kati watumishi wa serikali kuu, tamisemi na taasisi za umma.
Sisi wote ni watoto wa baba mmoja na kazi yetu ni kuwatumikia watanzania nawote tunazalisha kwa namna tofauti.
Nawasilisha.