Mishahara ya rais na wabunge yapunguzwa Kenya

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Tume ya mishahara na marupurupu ya watumishi wa umma nchini Kenya imetangaza kupunguzwa kwa mishahara ya maafisa wakuu wakiwemo rais na wabunge.

Mwenyekiti wa tume hiyo Bi Sarah Serem ametoa mpangilio mpya wa malipo ambao anasema utaokoa jumla ya Sh8 bilioni (dola 80 milioni za Marekani) kila mwaka na kupunguza jumla ya mishahara inayolipwa watumishi wa umma kwa asilimia 35 .

Tume hiyo imependekeza kufutiliwa mbali kwa marupurupu ya kipimo cha usafiri wa magari kwa magavana na wabunge na badala yake hilo litakuwa likifidiwa na mfumo mpya wa marupurupu kwa kuzingatia kanda.

Rais sasa atakuwa akilipwa Sh1.4 milioni kila mwezi badala ya Sh1.5milioni, naye naibu wake awe akilipwa Sh1.2 milioni.

Mawaziri watakuwa wakilipwa Sh924,000, Spika wa Bunge Sh1.1milioni nao magavana wa kaunti Sh924,000. Mabadiliko hayo yataanza kutekelezwa tarehe 8 Agosti, 2017.

Bi Serem amesema maafisa wa serikali walikuwa wakitumia vibaya mfumo wa marupurupu wa kupimiwa usafiri wa magari. Badala yake, maafisa sasa watakuwa wakilipwa marupurupu ya kila mwezi ya usafiri kwa kutegemea eneo anamotoka afisa husika.
Magavana na manaibu wa magavana pia hawatakuwa wakilipwa tena marupurupu.

Wabunge, ambao wamekuwa wakilipwa marupurupu kwa kuhudhuria vikao vya kamati mbalimbali, pia watakosa marupurupu hayo. Viongozi wa serikali ya upinzani bungeni, ambao pia walikuwa wakipokea marupurupu ya majukumu maalum pia hawatalipwa tena marupurupu hayo.

Mishahara hiyo mipya itaanza kutekelezwa baada ya uchaguzi mkuu wa Agosti.
Maafisa ambao mihula yao haitakuwa imemalizika mwaka huu wataendelea kupokea mishahara yao ya awali. Hata hivyo, watakaorithi nyadhifa hiyo watalipwa kwa kufuata utaratibu mpya.

Mishahara mipya:

  • Rais: Sh. 1.4 milioni kutoka Sh 1.65 milioni
  • Naibu Rais: Sh. 1.2 milioni kutoka Sh. 1.4 milioni
  • Mawaziri: Sh. 924,000 kutoka Sh. 1.056 milioni
  • Makatibu wa Wizara: Sh. 765,000 kutoka Sh. 874,000
  • Magavana: Sh. 924,000 kutoka Sh. 1.056 milioni
  • Wabunge: Sh. 621,000 kutoka Sh. 710,000
  • Maspika: Sh. 1.155 milioni kutoka Sh. 1.30 milioni
  • Naibu Spika: Sh. 924,000 kutoka Sh. 1.006 milioni
  • Viongozi wa Serikali na Upinzani Bungeni: Sh. 765,000 kutoka Sh. 1.020 milioni
  • Madiwani (Wawakilishi wa Wadi): Sh. 144,000 kutoka Sh. 165,000
  • Mawaziri wa Serikali za Kaunti: Sh. 259, 875 kutoka Sh. 350,000


Chanzo: bbc swahili
 
Ndo inavyo takiwa kwann ifichwe

Sent from my TECNO-W3 using JamiiForums mobile app
 
Mishahara mikubwa kwa vigogo Kenya ndo chanzo cha migomo kwa wafanyakazi wengi wa umma

A person who says something is impossible should not interrupt the person who is doing it.
 
Halafu ya kwenu muwe mnaweka hadharani na kuanika, mishahara kwetu inaratibiwa na tume huru.
Wazo zuri! Ila hyo tume yenu nayo ina makengeza.

A person who says something is impossible should not interrupt the person who is doing it.
 
Huku kwetu ukiuliza usishangae kuitwa mchochezi

Sent from my HTC One using JamiiForums mobile app
 
Mtukufu wetu alisema atatoa wake hajatoa hadi leo
 
Kumbe wakenya mishahara ya viongozi wenyu inaanikwa hadharani?

Tz hatujui sisi.
Wakenya wanatupiga gap sana tu!! Kuanzia kwa watawala mpaka kwa sisi raia, wenzetu wako vizuri. Hapa kwetu jamaa mmoja alijitapa eti ataweka kadharani salary slip yake mpaka kesho hajawahi kusema tena!!
 
Wakenya wanatupiga gap sana tu!! Kuanzia kwa watawala mpaka kwa sisi raia, wenzetu wako vizuri. Hapa kwetu jamaa mmoja alijitapa eti ataweka kadharani salary slip yake mpaka kesho hajawahi kusema tena!!
....Mkuu unayajua yale masaa 48 ya Ma DC & Ma RC? Halafu kuna yale ya kanda maalum...
 
Sanaaaaa
Wanasubiri uchaguzi kuuza show

Sent from my HUAWEI P8max using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…