Breakdown............
Bei ya Mafuta katika vituo vya mafuta ni kati ya shilingi 1,200 kwa jiji la Dar es Salaam na shiling 1,500 kwa mji wa Musoma, Mbunge amekuwa akipata lita moja ya mafuta kwa shilingi 2,500 ikiwa ni shilingi elfu moja juu zaidi kwa gharama ya Musoma ambayo ni mji wenye bei ya juu ya mafuta aina ya petroli.
Kama hiyo haitoshi, Mbunge mmoja anapatiwa Lita 1,000 za mafuta kila mwezi ambapo kiasi hicho ni sawa na Sh 2,500,000. Licha ya fedha hizo, kila Mbunge sasa anapewa asilimia 40 ya fedha hizo kwa ajili ya matengenezo ya magari yao, kiasi ambacho ni sawa na Sh 1,000,000.
Kiasi hicho cha fedha ni mbali na Sh 765,000 kwa ajili ya matumizi ya ofisi yake kwa mwezi, na pia anapatiwa mshahara wa dereva kiasi cha Sh 100,000 kila mwezi.
Malipo haya hayaisihii hapo, bali mbunge sasa anapata Sh 300,000 kama posho kwa ajili ya dereva wake kila mwezi kwa ajili ya kutembelea jimbo. Kwa maana hiyo dereva wa Mbunge anapaswa kulipwa Sh 400,000 kila mwezi kutoka kwa Mbunge.
Mbunge pia anapewa kiasi cha Sh 45,000 kila siku kwa muda wa siku 10, ambapo anapaswa kutumia fedha hizo kutembelea jimbo kila mwezi. Kwa ajili ya kazi hii jumla anapewa Sh 450,000 kila mwezi kwa ajili ya kutembeelea jimbo.
Mshahara wa mbunge nao umeogezeka sasa kutoka Sh 1,200,000Sh 1,800,000. Jumla kwa mwezi Mbunge anapata Sh 6,915,000 kutoka serikalini.
Magari hayo wanayoendesha wabunge kila miaka mitano huwa wanakopesha Sh 40,000,000 kwa ajili ya kununua gari analotumia kwa muda wote wa miaka mitano anayokuwa bungeni.
Hata hivyo, wabunge wanapata mafao zaidi ya hayo kwani kwa muda wanaokuwa bungeni hupata posho za vikao kwa wastani wa Sh 100,000 kila siku na hiyo haiesabiki katika sehemu ya malipo yaliyotajwa hapo juu.
Bunge linalipa $ 7,000 kila mwezi kwa ajili ya nyumba anayoishi Spika wa Bunge, Samwel Sita. Nyumba ipo Masaki. Nyumba iliyokuwapo awali, ilinunuliwa na Spika wa Bunge aliyemaliza muda wake, Pius Msekwa.