Baada ya hayo matamshi ya Pinda, ninahamu ya kujua manesi, polisi, walimu watamwambia nini. Watanywea au watamtolea uvivu?
Pinda sio tu kwamba haelewi bali hajui wala hafahamu. Tatizo hapa sio kwamba hiyo mishahara ya wabunge ni mikubwa bali ni mikubwa mno ukilinganisha na mishahara ya wafanyakazi wengine wa serikali. hasa madaktari, waalimu, polisi, jeshi, na watumishi wengine wengi serikalini.
Vile vile haina uwiano na mapato ya nchi na haizingatii maisha ya mtanzania wala pato halali la mtanzania. sasa kama mbunge hawezi kuishi kutokana na pato la nchi kweli ataweza kuwa na fikra za kuisaidia nchi yake. Hili ni tatizo la watu kugeuza siasa ndio ajira.
Pale wanapo fanya utafiti wa mishahara yabunge wakilinganisha na lile la uingereza nafikiri tunaona jinsi gani bunge limekuwa la kifisadi. bunge na wabunge wameamua kumfanyia mwananchi ufisadi kwenye kodi zake.
Ama kweli kila kitu chini ya jua ni ubatili mtupu.Ubatili ubatili mtu.
Sioni sababu gani , Polisi, wanajeshi, waalimu, madaktari,manesi,nk wasigome kudai nyongeza ya mishahara kwani wanayolipwa huwezi kuishi hata wiki moja. Waitishe migomo ya kitaifa kudai nao walipwe angalau robo ya mishahara ya wabunge wao na kuzingatia hali halisi ya maisha ya tanzania na bei na mifumoko yake.
Pinda nae anataka apate cheap support kwa wabunge wenzake ambao wana uchu sana na wameweka tamaa mbele kuliko uzalendo.aruhusu basi na mashangingi yanunuliwe maana hakuna sababu kuzuia mashangingi then unawalipa wabunge 12m kwa mwezi......unaacha nini unafanya nini?Pinda unatuzingua.
My take
Hivi ni kweli Pinda ni mtoto wa mkulima?
Ameacha kutetea mishahara ya watumishi wa ngazi za chini ambao maisha yao yamekuwa ya kukopa kopa na mshahara unaishia kulipa madeni ya mwezi uliopita..watumishi hawa ambao kwa kweli wanaishi maisha ya hali ya nchi sana kulingana na mishahara wanayo pata serikalini kama walimu,manesi,polisi na wengine neo.
Pinda umeshindwa kuwatetea hawa wanyonge umeamua kutetea ulaji wa tumbo lako,hivi haya mamilioni mnayo pewa kwa mwezi ukigawa utawalipa walimu wangapi kwa hiyo milioni 7? kwa mshahara wa 200,000/= naamini Pinda umepotoka na nina amini wewe sasa ni mtoto wa Bepari si mkulima tena.
Inamaanisha kazi ya siasa ni ya ufanisi zaidi na ya kuthaminiwa kuliko ya Professionals, haya yanaitwa matusi ya nguoni, na inasikitisha wasomi wa tanzania ni mabwege kama watu walio vijijini, kuanzia Ma-lecturer wa chuo kikuu ambao hutufundisha sisi, na ndio kioo cha jamii. Watu kama Akina Makamba ndio wanatuongozo na kutuibia, na sisi tunapiga makofi.Pinda sio tu kwamba haelewi bali hajui wala hafahamu. Tatizo hapa sio kwamba hiyo mishahara ya wabunge ni mikubwa bali ni mikubwa mno ukilinganisha na mishahara ya wafanyakazi wengine wa serikali. hasa madaktari, waalimu, polisi, jeshi, na watumishi wengine wengi serikalini.
Vile vile haina uwiano na mapato ya nchi na haizingatii maisha ya mtanzania wala pato halali la mtanzania. sasa kama mbunge hawezi kuishi kutokana na pato la nchi kweli ataweza kuwa na fikra za kuisaidia nchi yake. Hili ni tatizo la watu kugeuza siasa ndio ajira.
Pale wanapo fanya utafiti wa mishahara yabunge wakilinganisha na lile la uingereza nafikiri tunaona jinsi gani bunge limekuwa la kifisadi. bunge na wabunge wameamua kumfanyia mwananchi ufisadi kwenye kodi zake.
Ama kweli kila kitu chini ya jua ni ubatili mtupu.Ubatili ubatili mtu.
Sioni sababu gani , Polisi, wanajeshi, waalimu, madaktari,manesi,nk wasigome kudai nyongeza ya mishahara kwani wanayolipwa huwezi kuishi hata wiki moja. Waitishe migomo ya kitaifa kudai nao walipwe angalau robo ya mishahara ya wabunge wao na kuzingatia hali halisi ya maisha ya tanzania na bei na mifumoko yake.
Pinda anajichanganya mwenyewe, wafanyakazi wengine wa serikali wanatakiwa wangunge mikanda, Wabunge mishahara haiwatoshi. PINDA vipi tena wewe si ndio ulikuwa unajiita mtoto wa mkulima??? Leo unatuambia Milioni 7 wanazozipata wabunge haziwatoshi kwa kukaa bungeni na wengi wao wakiwa wanasinzia. Kweli 2010 ndio hiyo kila mtu anatafuta staili yake ya kutoka.
Wewe unamzungumzia pinda Yupi? aliyesema ni mtoto wa mkulima ni yule pinda ambaye alikuwa bado hajaapishwa! baada ya kuapishwa siyo mtoto wa mkulima tena. Ni mwenzao na wao. Ni huyu huyu ambaye huwa anasema serikali haina pesa!!
PINDA, hebu angalau uvae viatu vya walimu, polisi,na wakulima wa jembe la mkono kule kijijini ulikotoka - yaani kodi wanayoporwa kwenye vijishahara/vijipato vyao vidogo namna hiyo ndiyo mjiongezee mishahara hivyo!
muwe na angalau chembe ya huruma kwa mwananchi
Kwa kazi gani wanayoifanya hao Wabunge mpaka mishahara yao haitoshi? Wanakutana kwa vikao vya Bunge kwa miezi isiyozidi minne na miezi mingine zaidi ya minane wanafanya uzururaji tu. Namuunga mkono Dr Slaa kwamba mishahara na marupurupu ya Wabunge ni mikubwa mno na inastahili kupunguzwa kwa kiwango kikubwa na savings zipelekwe kwenye mishahara ya Walimu, polisi, madaktari na polisi.
Wapewe tu, mbona wenzao wa UK wanalipwa Pound 64,766/= kama Tsh 127,893,795.80 bila kodi na ukizingatia hili ni Bunge la kuigwa mfano na ni la Commonwealth.