geofreyngaga
JF-Expert Member
- Sep 7, 2014
- 658
- 946
Ni Rais wa Bolivia SIO Uruguay.Anaitwa Evo Morales.Huyu amepiga panga mshahara wake ili iingie kwenye miradi ya maendeleo.
analipwa mil 404.27 jiulize nimejuaje
Hapo na Mimi sielewi? Ni nani anayepanga mishahara ya hawa watu?Mwaka jana Mbeki aliongezewa kutoka Rand 1.18 milioni hadi rand 1.27 milioni ingawa Tume ya Moseneke ilipendekezwa alipwe rand 1.89 milioni. Rais Kibaki alikataa nyongeza ya 186% ambayo inasemekana ingemtoa kutoka US$ 10,000 kwa mwezi hadi US$ 27,600 na marupurupu ya US$ 18,600. Sisi wa kwetu analipwa ngapi? Na nani anayeamua kiasi gani anastahili?
Mkuu, hii thread umeianzisha mwaka 2007 mi nikiwa kidato cha kwanza mpaka leo karibia 2016 naelekea kuhitimu masomo ya chuo na bado umeikazania.!! loh...huu ni mfano bora sana kwangu wa namna mtu anakiwa kufuatilia jambo. Hongera na pole kwamba bado hujafanikiwa kufahamu unachokitaka.Hiyo thread nimeshaiona na nimeshatoa mchango wangu kwa njia ya swali.
Yeye kusema/ kuandika kuwa mshahara wa rais ni shilingi milioni 32 bila kuweka source ya uhakika na ya kuaminika haifanyi mshahara wa rais kuwa shilingi milioni 32.
Hata mimi hapa sasa hivi naweza kusema kuwa 'mshahara wa rais Kikwete ni shilingi milioni 128 kwa mwezi'.
Je, watu wakiona nimeandika hivyo ndo wachukulie hiyo kauli yangu kuwa neno la injili bila kuhoji nilipoitoa hiyo taarifa?
Saying it so doesn't make it so.
Hebu hapo ulipo jaribu ku Google mshahara wa rais wa Marekani, Kenya, Afrika Kusini, au ule wa waziri mkuu wa Uingereza uone hits utakazopata.
anapokea kiasi gani?Hbr wakuu!? Nijuavyo rais wa Tanzania ni kati ya marais wanaopokea mishahara Mukibwa Dunia, Sana naomba Magufuli nae ajitumbue kwa kupunguza Mshahara wake!!
Alafu eti kima cha chin cha mshahara ni laki tatu!!!
Kumlipa rais dola 192,000 ni uendawazimu kwa nchi kama Tanzania, kazi gani anayofanya hadi alipwe hivyo?