Mishahara ya wabunge, mawaziri na majaji juu!

Akili Unazo!

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2009
Posts
3,930
Reaction score
4,912
Mishahara ya wabunge,mawaziri na majaji imepandisha huku wa spika wa bunge ukipanda mara dufu.
Kwa kifupi tu;

Spika na Jaji mkuu Tshs 2,760,000/= mpaka 4,850,000/=
Naibu spika Tshs 2,080,000/= mpaka 2,172,000/=
Mbunge Tshs 1,840,000/= Mpaka 1,921,000/=
jaji wa mahaka kuu tshs 2,160,000/= mpaka 3,645,000/=
jaji Mahakam ya rufaa Tshs 2,310,000 mpaka 4,250,000/=

Wakuu ninchoomba kuelewesha inamaana kwa kuwa spika ni mbunge kwa hiyo anakula na mishahara mingine ya ubunge au?

Kwa hali hii kweli tutapona?
Source:Mwananchi news paper la leo
 
Hii serikali hata siielewi kabisa hivi hizi taarifa zinapomfikia mhangaikaji, mkulima inamtia majonzi na uchungu kiasi gani? We need a change.......
 

Source: Mwananchi Date:8/25/2009
 
Hili ndilo changa la macho la Ari mpya kasi mpya na nguvu mpya kwa wadanganyika. Wengi walipe kodi wachache wafaidi matunda ya Uhuru. Unyonjaji wa mtandao wa SISIEM na maisha bora kwa wote. Silaha ya iliyobaki kwa wanyonge ni kuikataa SISIEM mwakani.
 
Ofisa wa serikali mwenye masters anaanza kazi na TGSD 3 ambayo gross is less than 450,000/= net around 300,000/= halafu eti uniambie asipokee rushwa na kula dili za juju kwa juu!!! Hata kama kuna allowance na vikao but haitoshi kwa maisha ya gharama ya leo!!!!
 
Inauma sana mwalimu wa sec. mwenye Diploma anakula take home 170,000/= kwa mwezi hapo ana mke na watoto na ndugu wanamtegemea.
 
Inauma sana mwalimu wa sec. mwenye Diploma anakula take home 170,000/= kwa mwezi hapo ana mke na watoto na ndugu wanamtegemea.

mkuu kumbe wakuu wa mikoa na wilaya nao wamo!!.

Mkuu wa mkoa, ambaye anapata mshahara wa Sh2,172,000, sasa atalipwa Sh2,080,000 na mkuu wa wilaya amepandishiwa mshahara wake kutoka Sh1,840,000 hadi Sh1,921,000 kwa mwezi.
source
 
Mkuu hizo za hao walafi bado posho na malupu lupu na vikao visivyo vya lazima nimesahau na safari.
 
Inauma sana mwalimu wa sec. mwenye Diploma anakula take home 170,000/= kwa mwezi hapo ana mke na watoto na ndugu wanamtegemea.
Tena saaaaana. 170,000/= hiyo hiyo ale yeye mke na watoto, usafiri hiyo hiyo. Kweli tutafika namna hii? Wenyewe sasa wanapata mshahara milioni 4 halafu wanapewa lita 100 za mafuta ya magari yao kwa wiki n.k. Sisi wa chini ambao hata laki moja tu hatuifahamu sijui tutafika wapi?

Ngoja nianze kulia kama dakika mbili hivi. uwi, uwi, eeeh, eeeeeeeeeeeh. uuuuuh.
 
Mwal. Primary analipwa 150,000 kwa mwezi!
Nini Mwalimu,wazee walovunjiwa nyumba na mabomu mbagala wamepewa hundi za Tshs30,000/=kama malipo ya fidia ya uharibifu ulotokea.

Je,huu ni uungwana????
 
Jiulize mzee ana miaka 75 analipwa Tshs169,000/= fidia ya nyumba ilobomoka.
Je,atajenga nini na hiyo hela?
Kwanini hiyo mishahara wasikatw hawa jamaa wakajengewa tujumba kama tule twa magomeni kota ama ilala kota??

Kweli kazi ipo,...
 
Mh!! Sijui kama tutafika......Hao wabunge wanaoenda kupamba ufisadi kweli walipwe mahela yote hayo? Kazi ipo.
 
Where is justice and fairness ktk kutumia national cake??

Kwanini wanasiasa tu wafaidi hii cake??

Kwani ni dhambi kuamua kuwa mwal. katika shule za umma Tanzania??

Halafu basi usiambiwe: mishahara ya wenzetu visiwani ndo iko chini..yaani balaa!!
 
Mkuu wa mkoa, ambaye anapata mshahara wa Sh2,172,000, sasa atalipwa Sh2,080,000

Hesabu tatizo la kitaifa au wamepunguziwa mshahara?.
 
Hesabu tatizo la kitaifa au wamepunguziwa mshahara?.

1. Kama wamepunguziwa mishahara basi ingekuwa safi tu!

2. Hivi vyeo vya wakuu wa Wilaya bora tu vifutwe..hizi kazi wakurugenzi kule wilayani wanatosha..na hii pesa waongezewe waalimu!
 
Kama hiyo ndio mishahara yao KWELI ni midogo sana. Hebu jaribu kuulizia mishahara ya wafuatao uone ninalojaribu kulieleza hapa;
1. Gavana wa BOT,CAG
2. Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO,
3. Maafisa Watendaji Wakuu wa DAWASA, DAWASCO, EWURA, REA, SUMATRA, TCRA
4.Mkurugenzi wa TIC, PSRC
5. Uje pia kwenye Taasisi na asasi binafsi kama PSPF, LHRC, CTI uone watendaji wake wakuu wanalipwaje.
 
Nini Mwalimu,wazee walovunjiwa nyumba na mabomu mbagala wamepewa hundi za Tshs30,000/=kama malipo ya fidia ya uharibifu ulotokea.

Je,huu ni uungwana????

Duuh inaumaaaaaa! yaani unaweza fikiri tunaongozwa na mapunguani vile. Duuh kweli Serikari its a strange creature u can never think of what will strangely do next............
 
Hivi Ghasia wakati anawasilisha bajeti alisema alitangaza nyongeza hii?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…