Mishahara ya wabunge, mawaziri na majaji juu!

Mishahara ya wabunge, mawaziri na majaji juu!

mnasema walimu wa sekondari na msingi tu,mimi naomba kuuliza lecturer msaidizi analipwa kiasi gani?

MkamaP,

Mhadhiri Msaidizi sijui analipwa kiasi gani..ila atakuwa na Masters tayari..basi ni kati kati ya laki 7 hadi 1m! Kuna mtu aliniambia Full Prof. sasa analipwa kama 2.5m..3.0 m gross au zaidi bila marupurupu!

WanaJF mlioko Vyuo vya serikali..hebu mtuhabairishe!
 
MkamaP,

Mhadhiri Msaidizi sijui analipwa kiasi gani..ila atakuwa na Masters tayari..basi ni kati kati ya laki 7 hadi 1m! Kuna mtu aliniambia Full Prof. sasa analipwa kama 2.5m..3.0 m gross au zaidi bila marupurupu!

WanaJF mlioko Vyuo vya serikali..hebu mtuhabairishe!

Nashukur kwa dokezo lako,namimi naomba nitie msisitizo ktk maelezo yako kwa wana jf walio vyuo vya serikali tunaomba ufafanunuzi wenu.

Ili tuweke mambo sawa tu assume huyo mhadhiri msaidizi ana masters na hii iwe reference point.
 
Waeshimiwa mishahara juu,Mbagala waathirika na mabomu elfu 30 sawa na mifuko miwili ya sementi na mchanga je,tutarenoveiti vipi hiyo nyumba yenye kreki ama kweli kuna kazi kubwa ya kuyafikia maisha bora kwa kila mtanzania,hivi silikali yetu inatufundisha nini.
 
Sasa nyie mnaoshabikia siasa eti Zitto,Mwakyembe,Slaa N,k mbona hawakatai hiyo mishahara na marupurupu kama kweli wanapinga ufisadi?Nawaambieeni kuwa hao wote ni mafisadi tuuu,mimi machozi yananitoka nalia mungu eeeh,maamaaa,
 
Wakuu ninchoomba kuelewesha inamaana kwa kuwa spika ni mbunge kwa hiyo anakula na mishahara mingine ya ubunge au?

Kwa hali hii kweli tutapona?
Source:Mwananchi news paper la leo

YAANI WEWE UMEONA YA SPIKA...ACHENI WIVU WA KIJINGA UJAONA MAJAJI WANAVYOTOFAUTIANA KWANI WANAHUKUMU MAHAKAMA YENYE A/C NA ISIYO NA A/C AMA????

WACHE WALE MADHABAHUNI HAKI YAO...NA WEWE IBA UKO ULIKO UONGEZEWE MSHAHARA...UNAJUA KINACHOFANYA WATANZANIA NI WEZI....MISHAHARA MIDOGO NDIO MAAANA HTA WAKIMWONGEZEA MTU NAHSI HARUFU YA KIFISADI KUPUNNGUA
 
tukiamua tutafika, mbona uwezo tunao sisi wadaganyika tena bado miezi tu, jamani msisahau kununua picha ya Mh. ni 15,000 bila fremu lakini
 
Mishahara ya wabunge,mawaziri na majaji imepandisha huku wa spika wa bunge ukipanda mara dufu.
Kwa kifupi tu;

Spika na Jaji mkuu Tshs 2,760,000/= mpaka 4,850,000/=
Naibu spika Tshs 2,080,000/= mpaka 2,172,000/=
Mbunge Tshs 1,840,000/= Mpaka 1,921,000/=
jaji wa mahaka kuu tshs 2,160,000/= mpaka 3,645,000/=
jaji Mahakam ya rufaa Tshs 2,310,000 mpaka 4,250,000/=

Wakuu ninchoomba kuelewesha inamaana kwa kuwa spika ni mbunge kwa hiyo anakula na mishahara mingine ya ubunge au?

Kwa hali hii kweli tutapona?
Source:Mwananchi news paper la leo
Jamani naomba kujibiwa hili swali je kwa mkuu wa mkoa ambaye ni mbunge kwa hiyo anapokea mishahara miwili? ya ukuu wa mkoa na ubunge? Na je kama Rais ndie kiongozi mkuu serikalini na mwenyekiti wa chama tawala,amiri jeshi mkuu kwa ukubwa huu wa madaraka yeye kaongezewa kiasi gani?
 
Hesabu tatizo la kitaifa au wamepunguziwa mshahara?.

Bueray, cheki na hapa gazeti lilivyovurunda:


MWANANCHI
Waandishi Wetu


Habari zinadokeza kuwa majaji 70 wametengewa lita 100 za mafuta ya gari kwa juma, lita moja imekadiriwa kugharimu Sh1,500 hivyo kupewa Sh600,000 kwa wiki ambayo ni sawa na Sh504 milioni kwa mwaka.
Lita 100/wiki TIMES Sh 1,500/lita = Sh 150,000/wiki
Mwandishi kapata Sh 600,000 kwa wiki!

Sh 150,000/wiki TIMES wiki 52/mwaka = Sh 7,800,000/mwaka
Mwandishi kapata milioni 504!


 
1. Kama wamepunguziwa mishahara basi ingekuwa safi tu!

2. Hivi vyeo vya wakuu wa Wilaya bora tu vifutwe..hizi kazi wakurugenzi kule wilayani wanatosha..na hii pesa waongezewe waalimu!


Hali si Nchi ni mbaya na CCM haina la kufanya wanaogopa kuondoka madarakani .Kwanza kawapa washikaji wengi ujaji .Anajua makesi yenu ya Uchaguzi mwakani yataenda kwao na watayamaliza kirahisi na kuacha CCM inapeta .Wakuu wa Mikoa na Wilaya hawa Chadema walisema kuwe na majimbo ama Wakurugenzi wa Wilaya waendelee na kazi zao , lakini hizi n nafasi za asante kwa washikaji wakae wale na kuwalindia mambo yao .
 
Bueray, cheki na hapa gazeti lilivyovurunda:

Lita 100/wiki TIMES Sh 1,500/lita = Sh 150,000/wiki
Mwandishi kapata Sh 600,000 kwa wiki!

Sh 150,000/wiki TIMES wiki 52/mwaka = Sh 7,800,000/mwaka
Mwandishi kapata milioni 504!



Chukua kazi ya editor hapo. Or better yet, principal wa chuo cha habari.

Ningependa mtu kama huyu awe payroll huko, watu wangejibweda tu, unaona miziro inazidi tu katika account, lol!
 
mshahara wa rais ni shilingi ngapi?..........
naomba msaada...

Kama wa Judge ni huo basi unaweza kukisia wa Rais ni kiasi gani! Usisahau kwamba Rais mbali ya mshahara anayo marupurupu mengine ukiwemo 'Mfuko wa Rais' nadhani unaitwa 'Mfuko wa Rais wa Maendeleo' ambao nao una mahela yake ambayo anaweza kujichotea akatumia anavyoona inafaa!

"TANZANIA ITAJENGWA NA WENYE MOYO (KAMA BADO WAPO) ......."
 
Mishahara ya Wabunge, Mawaziri na Majaji yaongezwa
broken-heart.jpg
MSHAHARA WA SPIKA, JAJI MKUU WAONGEZWA MARADUFU

Waandishi Wetu

SERIKALI imewaongezea mishahara viongozi wa kisiasa, majaji, wakuu wa mikoa na wilaya kuanzia Julai mwaka huu, huku jaji mkuu na spika wakiongezewa maradufu.

Habari za uhakika zilizolifikia gazeti hili zimeeleza kuwa mshahara wa jaji mkuu na spika, ambao ni viongozi wa mihimili mikuu miwili ya nchi, umepanda kutoka Sh2,760,000 hadi Sh4,850,000 kuanzia mwezi Julai na ongezeko hilo ni sawa na asilimia 75.7

Kwa mujibu wa habari zilizothibitishwa na vyanzo mbalimbali vya habari kutoka mihimili yote ya dola, mshahara wa naibu spika umepanda kwa Sh92,000, kutoka Sh2,080,000 hadi Sh2,172,000 na mbunge kutoka Sh1,840,000 hadi Sh1,921,000, ikiwa ni ongezeko la Sh81,000 kwa mwezi.

Katibu wa Bunge Dk Thomas Kashilillah aliliambia gazeti hili mwishoni mwa wiki kuwa amesikia kuhusu nyongeza hiyo ya mishahara, lakini hana taarifa rasmi wala namna yoyote ya kuthibitisha, kwa kuwa mishahara hiyo haimuhusu.

"Viwango vya mishahara kwa viongozi wa serikali vinawekwa na serikali, mimi hainihusu hivyo siwezi kuthibitisha hilo. Nimesikia tu kama mlivyosikia ninyi," alisema Dk Kashilillah alipotakiwa na gazeti hili kuthibitisha ongezeko la mishahara ya wabunge.

Katika viwango hivyo vipya vya mishahara ambavyo Mwananchi imefanikiwa kuviona, jaji wa Mahakama Kuu ameongezewa mshahara kutoka Sh2,160,000 hadi Sh3,645,000, ikiwa ni ongezeko la Sh1,485,000 huku jaji wa Mahakama ya Rufaa ameongezewa Sh1,940,000 (kutoka Sh2,310,000 hadi Sh4,250,000).

Vyanzo vimeeleza kuwa mshahara wa waziri umepanda kwa Sh102,000 (kutoka Sh2,320,000 hadi Sh2,422,000) na mshahara wa naibu waziri umepanda kutoka Sh1,960,000 hadi Sh2,046,000, ikiwa ni ongezeko la Sh120,000.

Mkuu wa mkoa, ambaye anapata mshahara wa Sh2,172,000, sasa atalipwa Sh2,080,000 na mkuu wa wilaya amepandishiwa mshahara wake kutoka Sh1,840,000 hadi Sh1,921,000 kwa mwezi.

Vyanzo hivyo vya habari vimedokeza kuwa viwango hivyo vipya vya mishahara, havijumuishi posho za vikao, mafuta ya gari na fedha za kujikimu.

Habari zinaeleza kuwa jaji mkuu anapata posho ya madaraka ya Sh6 milioni kwa mwaka na jaji kiongozi anapata posho ya Sh3 milioni, kwa mujibu wa viwango hivyo vipya.

Majaji 70 wanapata posho ya simu na umeme inayofikia Sh 386,400,000 kwa mwaka na posho ya mavazi ya Sh35 milioni kila mmoja.

Habari zinadokeza kuwa majaji 70 wametengewa lita 100 za mafuta ya gari kwa juma, lita moja imekadiriwa kugharimu Sh1,500 hivyo kupewa Sh600,000 kwa wiki ambayo ni sawa na Sh504 milioni kwa mwaka.

Moja ya vyanzo vyetu vya habari kilidokeza kuwa nyongeza hiyo ni ya kawaida ambayo inaenda sambamba na nyongeza ya mishahara kwa watumishi wa umma, ingawa mwaka huu kwake imeonekana kuwa kubwa zaidi.

"Hili ni kweli; mishahara yetu imeongezwa kuanzia Julai, lakini sisi tulidhani ni nyongeza ya kawaida inayoenda sambamba na nyongeza ya mishahara ya watumishi wengine wa umma, lakini ukweli mambo ni mazuri zaidi," alisema.

Akiwasilisha hotuba yake kwa mwaka 2000/2010, waziri wa Nchi, ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa umma, Hawa Ghasia alisema serikali inatarajia kutumia Sh1,774 trilioni kugharamia mishahara kwa watumishi wa umma,

Fedha hizo pia zitatumika kulipa mishahara kwa watumishi waliopo kazini, ajira mpya, upandishaji vyeo watumishi, kulipia madai ya malimbikizo na mapunjo ya mishahara ya watumishi wa umma nchini.

"Serikali itaendelea kuhakikisha watumishi wake wanapandishwa vyeo na kurekebishiwa mishahara yao ipasavyo," alisema Waziri Ghasia wakati akiwasilisha makadirio ya wizara ambayo wabunge waliyapitisha bila marekebisho.

Suala la mishahara hiyo mipya limekuwa siri kubwa hasa ikizingatiwa kuwa wakati wa bajeti ya serikali ya mwaka huu, waziri mwenye dhamana hakuweka bayana viwango vipya vya mishahara ya watumishi wa umma.

Habari za uhakika zilizolifikia gazeti hili zilisema kuwa serikali hivi sasa iko katika mkakati muhimu wa kuboresha maslahi ya watumishi wa umma wenye taalumu ili kuzima wimbi la wasomi kukimbilia nyadhifa za kisiasa. "Katika miaka ya hivi karibuni tumeshuhudia madaktari na wanataaluma wengine wanaacha taaluma zao wanakimbilia ubunge kwa sababu anaona labda atateuliwa kuwa waziri na maslahi ni mazuri,。"kilidokeza chanzo chetu cha habari.
 
Dk. Slaa atabiri machafuko
• Kupanda mishahara ya vigogo

na Betty Kangonga
Tanzania Daima~Sauti ya Watu



amka2.gif

SIKU moja baada ya kupatikana kwa taarifa kuwa serikali imeongeza viwango vya mishahara ya mawaziri, wabunge na viongozi wawili wa mihimili ya dola, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willbrod Slaa ameionya serikali kuwa hatua yake hiyo inaweza kuleta machafuko nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, makao makuu ya CHADEMA, Dk. Slaa alisema hatua hiyo ya serikali kuweka tofauti kubwa ya mishahara ya watumishi wa serikali, wabunge na majaji inaweza kuzua matabaka yatakayosababisha machafuko nchini.
Alisema kuongezwa kwa viwango vya mishahara kwa watumishi hao, hususan wabunge ni ukiukwaji… na pia kuwaongezea mzigo wananchi ambao wana maeneo mengi yanayohitaji fedha, lakini hawazipati.
"Kama unaamua kuongeza kiwango cha mishahara kwa wafanyakazi si kwa kuwa unaongeza motisha kwao, lakini kutokana na mustakabali wa nchi kwa sasa kwani hali ya uchumi ni mbaya, hivyo jambo hilo linaweza kusababisha chuki kati ya wananchi na viongozi wao.
"Kitendo hiki cha kupandisha mishahara bila kuangalia hali halisi ya nchi, kinaweza kuleta migogoro kati ya wapiga kura na viongozi ambao baadhi yao, huenda wakapata wakati mgumu, hasa katika kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwakani," alisema.
Dk. Slaa ambaye pia ni Mbunge wa Karatu alieleza kusikitishwa na hatua ya serikali ya awamu ya nne kupandisha kiwango cha mishahara kwa baadhi ya viongozi, huku ikishindwa kuyatafutia ufumbuzi baadhi ya matatizo yanayowakabili wananchi wake.
Aliyataja masuala muhimu yanayohitaji kutafutiwa ufumbuzi kuwa ni pamoja na ukosefu na upungufu wa chakula, ukosefu wa pembejeo za kilimo na migogoro isiyoisha kwa baadhi ya makampuni.
"Kuna mambo mengi yanayohitaji pesa, wapo watu ambao hata mlo wao wa siku ni shida na hawajui watapata wapi chakula. Kwenye kampuni kadhaa migogoro ni kila kukicha, hii nayo inahitaji fedha, sasa serikali inashindwa kuangalia hayo na kubaki kumwongezea mtu aliyenacho," alisema Dk. Slaa.
Aidha, aliwataka viongozi kujali maslahi ya wananchi na kuachana na tabia ya kutaka kujilimbikizia mali, ikiwa ni pamoja na kukubali ongezeko kubwa la mishahara.
Alisisitiza kuwa hatua hiyo ni kushindwa kuwajibika ipasavyo kwa ajili ya wananchi waliowapa nafasi za kukaa katika nafasi walizonazo.
"Ni lazima ipatikane Tanzania isiyokuwa na matabaka, ambayo viongozi watakuwa na mishahara isiyopishana sana na wananchi wao, hapo serikali itafanikiwa kuondoa tofauti kubwa inayotaka kuingia kati ya aliyenacho na asiyenacho," aliongeza Dk. Slaa.
Suala la kupanda kwa mishahara ya viongozi wakiwemo wabunge, limekuwa siri kubwa ambayo wananchi hawatakiwi kuijua.
Hilo lilibainika katika mkutano wa Bunge la bajeti ambapo serikali ilishindwa kuweka bayana viwango vipya vya mishahara ya watumishi wa umma.
Katika hotuba yake ya bajeti ya mwaka 2009/2010, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Hawa Ghasia alisema serikali inatarajia kutumia sh trilioni 1,774 kugharamia mishahara kwa watumishi wa umma.
Alisema fedha hizo zitatumika kulipia mishahara ya watumishi waliopo kazini, ajira mpya, upandishwaji vyeo watumishi, kulipia madai ya malimbikizo na mapunjo ya mishahara ya watumishi wa umma nchini.
Habari zilizopatikana, zilieleza kuwa mshahara wa Jaji Mkuu na Spika wa Bunge umeongezwa maradufu kutoka sh 2,760,000 hadi sh 4,850,000 kwa mwezi kuanzia Julai, mwaka huu.
Viongozi wengine ambao mishahara yao imeongezwa ni pamoja na Naibu Spika wa Bunge kutoka sh 2,080,000 hadi sh 2,172,000 na mbunge kutoka sh 1,840,000 hadi sh 1,921,000 ikiwa ni ongezeko la sh 81,000 kwa mwezi.
Kwa upande wa Jaji wa Mahakama Kuu, sasa atalipwa sh 3,645,000 badala ya sh 2,160,000 huku Jaji wa Mahakama ya Rufaa akiwa ameongezewa sh 1,940,000 kutoka sh 2,310,000 hadi sh 4,250,000. Mshahara wa waziri umepanda kwa sh 102,000 kutoka sh 2,320,000 hadi sh 2,422,000 na Naibu Waziri kutoka sh 1,960,000 hadi sh 2,046,000 ambalo ni ongezeko la sh 120,000. Mkuu wa Mkoa kutoka sh 2,172,000 hadi sh 2,080,000 na Mkuu wa Wilaya kutoka sh 1,840,000 hadi sh 1,921,000 kwa mwezi. Viwango hivyo havijajumuishwa na posho za vikao, mafuta ya gari na fedha za kujikimu.
 
hizi ni dalili za kufunga midomo wabunge wakiongozwa na spika, wadau nipeni taratibu za kugombea ubunge, naona bora nikajaribu huko hapa nilipo hapalipi kabisa
 
Juzi tu tumeonyeshwa picha ya wanafunzi wamekaa chini hapo, waakina mama na watoto wanakufa vijijini kwa kukosa huduma za kujifungulia, usafiri n the like, eti wao they have guts za kujiongezea mshahara. haya ccm
 
Au kama vp kila mtu achukue chake mapema popote alipo.sasa tufanyeje bwanaaaaaaaaa! inauzi sana
 
Back
Top Bottom